Elections 2010 Kwa kumuapisha Shein Wamevunja Katiba ya Muungano?

Nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu hii issue ya Makamu wa rais wa Muungano.... nikafuatilia kwa makini kuapishwa kwa Dr Shein nikitegemea wangeeleza nini kinafuata kwa nafasi ya hiyo kwa muda ambao rais hajaapishwa.
Nadhani mwanasheria mkuu alipaswa kulitolea maelezo
 
Mzee MM, ukiwaza sana mambo ya Tz na watz unapasuka kichwa bure. Unashangaa uvunjifu wa katiba pale zanzibar? JK kaivunja mara ngapi? We uliona wapi amiri jeshi kukaa jukwaani kisha mizinga 21 anapigiwa head of state ndani ya state? Kaagwa head of state state kwa mizinga 21, kakaribishwa head of state state kwa mizinga 21. Maana yake ni kwamba kwa sasa Shein anayo mamlaka ya kupiganisha vita.
Hapo vipi?
 
Kwa vile Katiba ya Muungano inasema kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakoma kuwa Makamu kati ya sababu nyingi ni hii:



Kwa maana hiyo kwa vile hadi sasa Rais mpya na makamu wake hawajaapishwa na kwa vile sote tunakubaliana kisheria kuwa bado Kikwete ni Rais halali (kwani naye Urais wake wa miaka mitano unakoma pale atakapoapishwa kwa miaka mingine mitano) hivyo Dr. Mohammed Shein bado ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano - kwani namna nyingine zote za kuuondoa Umakamu kwa Mujibu wa Katiba hazihusiki


Na kuwa Katiba ya Muungano inatangulia kusema kuwa:




Sijui inawezekana kuwa sasahivi:

JMT - haina makamu wa Rais kwa vile aliyekuwa Makamu wa Rais ni Rais wa Zanzibar? Kama ni kweli, amepoteza umakamu wake vipi wakati Rais mpya na Makamu wake hawajaapishwa bado?

Kulikuwa na haraka gani ya kumuapisha Rais wa Zanzibar wakati bado ni makamu wa Jamhuri ya Muungano? Labda ninausingizi kuna kitu kimenipitia, naomba msaada.
Mwanakijiji,
kosa moja hupelekea la pili na kadha wa kadha. Wamebaka kura za wananchi. na sasa wanaibaka katiba.
nchi yao hii tuzidi kuwazua namna ya kuwasaidia na kuwaelimisha watanzania wenzetu. it will pay
 
Katiba ya JMT kwa masuala yanayoigusa Zanzibar imekuwa kama haipo vile. Wanaposema Zanzibar ni NCHI katiba ya JMT haisemi hivo. Walipompigia mizinga 21 Rais Karume kumuaga walikuwa na maana gani? Juzijuzi hapa tumeona Karume anawapa kamisheni wanajeshi wa vikosi vyake eti naye sasa Amiri Jeshi wa Vikosi vya Zanzibar! Makubwa zaidi yanakuja. Wewe subiri serikali mpya zianze kazi wiki ijayo.
Wakati huohuo wanakataa Mabadiliko ya katiba! KWA KWELI HUU NI UGONJWA NA UNAPOLEA UBOVU BAADAYE YAKAFUMUKA INAKUWA WORSE!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom