Kwa madaktari tu:

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
477
120
Ndugu zangu, Kweli madai yenu ni ya msingi sana na waunga mkono kwa hili, Hata Mh Rais wa jamhuri anajua sisi wananchi wa chini tuko pamoja nanyi. Tunalaani kitendo cha kupigwa na kuumizwa daktari mwenzenu Dr Stephen Ulimboka. Tumefedheheshwa na kukasirishwa na unyama wote aliotendea na tunalaani wote waliofanya hivyo. Madktari tunaomba mtoonee huruma tunakufa ndugu zenu serikali hii ni kiziwi haisikii asilaani. Ila ngoma ivumayo sana wote twajua.

Kuhusiana ombi liloshadadiwa la Mshahara tunawaomba mbadilishe ombi lile nanyi mdai kuwa na maduka yenu ambayo vitu vyake havikati kodi kama wafanyiwavyo wanajeshi na vilevile muwe mnapata fedha za posho mbali na mishahara yenu katikati ya mwezi kama wanajeshi kwani wao wanalinda uhai na nyie mnalinda uhai.

Ndugu zangu Madaktari naomba mbadili kima cha chini kwa million 3.5 kwenda kwenye hizo privileged nyingine na pia naomba muandae maandamano ya amani ya kupinga mazingira mabovu ya kufanyia kazi nasi tutawaunga mkono hata ikiwezekana mchana huu.

Madaktari naomba msikatishwa tamaa na watu ambao hawavilali vitanda vyenu kwani hawajui kunguni waliomo siku ndege ya rais ikidongoka akakosa CT scan hospital atajua mlikuwa mnamaanisha nini kwa sasa haelewi.

Riz akipata ajali ya mi VX yake wakati akienda kuangalie lile roli la mafuta litakalochomwa na wananchi tunduma kesho atajua nini maana ya uwepo wa x ray mashine kwenye hospital za wilaya.

Mama spika siku lile super Feo lake litakapo ungua moto na kutakiwa huduma ya haraka pale makambako na yeye akiwemo aajua nini maana ya umuhimu wa kuruhusu hoja ya mgomo wa madaktari ijadiliwe bungeni kwa dharura.

Madaktari tuko nanyinyi ila naomba, tutumie summary tu hapa ingieni barabarani kiwake mapema ili tutibu haraka yaishe baasi.

Ni hayo tu.

Wenu katika safari ya magwepande

Mwanaharakatihuru.
 
Unaota ,tumechoka kuona watu wanatufia mikononi mwetu huku hatuwezi kufanya lolote kisa vifaa,ukiambiwa katupigie ct-scan regency unadhani sie tuna ubia na hao private,ukianbiwa kwenye echo,na ecg watu ni wengi njoo mwezi ujao unadhani unatengenezewa zengwe la wewe kutoa rushwa ,ukiambiwa icu imejaa leo hatufanyi operation unadhani unatengenezewa mazingira ya rushwa .cc ni binadamu tuna mioyo ya nyama siochuma hayo yote tumeyachoka yametufika shingoni .tafakari chukua hatua#
 
Madactari mposahihi katk madai yenu lakini kwa kosa la serikali kwanini mnatuadhibu wananchi tusiyo na hatia? Tuhurumie jamani tunapenda kuishi tushuhudie mapambano ya mapinduzi ya kweli! Serikali yetu imechoka kuongoza tuvumiliane mpaka 2015 tutakapo weka serikali yenye nguvu madarakani. Solidality forever!
 
Madactari mposahihi katk madai yenu lakini kwa kosa la serikali kwanini mnatuadhibu wananchi tusiyo na hatia? Tuhurumie jamani tunapenda kuishi tushuhudie mapambano ya mapinduzi ya kweli! Serikali yetu imechoka kuongoza tuvumiliane mpaka 2015 tutakapo weka serikali yenye nguvu madarakani. Solidality forever!
sisi wananchi ndio wajinga , tunajua wazi kabisa kuwa tunalipa kodi kwa serikali ambayotumeiweka madarakani na tunajua wazi kabisa hatuna mkataba na madaktari.kwanini sasa tukubali serikali ichezee afya zetu kwa kugombana na madaktari...sisi ni wajinga wa kutupwa...kwa ujinga wetu ngoja tuendelee kufa huku mafisadi(serikali) wakiendelea kufaidi rasilimali za taifa letu
 
Iambie serikali iwarudishe interns waliowatimua madaktari watarejea kazini
 
Jamani msicheke, hapa kuna kitu huyu mleta mada anatabiri, au mimi ndiye naona matukio yajayo kupitia maandishi yake!
 
Back
Top Bottom