Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

nunua videsktop viwili ufungue biashara ya kompyuta games kwa watoto
NB:kwa huku kwe2 uswazi lakini kama we wa mikocheni au pande zile zenye ikulu ndogondogo biashara itasanda mdau

Kaka Asakri wa miguu, naona nami umeniteka kidogo kwenye ushauri wako. Nami ningependa nifahamu zaidi kuhusu hizi computer games za watoto. Je unaweza kunifafanuilia ni nini hizi games na biashara yake ikoje kaka?
ASANTE kujibu
 
Uko Mkoa gani na unahitaji asilimia ngapi?Unaweza kuifanya mahali popote TZ.Mbona umemkasirikia huyo ndg ambaye kakushauri kuhusu biashara ya kucha,ushauri wa kwanza kwenye biashara mthamini hata anayekutukana ilimradi wewe upate faida au pesa la sivyo biashara ni ngumu ndg yangu.

Kama uko tayari kwenda vijijini ni PM nikupe biashara amabayo utapa kama 200,000 kwa mwezi kwa laki 3,ila ukubali kufanya kazi kwenye mazingira yoyote sio ya mjini tu.
 
Kama upo dar na unaweza kupata kasehemu ukaweka meza mtaani kama genge, iyo laki 3 unaweza kuanza kuuza karoti, ndizi, machungwa na nyinginezo za chakula. Bidhaa zako uzinunue mojakwa moja kutoka kwa mkulima. Wala si mbali, nenda apo Ruvu unapata mzigo wa kutosha. Huhitaji ela nyingi sana. Kumbuka tu kwamba laki inajengwa na elfu,milioni inajengwa na laki, nk.

Kwa uchache tu, kwa mfano saivi chungwa 1 wanauza sh. 30 shambani. Ukinunua gunia machungwa kama 1200) ni elfu 36 au tufanye 40 elfu. Weka usafiri kama elfu 10. Garama ya gunia unapata kama elfu 50.

Bei ya gengeni chungwa 1 ni sh. 200. Ukiuza 1200 unapata 1200x200=240,000. Ukitoa garama elfu 50, unabaki na faida ya sh. 190,000. Hiki ni kitu kimoja tu, bado hujaweka karoti. Nafikiri unajua bei ya karoti moja.

Kwa mtazamo wangu, huhitaji mtaji mkubwa ili utoke. Kidogo ulichonacho ukikusanya kwa malengo kitakua kikubwa. Usidharau iyo laki 3, inategemea unaipangilia vipi. Swala ni kujipangia muda tu na wewe kuwa tayari.

Mi nafahamu mtu aliyeanza kufanya biashara ya kuuza mifuko ya rambo Arusha miaka ya 1990 kwa bei ya rejareja, badae kaanza kusafiri kuchukua mifuko hiyo kutoka Zenji na kuiuza kwa jumla Aru. na nairobi, akaongeza biashara ya kuuza nguo, kwa sasa ana ghorofa kariakoo na anasafiri kwenda china kununua mali.
 
Hamjaelewa swala la vitafunwa..tafuta wadada wako wa uswazi wanaojua mapishi..andaa sample za andazi, chapati, tumbua au any breakfast bites..pitisha sample ktk restaurant or officeee za mjini.. utanambia..

But hii ni kama unainterest na mambo ya makulaji...ktk mandaz usiweke ile akili ya kupanga karai barabarani , hapana utafeli..aim big ndugu yetu...kila la kheri
 
Ubaya hii mijamaa ya restaurant inaajiri hao wadada-inataka kukamua mpaka senti ya mwisho ya mteja.

Kama unazijua si umpe some ideas? Ndg yangu,nimepata tender sehemu nitakupa order ya kila siku 7 upate 50,000 i.e 200,000 pm?
 
Uko Mkoa gani na unahitaji asilimia ngapi?Unaweza kuifanya mahali popote TZ.Mbona umemkasirikia huyo ndg ambaye kakushauri kuhusu biashara ya kucha,ushauri wa kwanza kwenye biashara mthamini hata anayekutukana ilimradi wewe upate faida au pesa la sivyo biashara ni ngumu ndg yangu.kama uko tayari kwenda vijijini ni PM nikupe biashara amabayo utapa kama 200,000 kwa mwezi kwa laki 3,ila ukubali kufanya kazi kwenye mazingira yoyote sio ya mjini tu.

Nimemshangaa sana huyu ndg anayejiita moyo wangu ameomba ushauri tena kuan sehemu alisema anataka kufanya biashara kuhusiana na vitu vidogo vidogo vya wanawake na mimi nikamshauri afanye biashara ya kutengeneza kucha na kupaka rangi wanawake nimeshangaa sana kwa yeye kuniambia niianze kwanza mimi hiyo biashara.

Kwa wale wote ambao hawajui hiyo biashara inalipa sana mi nawafahamu vijana wengi wanaofanya biashara hiyo sehemu za mijini na kwa siku wanapata zaidi ya elfu 30.

Na pia biashara hiyo mtaji wake haufiki 50,000/=. nadhani huyu jamaa haombi ushauri anafanya utani na mawazo ya watu. Any way naamini nilimpa ushauri mzuri na wala sikumziaki au kumtukana.
 
punguza masifa,hutafika popote!hebu hiyo 200m iandike kwa tarakimu kamili,sitoshangaa kukuta hujui hata ina sifuri ngapi?
Mwanajamvi mwenzangu mbona tunakashfiana! Naami nilimpa ushauri mzuri mwananchama mwezangu aliyeomba ushauri nashangaa sana akanijibu sivyo kwamba nikafanye mimi mwenyewe, nikamjibu ukweli mimi ninabiashara zangu ambazo ninazifanya za zaidi ya 200,000,000/= . sasana wewe sijui umetokea wapi unaanza kunikashifu. sijafurahishwa kabisa na kitendo chako kuwa mstaarabu DullyJr
 
Kwa pesa hiyo unaweza kufanya biashara ya vitumbua au mama niwekee.

Kweli ktk msafara wa mamba hata kenge hamkosekani mtu anakuja na uzi wa kutaka ushauri mzuri unamletea upumbavu angeweka uzi wa mmu ungemsapoti vikali kwa jambo lisilokuwa la msingi
 
Duka la chakula uswahilini linalipa sana kwani hata kodi ya nyumba si khali sana na ni vitu frequent demanded na kwahuo mtaji wako unatosha
 
Chips zinalipa mkuu,tafuta kijiwe tu
nataman kujiajiri mwenyewe..je mtaj wa 3 naweza kujiajir na biashara gani wana jf.?..naomben mawazo yenu kama mdogo wenu na ntayafanyia kaz mana naamin naweza na ipo siku i can mek it yes in my life...wazoefu wa biashara naombeni mawazo yenu naamin wote humu ni magrt thnker's na sitegemei majibu ya dharau mana clazma kila ukionacho ukoment nawe ujulikane upo..kama huna pita njia na waache wenye busara na upeo watuelimshe..ahsante
 
mwanajamvi mwenzangu mbona tunakashfiana! Naami nilimpa ushauri mzuri mwananchama mwezangu aliyeomba ushauri nashangaa sana akanijibu sivyo kwamba nikafanye mimi mwenyewe, nikamjibu ukweli mimi ninabiashara zangu ambazo ninazifanya za zaidi ya 200,000,000/= . sasana wewe sijui umetokea wapi unaanza kunikashifu. sijafurahishwa kabisa na kitendo chako kuwa mstaarabu DullyJr

Samahani kama nimekukwaza,ila kimantiki hukutumia mtiririko mzuri ktk kufikisha wazo lako kwa mlengwa,bali ni kumkatisha tamaa kwa tambo zako kuwa una msingi wa 200m,ningeona bora zaidi kama ungempa mtiririko umeanzaje mpaka ukawa na msingi huo nafikiri hiyo ingekuwa changamoto na hamasa kwake.

Kwa kuona hata yeye anaweza kufika huko ulipo!sasa unapokurupuka na kusema una msingi >200m,unakuwa unakatisha tamaa na kuidharau >300,000 yake!sijui kama umenipata vizuri ndugu yangu!
Narudia tena samahani kama jibu langu limekukwaza..habari ya asubuhi?
 
Habari wana jf,kwanza kabsa naandika uzi huu nikiwa na imani kwamba jf ni sehemu ambapo naweza kupata majibu ya busara na hekima na sio dharau na mizaha.back 2 da point,nina sh.laki moja hapa nlpo,na nmemalza form six na sina kibarua.

But nategemea km nitachaguliwa nitaenda chuo bt nna hakika mkopo kwangu unaweza kuwa ndoto due to my points,so nilikuwa nataka nikazungushe haka ka hela ili kaongezeke.Natanguliza shukran...jf 4ever.
 
Swali la namna hii limekuwa likiulizwa na wengi, kwani watu wengi wanashindwa kubaini fursa ya biashara; hata hapa unaweza usipate majibu sahihi kwa biashara ya kufanya kutokana na vigezo vya fursa ya biashara.

Fursa yeyote ya biashara inategemea na mahali ulipo na uhitaji katika eneo husika. Kwa kufuata vigezo vya fursa ya biashara; unatakiwa kuangalia mahitaji yanayokuzunguka katika eneo ulilopo kutokana na kiasi cha mtaji ulionao.

Kama upo Dar, unaweza kufanya biashara kuuza samaki wabichi au kukaanga katika eneo ulilopo au eneo ambalo hakuna biashara hiyo. Hii unaweza kufanya nyakati za asubuhi na jioni unaweza kuuza supu ya pweza. Hii ya supu ya pweza ndio iwe biashara kuu kwa kukuza mtaji wako. Utahitaji meza, jiko na vyombo; unaweza kufanya uchambuzi yakinifu juu ya hili kwa kwenda feri.
 
unaweza pia kuuza maji baridi barabarani,au kukaanga vitumbua kwenye stend za daladala mida ya jioni,na tangawizi.mtaji unatosha huo
 
Swali la namna hii limekuwa likiulizwa na wengi, kwani watu wengi wanashindwa kubaini fursa ya biashara; hata hapa unaweza usipate majibu sahihi kwa biashara ya kufanya kutokana na vigezo vya fursa ya biashara. Fursa yeyote ya biashara inategemea na mahali ulipo na uhitaji katika eneo husika. Kwa kufuata vigezo vya fursa ya biashara; unatakiwa kuangalia mahitaji yanayokuzunguka katika eneo ulilopo kutokana na kiasi cha mtaji ulionao.

Kama upo Dar, unaweza kufanya biashara kuuza samaki wabichi au kukaanga katika eneo ulilopo au eneo ambalo hakuna biashara hiyo. Hii unaweza kufanya nyakati za asubuhi na jioni unaweza kuuza supu ya pweza. Hii ya supu ya pweza ndio iwe biashara kuu kwa kukuza mtaji wako. Utahitaji meza, jiko na vyombo; unaweza kufanya uchambuzi yakinifu juu ya hili kwa kwenda feri.

nashukuru kwa ushauri wako ndugu yangu,by nw npo geita na ndio nataka kuizungusha hii pesa.
 
Kama wadau walitangulia kusema hapo juu, jaribu kuangalia sehemu ulipo nini kitu gani kinahitajika au huduma gani ambayo iko katika kiwango kibovu! Mfano kuuza vocha za simu, kukaanga karanga bila aibu unatoka; Lakini lazima ujiamini uache uoga, jaribu kuwa mbunifu weka majonjo ya hapa na pale. Kwa geita unaweza kuwa na kijiwe chako cha kuuzia hizo karanga au vocha au kitu kingine ambacho kitakuwa kinakuweka busy nyakati za asubuhi tu na jioni pia. Mchana unajipanga kikamilifu kwa ajili ya mashambulizi.
 
Back
Top Bottom