Kwa kuwa sisi ni Wazembe wa Kusoma Vitabu vya Kufikirisha Akili--Hiki nachoo Kitapita!

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Tanzania imekuwa na waandishi wa Vitabu wengi sana na mara nyingi Vitabu hivi huongelea matukio ya kihistoria kama vile Uhuru, Ujamaa n.k na wengine huandika 'novel' zilizojaa hadithi za kusisimua na kuogofya na mazingira ya 'kufikirika' tu ambayo hayawezi kumjengea babu yangu kule uwezo wa kufikiri.
Wiki iliyopita katika kutafuta Vitabu vya Watanzania nikakutana na hiki kinachoitwa 'SINDANO INAYOVUJA-A leaking Needle, kitabu cha mtanzania ambacho kimechambua sekta ya Afya na Kupendekeza Mbinu Bora za kuiboresha, Mbinu ambazo kama zingetekelezwa labda tusingekuwa tunaongelea Mgomo wa madaktari sasa

Bofya Hapa: Amazon.com: SINDANO INAYOVUJA (A Leaking Needle) (Swahili Edition) (9781468156898): Kahabi G Isangula: Books

Jambo la kusikitisha ni kwamba Maarifa yaliyomo humu yaliyoandikwa na Mtaalamu huyu kwa Lugha ya KISWAHILI kwa kuwalenga Watanzania yatapita hivi hivi abda kwa kuwa sisi ni WAZEMBE wa kusoma VITABU vya KUFIKIRISHA akili zetu( Hii inadhihirika na watu humu JF wasivyopenda kusoma Post za kufikirisha akili zao kwa ushaidi kuwa watu wanao peruzi ukurasa wa 'Great Thinkers' ni wachache mno ukilinganishwa na kwenye 'mahusiano' 'Celebrity' na 'siasa') au kwa sababu ya DHARAU kwa waandishi wa Kitanzania na KUTOTHAMINI CHA NYUMBANI.

Mimi nimeshanunua nakala yangu, shukrani kwa CRDB Tembocard Visa iliyoniwezesha kununua kitabu hiki toka Amazon.
Waweza kuungana nami au ukaungana na kundi nililotaja hapo juu.
 
Huo ni ukweli ndiyo maana majibu ya wachangiaji wengi ni ya kupondana na siyo ya kutatua matatizo au kero zinazowasishwa humu. Lakini mkuu bado tunaweza kubadilika.
 
mkuu ebu toa darasa jinsi ya kununua kitabu hicho kupitia amazon.com; mimi ni member wa amazon, na kuna vitabu vingi vizuri online kule, tatizo ni jinsi ya kununua.
 
Tanzania imekuwa na waandishi wa Vitabu wengi sana na mara nyingi Vitabu hivi huongelea matukio ya kihistoria kama vile Uhuru, Ujamaa n.k na wengine huandika 'novel' zilizojaa hadithi za kusisimua na kuogofya na mazingira ya 'kufikirika' tu ambayo hayawezi kumjengea babu yangu kule uwezo wa kufikiri.
Wiki iliyopita katika kutafuta Vitabu vya Watanzania nikakutana na hiki kinachoitwa 'SINDANO INAYOVUJA-A leaking Needle, kitabu cha mtanzania ambacho kimechambua sekta ya Afya na Kupendekeza Mbinu Bora za kuiboresha, Mbinu ambazo kama zingetekelezwa labda tusingekuwa tunaongelea Mgomo wa madaktari sasa

Bofya Hapa: Amazon.com: SINDANO INAYOVUJA (A Leaking Needle) (Swahili Edition) (9781468156898): Kahabi G Isangula: Books

Jambo la kusikitisha ni kwamba Maarifa yaliyomo humu yaliyoandikwa na Mtaalamu huyu kwa Lugha ya KISWAHILI kwa kuwalenga Watanzania yatapita hivi hivi abda kwa kuwa sisi ni WAZEMBE wa kusoma VITABU vya KUFIKIRISHA akili zetu( Hii inadhihirika na watu humu JF wasivyopenda kusoma Post za kufikirisha akili zao kwa ushaidi kuwa watu wanao peruzi ukurasa wa 'Great Thinkers' ni wachache mno ukilinganishwa na kwenye 'mahusiano' 'Celebrity' na 'siasa') au kwa sababu ya DHARAU kwa waandishi wa Kitanzania na KUTOTHAMINI CHA NYUMBANI.

Mimi nimeshanunua nakala yangu, shukrani kwa CRDB Tembocard Visa iliyoniwezesha kununua kitabu hiki toka Amazon.
Waweza kuungana nami au ukaungana na kundi nililotaja hapo juu.

usilaumu tu watz. Hicho kitabu kimefanyiwa promo kiasi gani?
 
[h=2]Book Description[/h]Publication Date: January 1, 2012
[h=2]Book Description[/h]Publication Date: January 1, 2012
SINDANO INAYOVUJA (A Leaking Needle) Ni Kitabu cha Kiswahili kinachojadili Mianya, Vipimo na Udhibiti wa Rushwa katika Sekta ya Afya ili kuchochea Uwajibikaji, Uwazi na Uadilifu. Kimeandikwa kutokana na tafiti za ndani na nje ya Nchi zilizofanywa ili kusaidia kubuni sera, kanuni na taratibu bora za Kuzuia na Kudhibiti Vitendo vya Rushwa katika Sekta ya Afya. Kama vile Sindano inayovuja isivyoweza kutoa dozi kamili kwa Mgonjwa, Rushwa katika sekta ya Afya hupunguza kiwango stahili cha tiba na kuondoa Usawa wa Huduma kati ya Watoa Rushwa na Wasioweza kutoa. Kwa Muda mrefu tumeshuhudia ongezeko la Matukio yanayotokana na Vitendo vya Rushwa katika Sekta ya Afya, vitendo ambavyo bila kuwa na njia thabiti za kuvidhibiti , Ubora na Usawa katika huduma za Afya utadorola na Masikini wasioweza kutoa Rushwa wakiendelea kuumia. Kitabu hiki kinajadili mianya iliyopo katika sekta, Mapungufu ya kisera na kanuni za Kudhibiti Rushwa na kutoa Mapendekezo kadhaa ili kuboresha Uwajibikazi, Uwazi na Usawa katika Huduma ya Afya.
Ookay!
 
mkuu ebu toa darasa jinsi ya kununua kitabu hicho kupitia amazon.com; mimi ni member wa amazon, na kuna vitabu vingi vizuri online kule, tatizo ni jinsi ya kununua.

Fungua Amazon.com
Search jina la kitabu mfano 'Sindano inayovuja'
Bofya 'ADD TO CART'
Bofya 'Proceed to Check Out'

Chagua Sheeping Speed: Kila speed ina kiwango tofauti

Chagua aina ya kadi ya Malipo, mimi natumia 'VISA'

Ingiza Anwani yako "Shipping Address' unapotaka kitu kitumwe -Jina lako, Mtaa, Nyumba Number/ Ofisi, P.o.Box, Jiji, Mji, Nchi, Code ya Tanzania weka 00255 na simu yako.
Weka Billing Address; Jina La Benki na Anwani uliyoandika wakati unafungua account mfano:
Jina Kwenye Card: Joseph Pundamlia Malimoto
P.o.Box ....DSM
Tanzania
Mwisho Bofya 'PLACE ORDER'

Utapata confirmation E mail katika e mail uliyoandika yenye order number
Order yako ikitumwa utajulishwa na kupewa Tracking namba kufuatilia kujua ilipo bidhaa uliyonunua

Good luck
 
Breaking news hapo ni nini?
Du haya bwana tutanunua na tusome, ila jifunze jinsi ya kuwasilisha taarifa yako kwa umma
Nashauri kwa maboresho ya baadae

Kwangu mimi kupata dhahabu kama hii ni Breaking News!
 
mi namsubiri yule jamaa anayekuja na Amazon Kindles ili niki download hicho kitabu humo. posta zetu haziaminiki
 
Back
Top Bottom