Kwa maslahi ya Wadanganyika...Jenerali Ulimwengu rudia makala hii

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Ni makala uliyoiandika mwaka 2005 kuelekea uchaguzi. Ilizungumzia Sheria na Taratibu mbovu katika kusimamia taratibu za kupatika wagombea na matumizi ya fedha zisizo na kikomo wala maelezo. Ulikuwa ukitoa onyo kwa Serikali (Msajiri wa Vyama na NEC).

Sikumbumbuki jina na toleo la makala ila ulisema kwa kuruhusu matumizi ya pesa yasiyo na mipaka, atakuja mgeni asiye na uchungu bali uchu na rasilimali za nchi hii. Akifahamu kuwa ili mambo yake yaende vizuri lazima awe na ushawishi kwenye serikali. Na mojawapo ya mhimili ya ushawishi ni Bunge. Atauliza hivi: “Ni pilau ngapi, kofia ngapi na kanga ngapi zinahitajika kumpitisha mgombea kuwa Mbunge Na thamani yake ni Shilingi ngapi” watamjibu jimbo moja ni kama 100M. Kisha atauliza tena nahitaji wabunge wangapi kupitisha jambo lolote bungeni, watamjibu. Atachagua majimbo muhimu kwake na kusimika Wagombea kwa kuwafadhili. Matokeo yake mtakuwa na Bunge linalowajibika kwa Mgeni. Hii ni nukuu isiyo rasmi.

Mtazamo na maoni yangu:
Jenerali alikuwa anafahamu mbinu za wageni kuvamia mihimili ya nchi yetu. Yawezekana pia alikuwa na clue jinsi RAis alivyokuwa anajiandalia Mhimili katika nchi ya WADANGANYIKA kupitia ufadhili wa wagombea wa CCM. Alipiga kelele kadri awezavyo pasipo mafanikio. Sasa ishakuwa aibu ya kizazi, tumeacha kuchukua hatua madhubuti mapema.

Quiz:
Kama Bwana Harusi alishauriwa wakati wa ujenzi; kuwa mapazia pekee bila milango ya mbao au chuma nyumba haiwezi kuwa salama. Akaambiwa aweke mlango hasa chumbani kwake. Akakawia kuchukua hatua wakati wa ujenzi akaoa na kuhamia bila milango ya mbao wala chuma. Jirani akaleta taarifa juu ya waporaji wanaovamia kutoka vijiji vya mbali kuja kuiba na kulawiti kina mama na dada zao, bado mwenye nyumba akaziba masikio.

Ikitokea waporaji wakatembelea nyumbani kwake kwa nia njema labda kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Wakati wanazungusha macho wakamwona mkewe (Bi Harusi) yuko uchi chumbani. Kutokana na tabia yao ya kuiba na kulawiti, wakawashawishika na kumlawiti Bi Harusi. Maana wameisha vuruga, wakabaini hakutakuwa na mahusiano mazuri anymore kufanya Biashara. Hivyo basi wakamua wapore na kuondoka. Hili tendo la kulawiti limefanyka siku na saa mkeo (Bi Harusi) yuko kwenye “PEAK” hivyo yawezekana akawa amepata mimba.

Wewe kama Bwana wa Mgore, utafanyaje au utachukua hatua gani?


A Note of Thanx:

Nawashukuru NIPASHE kwa kuitikia wito huo hapo juu. Kwa mara ya kwanza niliutoa katika thread ya RA Kuvuliwa Uraia?

Katika toleo lao la jana wamejaribu kurejea aliyoandika Ulimwengu mwaka 2005 kabla ya Uchaguzi Mkuu. Kwa wale wenye nakala angalia:

Kichwa cha habari "Fedha katika Uchaguzi"

Urais sasa ni kwa mabilioni

  • Ubunge ni kitita cha Sh. milioni 100

  • Udiwani sasa mgombea awe na milioni 10/
 
Kwenye hii thread, nilimtumia ombi Jenerali kurudia makala INAYOISHI. Kwa mtazamo, fikra na uhalisia wa mambo. Hii makala angeirudia ingekuwa na mashiko kuliko aliyo recycle wiki inayopita.
 
Back
Top Bottom