Kwa kauli ya nassari inabidi chadema wasitishe kwanza sera yao ya majimbo otherwise itatucost.

Mbona Zanzibar inataka kujitenga na wala hakuna anaekamatwa? au Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?

Dogo janja amewazidi maujanja MABOLISI wa Kiwete. Hakuna kesi hapo baali ni kutaka kuwasumbua Wabunge wa CHADEMA ili washindwe kutekeleza majukumu yao ya Kibunge kama walivyodhaminiwa na Wananchi. Mimi nimeshauliza kwenye mtandano huu kuwa HIVI JOSHUA NASSARI ANA UBAVU GANI WA KUMZUIA KIWETE KUINGIA ARUSHA AU ANA NGUVU GANI YA KUITENGANISHA ARUSHA NA TANZANIA kama siyo uzezeta wa Jeshi la Polisi???

Ni kweli tumesikia kauli za Wazanzibar wakidai KUJITENGA NA MUUNGANO. Mbona hatujasikia MAFAILI YAO YAKO KWA DPP????

Polisi hebu acheni upuuzi wenu huo maana kwa kweli mnatukera Watanzania. Mimi naomba tu kuwa 2015 ifike mapema WATU WACHUKUE NCHI. Na kitu cha KWANZA KABISA KUFANYA BAADA YA RAIS WETU KUAPISHWA NI KUMPIGA CHINI IGP MWEMA PAMOJA NA WAKUU WOTE WA POLISI MIKOA kama alivyofanya Rais mpya wa MALAWI Bibi JOYCE BANDA.

Jeshi la Polisi Tanzania hasa Mikoa ya Arusha na Mwanza Pambaf zenu kabisa kabisa natamani hata leo hii yatokee mabadiliko ili muwekwe pembeni. Peeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeelz Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer!!

Ng'wabeja sana ng'wanawane.
 
Mbona Zanzibar inataka kujitenga na wala hakuna anaekamatwa? au Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?

Yaani unataka kusema huoni tofauti ya Meru na Zanzibar ktk Tanzania?
Naona mtu anamkimbiza kichaa uchi, baada ya kichaa kuchukua nguo zake!
Nahisi hili tamko limetolewa na wabaya wake, ili kuendelea kumchafua! Kwanini asiombe radhi hata kwa wanachadema waliopata usumbufu wa kuitafsiri kauli yake?
Kama ni tamko la Nassari, amechemka tena! Lakini bado ana nafasi!
Mungu wetu anaita!
 

Sina ugomvi na Dogo Janja ila akiteleza lazima tumwambie ha ha ha.
Ngongo,
Baada ya Godbless Lema kumkabidhi mikoba ya uwakilishi wa Arusha mjini Joshua Nassary kwa wakati huu anaposhughulika na kesi yake, basi na wewe umeamua kuhamishia chuki zako dhidi ya Lema kwa Nassary!? i didn't know kwamba una wivu kiasi hicho:thinking::thinking:
 
Last edited by a moderator:
Threads za umbea na ushabiki wa kukurupuka Rejao anazipenda sana,kwa nini usijunge na bendi mojawapo ya taarabu? pele kwa mzee Yusuph paweza kuwa mahali sahihi
 
Taarifa hii imekaa vyema, yeyote atakayeshindwa kumuelewa basi ana sababu zake zingine, na labda alikuwa anatafuta sababu!!!
 
... Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndio msimamo wangu ....​
sasa Nassari si ungesema tu huo msimamo wako, kuliko kusema "alichosema mwenyekiti ndio msimama wangu" !! Wengine hatukumsikia mwenyekiti wako. Hautakuwa tofauti na wale wanaoamka usingizini na kusema "naunga mkono hoja", akiulizwa hoja gani, atakuambia "hiyo iliyokuwa inajadiliwa". Funguka waziwazi, wengine tupo CHADEMA lakini hatupo huko kaskazini, tuambie nafasi yetu basi!​

 
CHADEMA kwa sasa ndiyo kimbilio la wengi hasa waliochoshwa na chama MFUU cha CCM sasa ushauri wangu chungeni sana kauli zenu mnapokuwa majukwaani, kwani mfaa maji CCM yeye anatafuta weak point ili ajiinue. Pia tunawategemea the seniors to mentor and couch the juniors on good politics that will sustain our party indivisibly. Hatutaki SUGU naye akisimama aongee maneno hayo hayo. Sitaki nisikie tena maneno ya kitoto kama hayo yanakatisha tamaa! Tatizo ni kwamba CCM they are opportunist.
 
japo inauma lakini NASSAri amedhihirisha siasa hajui anakurupuka ili kujipatia popularity ya kijingatu
ni mwehu mwendawazimu anaepaswa kupuuzwa kwa nguvu zote

baadae atakuja na ukanda, udini na ukabila


Hapana. Hayo hapo kwenye red hayawezekani.

Kinachowezekana hapa ni UJINSIA. Usishangae....... Soma hapa chini ili uone:-

Tarehe 20th June 2010 Mheshimiwa Sophia Simba (MB) alisema:-

“Ninyi wanawake wenzangu ambao waume zenu wapo katika vyama pinzani na mnajua wazi kuwa hawawapi ushirikiano wowote katika siasa ya CCM wanyimeni ‘nonino’, muone kama hawatarejea katika chama tawala, nonino nikiwa na maana ya tendo la ndoa,”

alisema Sophia Simba (MB) huku akishangiliwa na wanawake wote kuonyesha kuwa alilolisema limewagusa.

Upo hapo ?????????
 
walionzisha hiyo movement wote wamekamatwa! Na kesi inaendelea. Nasarri by this time ingetakiwa awe rumande

acha kudanganya wewe wote walioanzisha ile movement kule zanzibar hakuna aliyekamatwa, ila kuna kikundi cha wahuni kilienda baraza la wawakilishi bila taarifa ndio hao waliokamatwa mpaka sasa wapo lumande na wameshapandishwa mahakamani,

mashujaa-430x320.jpg
 
Yaani unataka kusema huoni tofauti ya Meru na Zanzibar ktk Tanzania?
Naona mtu anamkimbiza kichaa uchi, baada ya kichaa kuchukua nguo zake!
Nahisi hili tamko limetolewa na wabaya wake, ili kuendelea kumchafua! Kwanini asiombe radhi hata kwa wanachadema waliopata usumbufu wa kuitafsiri kauli yake?
Kama ni tamko la Nassari, amechemka tena! Lakini bado ana nafasi!
Mungu wetu anaita!
Kama vipi hulitaki basi toa lako tulione.
 
And that is it, can we please move on? Kujadili kitu kisicho na masilahi kwa taifa kwa mda mrefu hivi ni u-negative wa mawazo. Kuna mangapi mazuri ya Nassari na cdm hatutaki kuyasikia na kuyajadili? Nassari is more than that, ndo maana akaibwaga ccm Arumeru, and there are more to come. Tunajua kilichofanyika Meru kime sababisha mtikisiko mkubwa kwa siasa za Tz, na tunatarajia mazuri kwake, wasiompenda wanasubiri akosee wamponde! Ukweli ni kwamba atafanya mengi mazuri, lakini Nassari siyo malaika, atakosea pia.
 
Hebu tuondelee huo upuuzi hapa! Na wewe naye ni mbunge? Nani asiyejua chama chenu ni cha kikanda na kidini?
 
Msamaha wa nini.RIZ ONE aliesema rais hatatoka kaskazini kwanza atiwe mbaroni zandiki yule.! Inaniuma wezi wanaachwa wanaonewa wanaotoa civil education.AKAMATWE ismail jussa ladhu..shit

Kamanda Dalai, nadhani wengi wamwemwelewa Mb.Nasari, ila mi namshauri apate kitu kinaitwa 'DEVELOPMENT FEEDBACK' ili awe makini zaidi. Sisi hatutamwacha ikibidi tutamfinya ila hatumwachi. Na magamba wajue kwamba hii issue haiwahusu na wasitufundishe la kufanya.
 
Threads za umbea na ushabiki wa kukurupuka Rejao anazipenda sana,kwa nini usijunge na bendi mojawapo ya taarabu? pele kwa mzee Yusuph paweza kuwa mahali sahihi
Kwahiyo kumbe hili tamko la Nasarri alilolita hapa crashwise ni umbea??? Ngoja niondoke tu kwenye hii thread cuz ni ya kimbea!!
 
Akifunguliwa kesi watawasha moto mkubwa sana,kwani kuna matamshi mengi sana nchi hii yasiyochukuliwa hatua,kwa kuwa magamba wana fikiri oposite wanaweza kufungua kesi,hapo ndipo kijana atapanda chati vibaya sana.
 
sasa Nassari si ungesema tu huo msimamo wako, kuliko kusema "alichosema mwenyekiti ndio msimama wangu" !! Wengine hatukumsikia mwenyekiti wako. Hautakuwa tofauti na wale wanaoamka usingizini na kusema "naunga mkono hoja", akiulizwa hoja gani, atakuambia "hiyo iliyokuwa inajadiliwa". Funguka waziwazi, wengine tupo CHADEMA lakini hatupo huko kaskazini, tuambie nafasi yetu basi![/LEFT]

[/CENTER]


Hataki kurudiarudia maneno kwa vile huwa mnatafiri tofauti!!
 
Back
Top Bottom