Kwa mlio oa naomba mwongozo tafathali

ENGINE CONTROL

Senior Member
Nov 20, 2011
136
27
Wanajamvi naomba kuelimishwa/fahamishwa juu ya hili.
Mim ni kijana mwenye umri wa miaka 26.Nimekaa zaidi ya 8 yrs bila kufanya mapenzi.Lakin kwa sasa ninampango wa kutafuta msicha wa kuoa.Mim najishughulisha na kazi ya ufundi wa umeme wa magari kipato changu ni chakawaida sana wastan kama wa 10 000 per day.
Je nivigezo vip ambavyo hustahili mwanaume kuoa?? Maana wengi nimekuwa nawasikia wakisema kuwa wataoa mpaka mambo yakiwa safi/wakiwa na fedha. Je ? kigezo hiki huwa kinamata sana??
naomba msaada wenu ni vigezo vipi vyakuzingatia /ua ukidhi ili uweze kuoa..
HAKUNA TENA JANDO KWA SIS VIJANA HIVYO JF NDO JANDO KWANGU.
 
Hivi wale vijana kule vijijini ambao hawana kipato kabisa hawao?.Cha muhimu muoe mwanamke ambaye ataridhika na hali uliyokuwa nayo na ole wako ujichanganye utajuta
 
bado hujapata wa kupendana naye! siku ukimpata haitajalisha unakipato kiasi gani!
 
Samahani kwa kuingilia wenye ndoa zao. . .

Nwy Kigezo muhimu kuliko vyote ni kumpata unaetamani/penda awe mkeo, nae uwe mumewe.
 
ndoa pasua kichwa.......... 8 yrs bila ku do........big up...we si govi kweli????
 
dogo cha muhimu sio kipato maana kinaweza kushuka au kupanda pindi uoapo cha muhimu jipange kama kijana wa kisasa mahitaji yote yawepo mfano kitanda.viti.fridge.tv.radio na nk ukisha kamilisha hivyo hapo ni kijana tayari kwa kuoa baada ya kuoa kuna mingalio yake unatakiwa ujue yafatayo ingawa watu wengi huwa hawayafati.1.kuna muda wa kuoa 2.muda wa kuzaa 3.muda wa kujenga 4 muda wa kusomesha watoto mambo nne haya ukiyaweka katika mipangilio maisha daima yatakuwa mazuri ila ukichanganya walio wengi mambo huwa hayaendi.
 
dogo cha muhimu sio kipato maana kinaweza kushuka au kupanda pindi uoapo cha muhimu jipange kama kijana wa kisasa mahitaji yote yawepo mfano kitanda.viti.fridge.tv.radio na nk ukisha kamilisha hivyo hapo ni kijana tayari kwa kuoa baada ya kuoa kuna mingalio yake unatakiwa ujue yafatayo ingawa watu wengi huwa hawayafati.1.kuna muda wa kuoa 2.muda wa kuzaa 3.muda wa kujenga 4 muda wa kusomesha watoto mambo nne haya ukiyaweka katika mipangilio maisha daima yatakuwa mazuri ila ukichanganya walio wengi mambo huwa hayaendi.

asante sana mkuu.
 
Awali ya yote kabla hujaanza kumtafuta huyo mchumba Mshirikishe Mungu kwanza, Hakika Mungu ni Mwaminifu atakupatia aliye ubavu wako sahihi kabisa.Kuhusu uwe na nini nimeona watu wameshakueleza nisingependa kuvirudia tena ila ni lazima uwe na mipango endelevu unapoamua kungia kwenye maisha ya ndoa, usipokuwa na mipango ndoa utaiona chungu,Hiyo sh 10,000 unayoipata lazima uipigie mahesabu na uigawanye sawia na mwisho wa siku upate hela ya kuweka akiba kuna mambo mengi sana siwezi kuyaeleza yote ila ni vema pia ili kuepeuka ugomvi wa mra kwa mara ujue wajibu wako kwa mkeo na yeye ajue wajibu wake kwako mshirikiane kupanga maisha yenu.
 
Dah...shida ni kwamba mchumba hatfutwi kama bidhaa...

Mungu anahitajika,na akina dada wa sasa wasumbufu sana.. Anaweza asiwe katulia mara ukishamweka ndani...

Ila jaribu kuwa na mahusiano na akina dada hata yasiyo ya kimapenzi kama kukaa na kula nao lunch,au chakula cha usiku pamoja migahawani ili uweze kuwasoma tabia lakini kumbe ni kwa faida yako...

Hilo anza sasa, katika kipindi cha miaka minne utakuwa ushawasoma na kujua tabia zao..ila umri mzuri ni baada ya 30...
 
Hongera kwa kujitunza na kutokubali wadada waufanyie majaribio mwili wako.
Ili mradi unaweza kupanga chumba, ukalipa kodi na kuweza kula kila siku basi unamudu kuwa na familia. Kila la kheri, Mungu atakupa wa saizi yako. Hela haijai kakangu, ndo maana kina Rostam na Lowasa wanatoa macho kama mijusi. Usichoke kujaribu mipango mipya ya maendeleo lakini.
 
Back
Top Bottom