Kwa kuzikataa hoja mbili za Serikali; Kazi nzuri wabunge wa JMT!

Kubingwa

JF-Expert Member
Apr 23, 2010
505
69
Wabunge wa JMT wamerudisha hoja mbili zilizowakilishwa bungeni na serikali leo ili serikali iende ikajipange vizuri.Nawapongeza sana wabunge kwa kuweka maslahi ya taifa mbele.Hoja zilizogoma kupita ni ile kuhusu kupunguza ushuru wa maji toka nje na ile ya marekebisho ya katiba.


Bravo wabunge!








Source: Toka Bungeni,Idodomya!
 
Kuna sauti ya jimama fulani anakubali then anakaata halafu sijui kachakachua microphone yake maana dah lina sauti balaaaaaaaaaaaaa!
Ila kweli maslahi ya taifa mbele. Big up
 
Jamani namhurumia jaji Werema, ameshindwa kujenga hoja akaishia kutishia kuwa yeye bado ni jaji hajanyang'anywa ujaji wake, mwisho wa siku, jembe-Tundu Lisu akamzamisha kwa hoja nzito.
 
Safi sana Ndugai unanesha njia kwa huyu mama namna ya kuliongoza bunge! Ndungulile ni aina ya wabunge bora ccm wengine waige,huyu ndiye aliyetoa hoja ya kuahirisha mjadala wa hoja ya kubadili sheria mbalimbali kutokana na sheria ya bodi ya mikopo kuwa ya kishenzi na ingeleta ubaguzi baina ya wanafunzi!
 
Kama kweli wamefanya vizuri ila ukiletwa kwa mara ya pili hata kama ni mbovu wataupitisha na tusubiri muda utasema
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nampongeza mbunge wa jimbo la kigamboni faustine Ndungulile kwa kutoa hoja.Hakika leo bunge limefanya kazi ya kibunge
 
Inaonekana naibu spika alikuwa na kigugumizi cha maamuzi, alitamani iendelee kujadiliwa. Nafuu tupunguze rubber stamping katika bunge la JMT.
 
egoli ingine,tunapumbazwa ili tusahau habari ya posho.siliamini hili bunge wala chama twawala wala rais wao m kwere
 
Kuna sauti ya jimama fulani anakubali then anakaata halafu sijui kachakachua microphone yake maana dah lina sauti balaaaaaaaaaaaaa! Ila kweli maslahi ya taifa mbele. Big up
umeliskiaeee halafu lina sauti mbaya kama linakwaruza debe
 
sijalisiki hilo 'jimama' lakini kwa jins ulivyolielezea,lazma pat taim job yake ni nanihii..., . Bravo waheshmiwa,ingawa wakat mwingine hamtutendei haki watz
 
Sio kila hoja itakayokataliwa bungeni itakuwa na maslahi ya Taifa. Mleta mada, sema hata kwa ufupi nini maudhui ya hoja za serikali na kukataliwa na wabunge ni maslahi yapi ya nchi yamelindwa.
 
Kama kweli wamefanya vizuri ila ukiletwa kwa mara ya pili hata kama ni mbovu wataupitisha na tusubiri muda utasema

Huo ndiyo ukweli wenyewe,na watapiga meza sana siku ukirudi na utasikia kauli za kipumbavu kuwa serikali yetu ni sikivu wamefanya kile ambacho tulikuwa tunataka,atakayeongea atakuwa sendeka au kilango manake hao ndiyo wanajulikana kuwa na midomo ya kupepeta ila kichwani weupe.
 
Wanasiasa haswa wa CCM ni watu waajabu sana, wakienda huko wakakaa kama KAMATI YA CHAMA wakirudi wanagonga meza na kushangilia kwa kila kifungu! Hamna litakalo badilishwa au kurekebishwa, tusubiri hilo bunge lijalo tuone.
 
Ndugai; a standing ovation on this one!

This is a good surprise for new year 2012. You can very well be ANOTHER SAMUEL SITTA standards and speed only if you chose the path to be exactly that of a balance speaker of the National Assembly at mind and in action.

Do your BioChemistry here brother to the advantage of the weak and the voiceless majority in Tanzania. Seriously speaking, you can be another Samuel Sitta for our nation.
 
Sijui ni kwa nini napata mashaka sana na uwezo wa Jaji Werema? Ukimsikiliza tu bila kuambiwa kuwa ni mwanasheria/Jaji inakuwa vigumu kweli kujua kuwa ana taaluma ya sheria. Kuna haja hivi vyeo kama AG viwe ni vya kuomba na kufanyiwa interview kabisa badala ya kupeana peana tu.
 
kuna dada mmoja amekosoa kila kift,ngu kwenye mswada lakini mwisho likaunga mkono hoja mia kwa mia,.litakuwa la viti maalum tu.
 
Back
Top Bottom