Kwa kauli ya nassari inabidi chadema wasitishe kwanza sera yao ya majimbo otherwise itatucost.

Mkuu wangu kauli kama hiyo ya kutenganisha umoja wetu ni ngumu kusahulika.

Hivi kiasi CCM wanavyoichukia CDM na wanachama wake huu umoja upi unaouzungumzia? Acha ya CDM mbona nyinyi wenyewe mnatafunwa na makundi ndani yenu umoja upi mlionao? Acha hilo JK alifanya kampeni misikitini kwa misingi ya udini hapa Arusha kuelekea uchaguzi wa 2010 na kuwakandia wasio waislamu huo ndio umoja?

Nakushauri usidandie mijadala kwa mbele kama unadandia gari moshi kwa mbele kwa ajili ya njaa utateketekea tutakosa hata maiti ya kuistiri.
 
Duh, jamani muacheni Mheshimiwa Nassari achape kazi.....that waz politics also na ametoa maelezo ya kufafanua nini alimaanisha kwa hatuba ile.....Hata hivyo maelezo yake yamefikishwa kwa DPP kwa hatua zaidi....naamini hana Kessy ya kujibu....ni mizunguko tu ya Chama Tawala katika kuelekea kufa
 
....Hawa Magamba na vyombo vyao vya dola ni Vingwendu wa hali ya juu!!! Mafisadi makina Mkapa, Mzee wa Vijisenti, Rostam Aziz, Lowassa na wengineo chungu nzima wameshindwa kuwapandisha kizimbani kwa ukwapuaji wao wa mbailioni ya pesa za walipa kodi...lakini leo hii Nassari kutoa kauli moja tu basi wamemshupalia kutaka kumfungulia mashtaka!!!!! Nchii hii ni ya ajabu sana ndio maana badala ya kupata maendeleo inazidi kudidimia kimaendeleo miaka nenda miaka rudi....
 
Polisi mkoani Arusha, wamefikisha jalada kwa Mkurugenzi wa mashataka kulipitia na kuona ikiwa kuna substance tosha kumfikisha mahakamani Nassari na Heche kwa kosa la kusambaza chuki miongoni mwa jamii dhidi ya serikali kwa maneno waliyotamka jukwaani katika mkutano wa hadhara.
Tusubiri na kuona
Wanatapatapa na kujipendekeza kwa ****** tu,ila wajue ndio wako kwenye their final breath!future yao ni yenye giza nene!na huyo Riz ndio ajue amejijengea maadui wengi sana nchi hii kutokana na madudu anayofanya chini ya kivuli cha baba yake,ajue kabisa kikomo cha dhambi zake ni pale baba yake atakapokaa pembeni kama rais wa Tanzania,kama ajuhi jinsi Watanzania wengi wanavyomchukia atakuja kujua ikiwa late,ni bora mdogo wake Miraji hasiye na adui yoyote,maana yeye kajiamulia kula shangwe zake bila kumkera mtu!Riz ajiulize kuanzia Julius,Ally Mwinyi mpaka Mkapa hao wote walikua na watoto wa kiume mbona hatujawahi kuwasikia kuhusishwa na kashfa au kuchukiwa kiasi hiko na Watanzania?kwa nini yeye tu?watch out Riz
 
Mkuu wangu MM,

Unajua kuna wakati napata hofu juu ya huu mwenendo wenu hapa jamvini.Mtu akitenda kosa anaangaliwa anatoka chama gani kwanza ha ha ha ha.


Ngongo,
Baada ya Godbless Lema kumkabidhi mikoba ya uwakilishi wa Arusha mjini Joshua Nassary kwa wakati huu anaposhughulika na kesi yake, basi na wewe umeamua kuhamishia chuki zako dhidi ya Lema kwa Nassary!? i didn't know kwamba una wivu kiasi hicho:thinking::thinking:
 
Ukweli Hii nchi ishakuwa kubwa sana kuliko uwezo wa wanaoiongoza, ni bora ikagawanywa vipande hata kumi zikapatikana nchi ndogo ndogo zinazojimudu kiongozi.

Nchi zote za Africa zenye eneo kubwa chini ya rais mmoja zimethibitika hazijiwezi kimaendeleo ispokuwa maeneo fulani tu ya nchi husika mfano


Congo jamuhuri Kmsq 350,000 hivi watu 4m kipato cha chini $3,900
Tanzania KmSq 945,000 watu 40m GDP $725
Nigeria Kmsq 924,000 wat 155m GDP $ 1200
DRC Kmsq2.3m watu 71mil GDP $800

Angalia Gabon, ghana, ivory coast, cameroon zina ukubwa wa almost sawa na congo brazavile na GDP zao ziko juu ya $1000

We need to break this country tanzania, ama kwa majimbo au mataifa huru japo manne au tano
 
Namshangaa kila siku anazunguka zunguka tu!!

Pinda alisema kauli za kuyatenga majimbo yanayochagua upinzani ni bahati mbaya, ulimshangaa sana rejao, sana. Najua pia unamshangaa sana Riz1 kusema raisi hatatoka kasikazini! Matusi ya Lusinde ndo kabisaa, umepigwa na bumbuwaziii! You are a geneous "gamba", nakushauri 2015 uwe karibu na daktari wako usijekufa kwa mshituko!
 
Kwamba CHADEMA imempitisha mtu aliyeweza kutoa kauli hizi za kukitia aibu mapema hivi baada ya kuchaguliwa, inaonyesha CHADEMA kisivyo makini katika kuchuja wagombea ili kupata wagombea walioiva kisiasa.

Huyu mbunge si kaapishwa kiapo cha uaminifu kwa Jamhuri? Ina maana alivyoapa pale alikuwa anafanya mzaha au?

Na CHADEMA wanaposema "ni kauli za kitoto tu" wana maana siku hizi wanapitisha watoto au watu wenye kauli za kitoto kugombea ubunge?


Unafukuza upepo kwa hoja mufilisi, kapitie hoja za magamba akina sofia simba na uvccm bagamoyo ulinganishe
 
polisi mkoani arusha, wamefikisha jalada kwa mkurugenzi wa mashataka kulipitia na kuona ikiwa kuna substance tosha kumfikisha mahakamani nassari na heche kwa kosa la kusambaza chuki miongoni mwa jamii dhidi ya serikali kwa maneno waliyotamka jukwaani katika mkutano wa hadhara.
Tusubiri na kuona

ningekuwa mimi ndiye dpp wala nisingesoma nini kilichoandikwa kwenye hilo jalada. Haya ni mambo ya kisiasa zaidi kuliko kisheria. Wapo wengi tu wametoa maneno kama hayo kwenye majukwaa ya kisiasa na mihadhara ya kidini lakini hajaitwa na polisi kuhojiwa hata siku moja.

Dpp akifuata utaaributi wa kufungua kesi kwa kutumia maneno ya kwenye majukwaa atakuwa na kesi nyingi sana.

 
TAARIFA KWA UMMA

Ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala CCM.


Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.


Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.





Joshua Nassari (MB)
Mei 09, 2012.


Joshua kwanza nakupongeza kwa kuwa ni kijana mdogo sana kuanza kutumika katika nchi ambamo demokrasia yake ni ya maskini kuwalinda matajiri wanaowaibia, wanyonge kuwatetea wanaowaonea, wagonjwa kwatetea wanaowaletea ugonjwa. Ni nchi ambamo katika kipidi hiki bado kuna kundi kubwa haliko huru, kifikra, na kimtazamo. Pole mdogo wangu. Mungu amekutuma, na kawaida Mungu hutuma vijana wadogo.

1. Joshua kwaa maana halisi ni Mungu Huokoa. God rescues. Kwa tafsiri hiyo usiichukue kkirahisi tu, waulize hata wazazi wako kwa nini walikuita 'Joshua' utaelewa. Mungu alikuandaa tangu mwanzo.

2. Dogo kama ulifikiri mtihani umekwisha baada ya uchaguzi, pole. Kwanza kabla sijaendelea zaidi je unaendelea kutekeleza ahadi ya visima uliyotoa, Kama inaendelea kuanzia kesho hamia site (mie mhandisi) fanya kzazi na wananchi, nashukuru kwa kutoa ufafanuzi, untosha, na polisi umewaeleza inatosha. Fanya kazi. Watashindana lakini hawatashinda, watapigana lakini watatawanyika. Na nikuambie, mwishowe uma ndio mshindi usitegemee waweza kuwa wewe. So Endelea kuwatumikia wananchi.

3. Njiani maakwazo ni mengi, mengine yatatokana na wewe binafsi kama hutakuwa makini, marafiki watakukatisha tamaa, wanasiasa wenzako, watu wa karibu ulioowaamini, 'media' zitataka kuuza,wengine watasema 'atatuambia nini kijana mdogo huyu' Nakupa moyo usiwasikiliza, sikiliza sauti iliyokuita mwanzoni na ifuate hiyo. Usishangae hata wazazi wako wakaogopa. Songa mbele wewe ni 'mtumwa mzuri'. Yashinde hayo kwa kufanya agenda za wananchi, endelea na project ya maji kwa visima ulivyoahidi, nafikiri 10 tayari uliahidiwa, hizo ndizo habari tuazotaka kusikia kwa sasa

5. Binafsi nimeridhika na ufafanuzi uliotoa, pengine kwa namna moja au nyingine ulimi uliteleza, wewe ni mwanadamu. wapo walioharibu kuliko wewe. "kunya anye kuku, akinya bata kaharisha", usisahau ni misemo yenye busara na mantiki.Tumikia wananchi, tuko nyuma yako na tunakuombea

6. Joshua Nassari, TUMEKUELEWA SANA

VIVA CDM,Alutta continua josh nasari
 
Mkuu wangu kauli kama hiyo ya kutenganisha umoja wetu ni ngumu kusahulika.

Ngumu kusahaulika kwa sababu inatenganisha umoja wetu ???

Hebu tujikumbushe kauli hii amabyo ndio kauli ya ukweli katika kutenganisha umoja wetu !!!

“Ninyi wanawake wenzangu ambao waume zenu wapo katika vyama pinzani na mnajua wazi kuwa hawawapi ushirikiano wowote katika siasa ya CCM wanyimeni ‘nonino’, muone kama hawatarejea katika chama tawala, nonino nikiwa na maana ya tendo la ndoa,”

alisema Sophia Simba (MB), huku akishangiliwa na wanawake wote kuonyesha kuwa alilolisema limewagusa.

Hii ilikuwa tarehe 20th June 2010.

Hapo Vipi ???? { Hii "Hapo Vipi" - ni kwa hisani ya Edward Lowassa}
 
quote_icon.png
By ritz

Mkuu wangu kauli kama hiyo ya kutenganisha umoja wetu ni ngumu kusahulika.
Babu zako wataikumbuka siku wakiwa Segerea.
 
Ndugu WanaJF,

swala la nasari kwa maono yangu nayachukulia ni mtaji wa Chadema tena mzuri tu.

1. PUBLICITY

katika hali ya kawaida CCM ilitakiwa iwaonyeshe watanzania kuwa chama chao kupitia serikali iliyopo madarakani kinawasikiliza wananchi ndio maana sasa wamebadilisha wawaziri(hata kama hoja ilianzishwa na wapinzani ni watanzania pia kwahiyo mesemo wa serikali sikivu ungekuwa wa kuweka ushawishi) na kuteua wakuu wa wilaya. jamabo la ajabu midomoni mwa makada wa CCM yanatoka maneno sita neno chadema manne yanaendelea kuilezea chadema.

Kwangu Nape anyokazi kubwa.

2. KUIMARISHA NGUVU YA UMA

Wakati CCM inaendelea na mtindo ulele ule wakushawishi dola ichukue hatua dhidi ya Chadema kwa kuonyesha imefanya jambo baya sana lisilokubalika, Chadema wao wanapita kwa wananchi na kuwaeleza shida wanazopata zinasababishwa na CCM na kuwapa matumaini ya kuwa wao ni mbadala hata kwa kukamatwa na kuwekwa rumande na ya kuwa wako tayari kwa hilo katika kutetea haki zao na sio kufumbia macho ufisadi.

Kwa stahili hii CCM haitawakonga moyo wananchi bali itazidi kuwasha moto.


3. HOJA NZURI KATIKA WAKATI USIO MWAFAKA

kutokana na ukweli kwamba asilimia kubwa ya watendaji wa serikali ni MAKADA WA CCM, watakapoendelea na makati huu wa kusimamia hoja isiyo na mashiko wala tija kwa taifa ni wazi makada hawa nao watalazimika kusimamia kauli za viongozi wao. hali hii itasababisha utendaji kuzorota na matokeo yake ni maisha kuendelea kuwa magumu na kwa hali hii mwananchi hatahitaji lolote kutoka kwa kada wa serikali iliyopo madarakani zaidi ya wanatatuaje matatizo yanayoendelea kuwakabili.

Wana CCM wakati umefika wa kuchagua viongozi wenu wanaojua siasa za ulimwengu wa leo.


nawakilisha, kupinga kwa hoja ni sawa.
 
Mkuu wangu MM,

Unajua kuna wakati napata hofu juu ya huu mwenendo wenu hapa jamvini.Mtu akitenda kosa anaangaliwa anatoka chama gani kwanza ha ha ha ha.

Mkuu Ngongo hakuna mtu asiyekosea. Tatizo lenu ni kila mnapopata upenyo wa kumshikia bango kiongozi yeyote wa Chadema anapoteleza basi mnafanya hivyo kwa kiwango ambacho mtu yeyote makini atashtuka kwamba kuna agenda ya siri dhidi yake.
Ni mara nyingi tumeshuhudia kauli mbaya zaidi ya hii ya Nassary kutoka kwa viongozi wa ccm na serikali ambao wanaweza kuviamrisha vyombo vya dola kufanya uhalifu dhidi ya wapinzani wao lakini hatukuwaona mkiwashikia bango kiasi hicho. Pamoja na maelezo ya ufafanuzi yaliyotolewa na Kamanda Mbowe pale pale NMC baada ya kauli ya Nassary lakini kwa makusudi mazima mmeamua kufumba macho na masikio ilimradi mkamilishe majukumu yenu vizuri ya kujaribu kuibrand Chadema kitu ambacho wengine hatuwezi kukubaliana nacho na kuwaacha mkiendelea kupotosha.

Tunafahamu ugomvi wako na Lema, so tunashangaa sasa unaanza kuhamishia mashambulizi kwa Nassary, sasa hapa kwanini tusiamini kwamba una chuki na chadema, na si Lema kama ambavyo umekuwa ukijaribu kutuaminisha siku zote?
Kuna tofauti gani kati yako na nape katibu mwenezi wa ccm anayezunguka vyombo mbalimbali vya habari kueneza propaganda dhidi ya chadema kwa kushikia bango kauli ya Nassary? au wewe ndiye katibu mwenezi wa ccm hapa JF!?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MM,

Si kweli hata kidogo kwangu mimi mwanasiasa yoyote akikosea siangalii chama anachotoka namkosoa,namwonya na kumshauri.Kuna yule mbaguzi wa waTanganyika kule visiwa vya karafuu Bwana Jussa alipotoa kauli zake za kibaguzi dhidi ya waTanganyika nilimkosoa bila kujali anawakilisha chama gani nashangaa inakuwa nongwa Nassari akikosolewa.

Viongozi wa CDM tafadhalini sana msichukie tukiwakosoa,tukiwalaumu,tukiwapa taadhari juu ya mambo yanayohusu nchi yetu tukufu Tanganyika.Leo CDM ni wapinzania wanachukia wakikosolea siku mkiwa watawala itakuwaje ?.

Sina chuki na chama chochote cha siasa ikiwemo CDM mbona namkubali sana John Mnyika kiasi naacha shughuli zangu muhimu kwaajili ya michango yake mjengoni ?.




Mkuu Ngongo hakuna mtu asiyekosea. Tatizo lenu ni kila mnapopata upenyo wa kumshikia bango kiongozi yeyote wa Chadema anapoteleza basi mnafanya hivyo kwa kiwango ambacho mtu yeyote makini atashtuka kwamba kuna agenda ya siri dhidi yake.
Ni mara nyingi tumeshuhudia kauli mbaya zaidi ya hii ya Nassary kutoka kwa viongozi wa ccm na serikali ambao wanaweza kuviamrisha vyombo vya dola kufanya uhalifu dhidi ya wapinzani wao lakini hatukuwaona mkiwashikia bango kiasi hicho. Pamoja na maelezo ya ufafanuzi yaliyotolewa na Kamanda Mbowe pale pale NMC baada ya kauli ya Nassary lakini kwa makusudi mazima mmeamua kufumba macho na masikio ilimradi mkamilishe majukumu yenu vizuri ya kujaribu kuibrand Chadema kitu ambacho wengine hatuwezi kukubaliana nacho na kuwaacha mkiendelea kupotosha.

Tunafahamu ugomvi wako na Lema, so tunashangaa sasa unaanza kuhamishia mashambulizi kwa Nassary, sasa hapa kwanini tusiamini kwamba una chuki na chadema, na si Lema kama ambavyo umekuwa ukijaribu kutuaminisha siku zote?
Kuna tofauti gani kati yako na nape katibu mwenezi wa ccm anayezunguka vyombo mbalimbali vya habari kueneza propaganda dhidi ya chadema kwa kushikia bango kauli ya Nassary? au wewe ndiye katibu mwenezi wa ccm hapa JF!?
 
hapo ndio pale siasa za Tz zinaponiacha hoi. Nasari amechemka na inabidi chama ki-moderate hotuba zake zote zitakazofuatia. Cha kushangaza kuna watu wanatetea upuuzi wake kisa wao ni wanachama/wapenzi/mashabiki wa CHADEMA. Ndivyo hivihivi itakavyokua atakapoiba pesa za umma Chadema ikiwa madarakani, bado kuna watu watakaotetea. Na hili ndilo tatizo kubwa walilonalo CCM sasa hivi. Kwa stahili hii ya kutetea kila kitu kisa ni mtu wa chama chako amefanya, utawala wa CHADEMA utakuwa sawasawa na utawala wa CCM.
 
Back
Top Bottom