Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, video hii yaniliza!

mag3;

first; Unaonaje tukichukua zile Bil.90 tunazowapa kanisa through MoU tukawapa madaktari utakubali?? najua hutakubali uache unafiki wako wewe ungelia na Richmond ya kanisa i.e. MoU ambayo hata hivyo wameshindwa kuboresha mazingira KCMC na Bugando..

Pili; nawa challenge hawa madaktari wajenge hospitali yao waendeshe na walipane kama wanavyotaka (kama wanafikiri ni rahisi let them try) waache wale madaktari wanaotosheka na mshahara wa serikali wachape kazi ..otherwise hii ni siasa na kukosa utu na inachochewa na wanasiasa kama wewe..na mwanakijiji et al. after all this is free market

tatu; madakatari Tanzania wanasoma bila kulipa mikopo, hizo hela zinatoka kwa wananchi wanaowatesa kwa sasa; simply hawana hoja isipokuwa harakati za kisiasa..
Choko yaani choko
 
Huyo achana naye, kumjibu ni kumpa heshima asiyostahili na hata akihangaika kuitafuta kwa udi na uvumba, kamwe hataipata!

Usingeweka jina langu kwenye thread yako lol..

Najua wanafiki kama nyie hamtaki kusikia tukiwaambia kanisa linatuibia kwasababu mnafaidi pesa za umma kwa mgongo wa dini..

Siyo lazima ujibu lakini tutaendelea kuwajulisha japo hampendi kusikia ...eti nimelia lia nisikie hizo bil.90 mnazotafuna halafu hamboresha hospitali zinaenda wapi?
 
Usitukane wewe jibu hoja tatu nilizoweka hapo one after another nitakuelewa..

Nasema hivi madai ya madaktari ni illusion hayatekelezeki wakae chini wajadiliane wakiwa hawana jazba na serikali; lakini kama vipi hii ni soko huria

a. Wajenge hospitali zao walipane wapendavyo (problem solved) serikali itashindana na soko katika la ajira

b. Kila anayesomea udakatari Tanzania nakusomeshwa na kwa kodi za wananchi aingie bond na serikali kwamba atafanya kazi serikalini for 5-8 kwa mshahara wa serikali uliopo

c. Tuchukue bil.90 tunazo wapa kanisa tuwalipe madaktari maana kanisa limeshindwa kuboresha hospitali zake japo wanapokea pesa za umma..

JIBUNI hizo hoja

c.

Kwa nn unang'ang'ania 90b za kanisa una maana kanisa ndo limesababisha mgomo!ww ms.....ng!
 
Kwa nn unang'ang'ania 90b za kanisa una maana kanisa ndo limesababisha mgomo!ww ms.....ng!

Kwasababu zinatosha kuboresha madai ya madaktari, kwanini wewe unaogopa bil. 90 za kanisa ni kodi yetu sote ila zinaliwa kifisadi na maaskofu na wanasiasa..haziboreshe services
 
Si kawaida yangu kuandika lakini leo wacha niandike maana I have to. These things are getting into my nerves na watatusababishia wengine tutake kuwa wanasiasa kuleta mageuzi ingawa si wito wetu:

a. Yes ni kweli kwamba serikali inatoa bil.90 kwenye project za kanisa na hakuna auditing yeyote ile siyo kutoka kwa mkaguzi mkuu wala kamati ya bunge..hii ni sawa na richmond skendo ..wananchi tunatakiwa kuikumbusha serikali mara kwa mara hii issue maana inavyoonekana ni ulaji kati ya maaskofu na wanasiasa...hapo serikali inastahili lawama kubwa sana..

Mkuu Tropical, kama una facts zozote unaweza kuweka hapa ingweza kusaidia. Kama huo ni ukweli basi kuna makosa na ni budi yasahihishwe. Hili pia linaonyesha ni kwa kiasi gani viongozi hawako makini unless kama benefits za hizo pesa zinaonekana na ni msaada mkubwa kwa walio wengi.

Hata hivyo bado kuna hoja ya kimsingi kwamba, kwa maelezo yoyote serikali yetu inapaswa kuwajibika juu ya eneo ili muhimu linalohusiana na haki ya mtu kuishi. Haingii akilini ni kwa namna gani mishahara serikalini inaweza ikatofautiana kwa kiasi kikubwa hasa ukilinganisha na baadhi ya Agencies na mashirika mengine ya serikali, i.e BoT, TRA etc.

Hoja ya kuwa Madaktari watafute kazi sehemu nyingine haina upako wala mshiko. The doctor :patient ratio in Tanzania is 1 : 26,000. Tena hii haihusishi madaktari bingwa, na kama unafikiri ni rahisi kwa nini Pinda hajatekeleza maagizo yake ya kuwafukuza. bado sana tunawahitaji madaktari na hizo Private hoaspital unazozisema ziko mijini tu wakati vijijini ambako ndiko kinanuka zaidi hakuna Private Hospitals kwa kiwango cha serikali kuonyesha misuli yake.

b. Nafahamu private ndio maana nikawashauri madaktari kama wanaona huyu muajiri aitwe serikali anatoa mshiko mdogo waache kazi waende private au wajenga hospitali zao walipane mshahara huo..hii itasaidia kupandisha soko lao na hivyo serikali ikikosa waajiriwa itapandisha mshahara ndio soko huria hiyo..ya nini kulialia na mwajiri hana uwezo??

Mkuu unaonekana, you are out of touch. katika nchi hii kuna taaluma zinaitwa "Rare Professionals" na Udaktari ni moja wapo. Ni Sekta ambayo bado tunahitaji msaada mkubwa sana. Dont compare na sectors zingine za trading nk unless kama hujaelewa mantiki ya soko huria katika Muktadha wa Sekta ya Afya kwa Umma ambao ni wajibu wa serikali.

c. Ikiwa watafanya kama kipengele (b) wale watakaotaka kufanya kazi serikalini watakuwa wamekubali hali halisi ya muajiri wao kifedha na kimazingira..kuna wengi wanafuata group pressure tu ndio kawaida ya mgomo..kuna walio comfortable na mshahara huo japo wakiongoezewa itakuwa swa tu..

Kamanda sikiliza, ajira za Madaktari ni lukuki hata nje ya Tanzania. Kuna Madaktari wengi wa TZ Cuba; Brazili; Germany; Botswana nk nk na wakati wowote wakitaka baadhi wanaweza kuondoka na kupata ajira. So, hoja yako haina upako.

d. Unaposomea udaktari tanzania hulipi mkopo japo unalipiwa na wananchi bure, lakini fani zingine unatakiwa kulipa mkopo; nafikiri ni high time serikali iweke bond na wanaosemea udaktari kwenye vyuo vya umma kwa mkopo wa serikali wafanye kazi kwa miaka 5-8 bila kuhama kwa mshahara uliopo.

Refer facts za hapo juu. Nadhani ukidadavua juu ya allowances wanazopata hawa Madaktari V/s mazingira ya kazi na vifaa duni wana haki ya kuomba ongezeko na hasa pale serikali inapokuwa imeziba masikio.

Hata hivyo wanaweza wasipate wanachodai kwa kiasi hicho simply kwa kuwa serikali haina pesa na imefilisika. This means tayari matumizi yake ni makubwa kuliko mapato pamoja na kuongoza kwa kupokea misaada. Of course sababu ya udumavu huu ni kukosa uongozi mbunifu ambao utajikita katika kuleta maendeleo ya kweli badala ya siasa za kuchumia matumbo.

QED
 
mag3;

first; Unaonaje tukichukua zile Bil.90 tunazowapa kanisa through MoU tukawapa madaktari utakubali?? najua hutakubali uache unafiki wako wewe ungelia na Richmond ya kanisa i.e. MoU ambayo hata hivyo wameshindwa kuboresha mazingira KCMC na Bugando..

Pili; nawa challenge hawa madaktari wajenge hospitali yao waendeshe na walipane kama wanavyotaka (kama wanafikiri ni rahisi let them try) waache wale madaktari wanaotosheka na mshahara wa serikali wachape kazi ..otherwise hii ni siasa na kukosa utu na inachochewa na wanasiasa kama wewe..na mwanakijiji et al. after all this is free market

tatu; madakatari Tanzania wanasoma bila kulipa mikopo, hizo hela zinatoka kwa wananchi wanaowatesa kwa sasa; simply hawana hoja isipokuwa harakati za kisiasa..

It is better to keep your mouth closed and let people think you are a fool than to open it and remove all doubt.
 
@ Superman

a. Hizo mbona facts za 90 bil. hakuna anaye despute siyo kanisa wala siyo serikali maana serikali yenyewe imesema inapeleka hizo pesa za umma kwenye miradi ya kanisa lakini hakuna kamati ya bunge wala mkaguzi mkuu anayefanya auditing na sijawahi kuona public report kuhusu matumizi hayo then hizo pesa wanakula maaskofu na baadhi ya wanasiasa (untouchable)..kwani hospitali haina ubora wowote na gharama kubwa..

b. Kama market ya madaktari ni kubwa sana (kama unavyosema) ndio wakati muafaka wafanye kweli waende private serikali ndio itatia akili; wakiweza waende hata nje ya nchi serikali ndio itatia akili..maana lazima wataongeza mshahara..

c. As long as wanalia lia kutaka muajiri awape mshahara huko wakiwaumiza wagonjwa naona bado soko lao ni ndogo; wanatakiwa watoke wamfundishe mwajiri adabu; sioni mantiki ya kugoma na kulazimisha kuongezewa mshahara wakati kuna sehemu nyingine nzuri ya kufanya kazi na mshahara mkubwa; muajiri habembelezwi hivyo
 
Lililoniongezea uchungu zaidi ni hivi vitisho wanavyopewa wananchi wanapodai haki zao. Hebu mshuhudieni huyu ruga ruga wa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa tamko la serikali wakati ambapo kama hekima kidogo tu ingetumika, mambo yasingefikia hapa tulipo.

Yaani Pinda anakubali kutumiwa kama taulo ya mkulu kujipangusia jasho! Nasikia sasa anataka kuonana na madaktari ambao kutokana na tamko lake walishafukuzwa, sijui anajisikiaje kutumika vile.
 
Last edited by a moderator:
@ Superman

a. Hizo mbona facts za 90 bil. hakuna anaye despute siyo kanisa wala siyo serikali maana serikali yenyewe imesema inapeleka hizo pesa za umma kwenye miradi ya kanisa lakini hakuna kamati ya bunge wala mkaguzi mkuu anayefanya auditing na sijawahi kuona public report kuhusu matumizi hayo then hizo pesa wanakula maaskofu na baadhi ya wanasiasa (untouchable)..kwani hospitali haina ubora wowote na gharama kubwa..

Mkuu don't assume kuwa hii issue naijua. Silali JF wala si 24X7. The Burden of Proof na kuleta evidence ni yako maana wewe ndo umeamua kuchanganya subjects. No matter ufisadi unafanyikia wapi kama ni Msikitini, kanisani, Serikalini au popote, Fisadi ni Fisadi tu. Sijaona facts zozote zaidi ya tuhuma tu. I dont live kwa tuhuma.

b. Kama market ya madaktari ni kubwa sana (kama unavyosema) ndio wakati muafaka wafanye kweli waende private serikali ndio itatia akili; wakiweza waende hata nje ya nchi serikali ndio itatia akili..maana lazima wataongeza mshahara..

Which is as good as wakiacha kufanya kazi. The choice is theirs. Sasa unafikiri kwa nini Serikali na Bunge wanahaha kumaliza mgogoro? Fungua macho fikiria beyond the scope na si kwa ushabiki Mkuu.

c. As long as wanalia lia kutaka muajiri awape mshahara huko wakiwaumiza wagonjwa naona bado soko lao ni ndogo; wanatakiwa watoke wamfundishe mwajiri adabu; sioni mantiki ya kugoma na kulazimisha kuongezewa mshahara wakati kuna sehemu nyingine nzuri ya kufanya kazi na mshahara mkubwa; muajiri habembelezwi hivyo

Bado huzioni hoja za msingi. Na wala hoja zako hazitoi ufumbuzi. Ulatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Wakishatoka, then what next kwa maana ya maendeleo ya sekta ya Afya na huduma?

Madaktari hawajambembeleza. Wameweka Tools Chini. Period. Serikali na Bunge na Vinahaha sasa. Au uko Dunia ipi Kamanda?
 
Mag3 asante sana kwa kutuhabarisha....Inakuwa vigumu sana kuzuia machozi. Serikali imeenda wapi? Kweli hayo ndio maisha bora kwa kila Mtanzania? Kikwete historia itakuhukumu siku si nyingi. Serikali nzima haina budi kuwajibishwa pamoja na wabunge wote wameshindwa kusimamia haki za watu wao waliopigia kura. Dodoma mnafanya nini kama mlikuwa na uchungu na watanzania bunge lilitakiwa kuahiirishwa na kushughulikia hili jambo..Nawahurumia Watanzania wangu, Nawapa pole Watanzania wangu, Nazidi kuliomba Taifa langu mungu aturehemu.
 
@superman

a. Kuweka tools chini si kuacha kazi ni kutaka kuongezewa mshahara na madai mengine...that means wako tayari kufanya kazi ikiwa muajiri anaweza kufanya ABC, issue hapa ni kama muajiri ni mbaya kihivyo na wewe daktari una soko nzuri kwanini usiende kwa mwajiri mwingine..halafu kila siku wanafiki hospital kujionyesha na kuwaudhi wagonjwa unethical kabisa..waende kwa waajiri wazuri kuliko serikali nje na ndani ya nchi; serikali ni muajiri mbay hana uwezo..waende kwa wenye uwezo na anaweza kuwapa wanachota kama yupo..kwanini wanashinikiza kuajiriwa serikalini??

b. Hizo bil. 90 zilizonda kanisani tulitegemea zingeboresha hospitali za kanisa lakini nazo zimeliwa na wajanja; nao wamegoma kama kawaida; hiyo ni proof tosha besides tafauti hotuba za Rais za kila mwezi ameproof kwamba kanisa linavuta 90 bil. kila mwaka..nafikiri wanashirikiana kuzifisadi maana hakuna matokeo ya pesa hizo kwenye cite level.
 
Mag3 asante sana kwa kutuhabarisha....Inakuwa vigumu sana kuzuia machozi. Serikali imeenda wapi? Kweli hayo ndio maisha bora kwa kila Mtanzania? Kikwete historia itakuhukumu siku si nyingi. Serikali nzima haina budi kuwajibishwa pamoja na wabunge wote wameshindwa kusimamia haki za watu wao waliopigia kura. Dodoma mnafanya nini kama mlikuwa na uchungu na watanzania bunge lilitakiwa kuahiirishwa na kushughulikia hili jambo..Nawahurumia Watanzania wangu, Nawapa pole Watanzania wangu, Nazidi kuliomba Taifa langu mungu aturehemu.

Emotional and useless sensational information
 
Mkuu wewe pekee ndio umetumia brain kujibu hoja zangu..wengine washabiki wakubwa

a. Yes ni kweli kwamba serikali inatoa bil.90 kwenye project za kanisa na hakuna auditing yeyote ile siyo kutoka kwa mkaguzi mkuu wala kamati ya bunge..hii ni sawa na richmond skendo ..wananchi tunatakiwa kuikumbusha serikali mara kwa mara hii issue maana inavyoonekana ni ulaji kati ya maaskofu na wanasiasa...hapo serikali inastahili lawama kubwa sana..

b. Nafahamu private ndio maana nikawashauri madaktari kama wanaona huyu muajiri aitwe serikali anatoa mshiko mdogo waache kazi waende private au wajenga hospitali zao walipane mshahara huo..hii itasaidia kupandisha soko lao na hivyo serikali ikikosa waajiriwa itapandisha mshahara ndio soko huria hiyo..ya nini kulialia na mwajiri hana uwezo??

c. Ikiwa watafanya kama kipengele (b) wale watakaotaka kufanya kazi serikalini watakuwa wamekubali hali halisi ya muajiri wao kifedha na kimazingira..kuna wengi wanafuata group pressure tu ndio kawaida ya mgomo..kuna walio comfortable na mshahara huo japo wakiongoezewa itakuwa swa tu..

d. Unaposomea udaktari tanzania hulipi mkopo japo unalipiwa na wananchi bure, lakini fani zingine unatakiwa kulipa mkopo; nafikiri ni high time serikali iweke bond na wanaosemea udaktari kwenye vyuo vya umma kwa mkopo wa serikali wafanye kazi kwa miaka 5-8 bila kuhama kwa mshahara uliopo.

My take:

a. Unakubali serikali na uongozi wake ni legelege isiyoweza kupanga na kusimamia majukumu yake. mifano ni mingi sio MoU tu ambayo kimsingi anayetakiwa kulaumiwa (kama kweli zipo lawama genuine) ni serikali kwa uzembe wa kutosimamia uhalali wa matumizi ya hizo pesa. kuna EPA, Meremeta, Kagoda, Deep green, IPTL, Buzwagi, Rada, kiwira, Jairo, Richmond, DOWANS nk nk nk yote haya yanatokea na jamaa wanachekacheka tu.

b. Kwanza hiyo solution yako haitoi ufumbuzi wa tatizo tulilonalo leo, maana hivi tunavyoongea kuna watu wanakufa kwa kukosa maDrs ambao unawashauri wakaanze kujenga hospitali zao za bei juu. lakini pili wanaolialia sasa si maDr ni wananchi na wagonjwa, hii thread yenyewe haionyeshi Dr hata mmoja analialia bali wagonjwa na ndugu zao. kuna thread pia zinazoonyesha wanaharakati wamebeba mabango, umemuona Dr hata mmaja pale?. Hiyo ndiyo reality iliopo mtaani. umesikia wapi maDr wakilialia? wao walitoa hoja solid wakatulia.

c. Unaonekana kuamini kuwa hali ya serikali kifedha na kimazingira ni mbaya. Inawezekana hilo ni kweli. lakini katikati ya ufisadi mkubwa usioshughulikiwa na yeyote kama nilivyoeleza hapo kwenye a. wawezaje kusema huna uwezo? tungekuwa na kiongozi serious katika kushughulikia ufisadi na kupanga na kusimamia vipaumbele vya taifa, sio anayesema "...rudisheni mlichoiba mwisho october" au "...wameiba lakini wanahaki zao" ingekuwa rahisi kuamini kuwa kweli serikali haina uwezo. Pia ni wajibu wa serikali kuweka mfumo wa usawa na haki hasa katika malipo ya watumishi wa umma ili kuondoa double standards. Na jambo moja dhahiri linaloweka tofauti kubwa kwa watumishi wa umma ni malipo ya posho zisizo na tija. Mfano Bunge linaahirishwa saa tano, mbunge anaenda semina saa nane hadi saa kumi - analipwa 200,000. Daktari anaanza zamu saa 9 mchana hadi saa mbili asubuhi kesho yake, pesa anayolipwa 10,000 (tena nayo Mungu akipenda!) na baada ya saa mbili anatakiwa aunganishe non stop hadi saa 9. kuna usawa hapo? akilalamika atakuwa analialia?

d. Serikali ina wajibu wa kuwasomesha maDr kwa niaba ya wananchi na maDr wana wajibu wa kusoma (maana nayo sio kazi rahisi - ni kazi yenye adha na machungu mengi tu). Serikali haina haki kuwanyanyasa kwa kutengeneza mazingira mabovu na kuwaonea katika malipo. Serikali inasomesha maDr kwa niaba ya wananchi walioiweka madarakani na wanaolipa kodi. leo hii wananchi haohao (...ofcourse except you!) ndio wanaoiagiza serikali kuwalipa madaktari haki zao.
 
9.jpg

hawa polisi ndio nini sasa!
 
a. Ni kweli serikali inawachekea mafisadi wengi uliowataja ikiwemo hizi za MoU na kanisa, kwakuwa hizo pesa zinatolewa na wizara ya afya kupelekwa kuboresha hospitali za kanisa ambazo bado hazijaboreshwa (ndio madrs wamegoma huko pia) ni budi sasa serikali i-stop kulipa na kiwango hicho wapewe madrs haraka iwezekanavyo..hiyo ni immediate solution

b. Madai ya madaktari hasa mshahara ni illusions hakuna serikali inaweza kulipa labda tusimamishe shughuli zingine, after all hakuna budget yao kwa sasa, kwakuwa muajiri hana uwezo wasiendelee kujiita mdrs wa serikali waache tu waende private au waanzishe hospitals zao walipana vema; serikali na wananchi wake that is the price they have to pay..ili wapange long run solution ikiwemo kuwepo na bond ya kufanya kazi serikalini for some yrs kama umesomea pesa za wananchi wa Tanzania..

c. Nakubaliana na wewe tuanze kushughulikia mafisadi hasa hii pesa maalum za MoU maana imekuwa long overdue na haikuleta effect yoyote katika kuboresha health services

d. Wamesomeshwa na wananchi ili wawahudumiwe siyo kukataa kuwahudumii huki kusomeshwa umesomeshwa bure na pesa za kodi; ndio maana nasema kama drs waliona mazingira, haki (una maana maslahi) ni duni walitakiwa wasikubali ajira za serikali simple as that; wanalia kwasababu wasingekuwepo serikalini wakiwa private serikali ingesha jua cha kufanya
 
MGOMO WA MADAKTARI :Mtafaruku
Wednesday, 08 February 2012, 22:05
Waandishi Wetu
Mwananchi

MGOMO wa madaktari nchini umeingia katika sura mpya baada ya wanaharakati kutoka asasi 15 za kiraia kufanya maandamano ya amani jana, wakitokea maeneo mbalimbali kuelekea Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuwasilisha kilio chao kwa Rais Jakaya Kikwete. Hata hivyo, wanaharakati hao hawakufanikisha lengo lao baada ya kujikuta wakidhibitiwa na kusambaratishwa na polisi waliokuwa na silaha .

Pamoja na kukwamishwa mkakati wao huo, wameipa Serikali saa 24 kuchukua hatua za haraka kumaliza mgomo wa madaktari na kutishia kwamba kinyume na hapo, watawahamasisha wananchi kuingia barabarani, kufanya maandamano makubwa ya kuishinikiza Serikali kujiuzulu.

Kwa muda wa wiki mbili sasa nchi imekuwa ikitikiswa na mgomo wa kihistoria wa madaktari, ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa utoaji huduma za afya kwenye hospitali za rufaa ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa (MOI), ambako huduma zimesitishwa.

Katika maandamano ya jana, wanaharakati hao walifunga Barabara za Ali Hassan Mwinyi na Ocean Road kwa muda wa saa moja na kusababisha foleni kubwa ya magari.

Maandamano hayo ya kushtukiza yaliyoanza saa 8:00 mchana, yalishirikisha asasi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa).

Awali, wanarahakati hao walianza kujikusanya taratibu kati ya eneo la Hoteli ya Palm Beach na Kituo cha Polisi cha Oysterbay kilichopo jirani na daraja la Salender, huku wengine wakilala barabarani.

Wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, wanaharakati hao wametaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Lucy Nkya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni wajiuzulu kwa kuwa wanafanya mzaha kwasababu Rais na viongozi wengine hawatibiwi nchini wakiugua.

Katika maandamano hayo, waanaharakati hao pia walimlaani Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa kuzuia kujadiliwa kwa suala hilo la dharura na kuongeza kwamba, kwa kuwa tatizo linajulikana hakukuwa na haja ya kuunda kamati kutafuta chanzo.

Akizungumza jana Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya alisisitiza kuwa maandamano hayo ni ya wananchi. Alieleza kuwa ujumbe wao walioutuma kwa Serikali usipotekelezwa, watawaambia wananchi waingie mtaani kudai haki yao ya kupata matibabu.

Tunatoa saa 24 kwa hatua za haraka kuchukuliwa kuhusu mgomo wa madaktari la sivyo, kesho (leo) tutawaeleza wananchi jinsi ya kuingia barabarani ili kuishinikiza Serikali ijiuzulu,alisema Nkya.

Mratibu wa Mtandao wa Asasi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha (Angonet), John Bayo, alisema mgomo wa madaktari unapaswa kusitishwa sasa, kwa pande hizo mbili yaani Serikali na madaktari, kukaa na kukubaliana.

Lazima wakae, watu wanakufa kwa kukosa matibabu, hapa hatafutwi mshindi bali haki na maisha ya watu,alisema Bayo. Bayo alisema katika kikao hicho kwa kuwa madai ya madaktari yanafanana na wafanyakazi wengine wa umma katika sekta nyingine, lazima kuwapo mpango wa kumaliza matatizo ya muda mfupi, wa kati na mrefu.

Alisema haiwezekani sasa maisha ya watu yanapotea, huku Bunge likiendelea kulumbana na Serikali ambayo nayo inatoa matamshi ya vitisho kwa madaktari jambo ambalo, si jema.

Polisi
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema watu hao walikuwa wamekusanyika eneo la Palm Beach na kwamba, mkusanyiko huo ulilenga kuwashawishi madaktari kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa. Lilikuwa kundi la watu takribani 150 na walikuwa wakitaka kufanya maandamano kushinikiza madaktari kurudi kazini, tulichokifanya Polisi ni kuwataka watawanyike na walitii amri hiyo, alisema Shilogile.

Alisema kazi ya Jeshi hilo sio kutatua tatizo la mgomo wa madaktari bali ni kuhakikisha usalama wa raia na kwamba, watu hao wanatakiwa kuwasilisha madai yao sehemu husika.

Bungeni

Mgomo huo jana ulirindima tena bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, kufuatia Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), akiwa ni mbunge wa sita kutaka kujadiliwa hoja hiyo, aliomba kwa kutumia kanuni ya 47, Bunge kujadili jambo hilo la dharura. Naibu Spika, nchi yetu inalo jambo la dharura sana. Hii ni karibu wiki ya pili Watanzania wenzetu wanakufa mahospitalini. Hili limekuwa linaombwa hapa, naona tena leo niombe Bunge lako lijadili suala la mgomo wa madaktari pamoja na yote yanayoendelea. Wako watu wanaosema ni kuingilia mihimili mingine, hapana, wanaokufa ni Watanzania ambao leo tuko hapa kuwawakilisha, alisema Serukamba na kuongeza:

Litakuwa Bunge la ajabu sana na tutaingia kwenye historia, Watanzania wanakufa tunasema hatuwezi kuingilia mhimili mwingine. Ninaomba leo wabunge mniunge mkono ili Spika uamue sasa tuanze kujadili suala hili gumu ambalo Watanzania wanapoteza maisha yao.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na kukubaliwa na wabunge wote. Lakini, akitoa mwongozo wake, Naibu Spika Job Ndugai, alisema kwa mujibu wa Ibara 63 ya Katiba ya Nchi, inatambua Bunge kama chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambacho kitakuwa na madaraka ya niaba ya wananchi kusimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake vyote.

Sasa huwezi kusimamia jambo au huwezi kuwa mshauri mzuri kama hujapata ukweli au hujapata kidogo undani wa mambo na ndiyo maana jambo hili mliposimama mara ya kwanza, tena mkasimama tukashauri kwamba ni vizuri liende katika Kamati yetu ili tutakapoishauri Serikali, tukiwashauri hawa watumishi wa Serikali tuwe tunatoa ushauri ambao unatokana na watu ambao wako informed,(wanauelewa) alisema Ndugai. Madaktari Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayosimamia madai yao Dk Stephen Ulimboka, alisema lawama zinazotokana na wagonjwa kwa kukosa tiba zinapaswa kuelekezwa serikalini.

Dk Ulimboka alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa kuelezea hatua walizofikia kati yao na Serikali kuhusu mgomo unaoendelea hivi sasa. Tangu madaktari wagome leo (jana) ni siku ya 16, Kamati iliyoundwa na Serikali kushughulikia suala hilo haijawahi kutoa taarifa yoyote wala kukutana nasi, sisi tulishasema na leo tunarudia, milango iko wazi kwa ajili ya majadiliano na Serikali,alifafanua Dk Ulimboka.

Alisema kimsingi, wao wanaumizwa na hatua hizo, lakini, akadai msimamo wao unadai haki zao sababu wamelenga kusaidia haki zao na za wananchi ambao wanakosa tiba bora kutokana na Serikali kutozingatia umuhimu wa huduma za afya hapa nchini.

Dk Ulimboka alisema kamati yake imeendelea na vikao kujadili mambo mbalimbali huku ikisubiri tamko litakaloonyesha nia ya Serikali ya kushughulikia madai yao.

Viongozi wa dini

Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Arusha, Abbas Mkindi maarufu kama Darwesh, alisema baraza hilo linapinga mgomo, lakini pia linataka Serikali kukaa na madaktari.

Lazima Serika imalize mgogoro huu na pia ichunguze chanzo chake na hizi kauli za watendaji wake, kwani hapa tunahisi kuna hujuma dhidi ya Serikali ya Rais Kikwete, alisema Mkindi. Kwa upande wa Mchungaji Anicet Maganya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Arusha, alisema kubwa katika madai ya madaktari ni maslahi, lakini wameonekana kukerwa na majibu ya watendaji wa Serikali na vitisho. Mchungaji Maganya ambaye ni Mkuu wa Idara Utetezi ya Kanisa hilo , alisema ingawa haungi mkono mgomo unaoendelea anaamini kauli za viongozi wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwatisha madaktari ndio umefikisha hapa.

Habari hii imeandaliwa na Geofrey Nyangoro, Joseph Zablon, Dar na Mussa Juma, Arusha
 
a. Ni kweli serikali inawachekea mafisadi wengi uliowataja ikiwemo hizi za MoU na kanisa, kwakuwa hizo pesa zinatolewa na wizara ya afya kupelekwa kuboresha hospitali za kanisa ambazo bado hazijaboreshwa (ndio madrs wamegoma huko pia) ni budi sasa serikali i-stop kulipa na kiwango hicho wapewe madrs haraka iwezekanavyo..hiyo ni immediate solution

b. Madai ya madaktari hasa mshahara ni illusions hakuna serikali inaweza kulipa labda tusimamishe shughuli zingine, after all hakuna budget yao kwa sasa, kwakuwa muajiri hana uwezo wasiendelee kujiita mdrs wa serikali waache tu waende private au waanzishe hospitals zao walipana vema; serikali na wananchi wake that is the price they have to pay..ili wapange long run solution ikiwemo kuwepo na bond ya kufanya kazi serikalini for some yrs kama umesomea pesa za wananchi wa Tanzania..

c. Nakubaliana na wewe tuanze kushughulikia mafisadi hasa hii pesa maalum za MoU maana imekuwa long overdue na haikuleta effect yoyote katika kuboresha health services

d. Wamesomeshwa na wananchi ili wawahudumiwe siyo kukataa kuwahudumii huki kusomeshwa umesomeshwa bure na pesa za kodi; ndio maana nasema kama drs waliona mazingira, haki (una maana maslahi) ni duni walitakiwa wasikubali ajira za serikali simple as that; wanalia kwasababu wasingekuwepo serikalini wakiwa private serikali ingesha jua cha kufanya

Mbona mwenyewe umekiri kuwa pesa za MoU hazikaguliwi na yeyote? sasa umejuaje kuna ufisadi. Nimekuuliza hizo biliono 90 hutolewa kwa terms zipi na nini ambacho hakijatimizwa? je ni mishahara na posho za maDrs? - kama hakuna auditing wala terms tunathibitishaje kuwa kuna ufisadi?

Halafu by the way, hivi kwa nini hakuna MoU na misikiti?
 
Back
Top Bottom