Kwa kauli ya nassari inabidi chadema wasitishe kwanza sera yao ya majimbo otherwise itatucost.

Jussa ,lusinde na magufuli mzee wa mbizi waombe radhi kwanza.waachwa fisadi riz na kina maige,nyalandu ngeleja kupelekwa kortini ,maneno mepesi ya nasary yafatiliwe?ajabu.ASIYE NA KOSA AWE WA KWANZA KUMNYOOSHEA KIDOLE NASSARY.
 
Nilishasema hapa JF na huwa nasema kila mara, wabunge wa CDM hawajitambui. Wengi wameshinda ubunge kihuruma huruma tu kwasabu tunazozifahamu sisi. Tumeona wengi wakijiongelesha tu bila kupima wanachoongea kina impact gani. Cha muhimu ni viongozi wao wawaweke chini na kwaeleza na kuwafunza nini kinahitajika kusemwa wakati gani na mahali gani.

Mramba alisema watu wale nyasi lakini ndege ya rais itanunuliwa alikuwa anajitambua? Acha fikra za kinafiki wewe. Mramba alisema hayo akiwa Waziri wa Fedha, mtu mwenye familia, mmwenye uzoefu na utumishi mpana serikalini, mwenye uzoefu mkubwa ktk siasa, umri wa makamo, nk, Nassari kijana mdogo tu asiyekuwa na uzoefu wa kutosha ktk siasa kuteleza tu umekuwa wimbo wa Taifa?!! Wasiojitambua wako CCM kibao. Toa boriti kwanza ndani ya jicho lako ndo umwambie mwenzio ana kibanzi.
 
Acha kufikiria kama uko ndani ya chupa.....kashauriwa kuomba msamaha kwa jamii for the sake of his own reputation.......ujasiri kama wako bila busara ni ujinga pia

Umesema kashauriwa kuomba msamaha.
Swali ni dogo saaana:-
Aombe msamaha kwa kosa gani??
Hivi ninyi wote mnaosema 'aombe msamaha' mnashindwa kutaja kosa ambalo anatakiwa aliombee msamaha ???
Ukisema 'aombe msamaha', toa nukuu ya kipande cha hutoba husika ambacho anatakiwa 'akiombee msamaha'
 
hakuna kuomba msamaha hapa!
ccm wao ndo kwanza huwa wanaongea sana ubaguzi kwanza wameomba msamaha kwaa kuua watanzania!??

Ccm wameikosea jamii ya watanzania, adhabu wanayopata ni kukimbiwa, na wamehadiwa kupigwa chini kabisa 2015. Sasa, kama unadhani chadema haiwezi kukimbiwa hata itufanyie maovu kiasi gani, utakuwa umekosea. Ccm wanashtumiwa kuiba mali za umma, je chadema nayo ifanye hivyo kwa sababu wenzao wamefanya! Sio vizuri kuanza kufananisha matukio, eti mbona Lusinde kafanya hivi... inawezakuwa kauli ya Lusinde ilivulisha gamba mamia. Unadhan kauli ya Nassari haiwez kuwavulisha gwanda raia? Chadema isikae kimya kama inataka kuiangusha ccm, huo ni mtaji wa kisiasa pande zote mbili, inategemea tu watautumiaje.
Mungu wetu anaita!
 
Haombe msamaha ili iweje?wewe ndio unaikuza hii hoja mwenyewe kashaitolea maelezo na mwenyekiti ameshaclarify ww unakurupuka eti aombe msamaha ili iweje?awaridhishe ccm?hiyo ni nidhamu ya uoga acha ujinga bwana.
 
Mnalazimisha Nasary aombe radhi.. Kwa maneno gani aliyoyasema..? Na yameleta impact gani kwa hao aliowaambia..? Hivi hayo mnayodai kayasema Nasary mnaweza kufananisha na yale yanayofanywa na CCM..? Imefikia mahali Serikali haipeleki maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na upinzani.. Wilayani Sengerema Madiwani wa CCM wamehamisha mradi wa kujenga shule toka kwenye kata kisa tu kata hiyo kuongozwa na CDM pamoja na kwamba ilikidhi vigezo vya kupata mradi huo..! Impact kubwa ni ipi..? Kwa yule mnaedai alisema kwenye mkutano au kwa hawa wanaonyimwa maendeleo kisa wamechagua upinzani..? Nasary alitumia neno "iwapo".. but CCM wana-practice kabisa ubaguzi wa kuwabagua watanzania.. Acheni undimilakuwili huo..Ninaamini watanzania walio wengi wameamka na wanaelewa ni nani anaestahili kuomba radhi kwa kuhatarisha ustawi wa taifa hili..
 
Ni wazi kwa maneno uliyoyatoa pale NMC sasa yanachukua sura mpya na pana zaidi ya ulivyo firiki,Tunafahamu ilikuwa ni hamasa na haukudhamiria kama tunavyo jaribu kuaminishwa kwa sasa,Ni ukweli siopingika sasa kuwa umewàpa CCM maneno ya kuongea,Watanzania tanafahamu kuwa kujisaidia ajisaidie Kuku akijisaidia Bata kaharisha,kwa nia njema tu na kwa ushauri wa bure JITOKEZE HADHARANI NA KATIKA VYOMBO VYA HABARI OMBAMSAMAHA.Hàita kupunguzia kitu bali itakuongezea heshima mbèle ya jamii,maneno uliyo yatamka ni mazito sana haswa kwa jamii ya kitanzania ambayo haina elimu ya kutosha katika kuchambua mambo,na nimepesi sana kwa wanasiasa,kwasasa ni wazi yanakigharimu chama chetu,na nimabaya sana kwako kwani yanagharim katika ulimwengu wa siasa. onyesha dhana ya kuwajibika na urudishe heshima yako na ya chama kwa ujumla.

Nafahamu wewe ni memba hapa JF na utajitokeza

NI MIMI MWANA CHADEMA MTIFU.
Kweli wewe huwezi kuwa mwanachadema Mtiifu wakati hata jina la mbunge unaejaribu kumzungumzia huwezi kuliandika.
Na mbona hujamalizia Nassari aombe msamaha kwa lipi?

Mtajulikana tu hata kwa maandishi yenu.
 
Be the change you preach. Kama unashindwa kuomba msamaha kwa kutoa kauli tata ukiwa bado "mtu mdogo sana katika nchi hii", tutegemee nini pale utakapokuwa kigogo katika nchi hii?

Mnakumbuka mlisema hivi hivi wakati wa swala la wana-chadema 'kumteka' mkuu wa wilaya ya Igunga?
'Maoni' mengi saana yalitolewa, eti 'ooh, chadema waombe radhi wananchi, ooh, chadema iombe radhi wanawake wa Tanzania'.
Na baya zaidi, swala lile (kama kawaida) likakuzwa sana na kupewa sura ya udini, nk., mpaka baadhi ya taasisi za dini zikatoa 'ultimatum' kwa chadema kuomba radhi kwa 'kudhalilisha' muumini wao.
Mnakumbuka ???
Na zaidi ya hapo (kama kawaida) ikafunguliwa kesi kwa mbwembwe saaana.
Swali ... Je leo swala lile liko wapi ???
Watanzania wengi ama ni wanafiki, au ni vipofu saaana wa kuona mbinu za chama tawala kuwabambikizia kesi chadema?
Kila kitu ni wazi kabisa. Chadema inawindwa sana na serikali na vyombo vya dola ili ibambikiziwe kesi.
Kama ni swala la kutoa matamshi ya 'uchochezi', nk., basi kila mtoa maneno ya uchochezi ingebidi akamatwe na polisi.
Ila polisi (kama kawaida) wanachagua nani wa kumkamata. Watanzania bado hawalioni hilo !!!
 
Ni wazi kwa maneno uliyoyatoa pale NMC sasa yanachukua sura mpya na pana zaidi ya ulivyo firiki,Tunafahamu ilikuwa ni hamasa na haukudhamiria kama tunavyo jaribu kuaminishwa kwa sasa,Ni ukweli siopingika sasa kuwa umewàpa CCM maneno ya kuongea,Watanzania tanafahamu kuwa kujisaidia ajisaidie Kuku akijisaidia Bata kaharisha,kwa nia njema tu na kwa ushauri wa bure JITOKEZE HADHARANI NA KATIKA VYOMBO VYA HABARI OMBAMSAMAHA.Hàita kupunguzia kitu bali itakuongezea heshima mbèle ya jamii,maneno uliyo yatamka ni mazito sana haswa kwa jamii ya kitanzania ambayo haina elimu ya kutosha katika kuchambua mambo,na nimepesi sana kwa wanasiasa,kwasasa ni wazi yanakigharimu chama chetu,na nimabaya sana kwako kwani yanagharim katika ulimwengu wa siasa. onyesha dhana ya kuwajibika na urudishe heshima yako na ya chama kwa ujumla.

Nafahamu wewe ni memba hapa JF na utajitokeza

NI MIMI MWANA CHADEMA MTIFU.

kwa mawazo yako sawa watanzania wengi hawana elimu ya kutosha lakini hayo ni matusi.sijui elimu unayoiongelea wewe ni elimu gani.ninavyofahamu mimi watanzania wengi wana elimu ya kutosha ndiyo maana wanafanya mabadliko ya kisiasa,kielimu na kiuchumi pia.swala la nassari ni mchezo tu wa kisiasa.mimi sioni kama ni kitu serious sana ila tu ni mchezo wa kisisa.hata kama kuna watu wamepata sababu ya kusemea lakini ninachokifahamu mimi ni uchanga wetu wa kisiasa na watu kusukumwa zaidi na itikadi zao.hili ni tatizo linaloitafuna tanzania.kuacha ukweli na kusema uongo.
 
japo inauma lakini NASSAri amedhihirisha siasa hajui anakurupuka ili kujipatia popularity ya kijingatu
ni mwehu mwendawazimu anaepaswa kupuuzwa kwa nguvu zote

baadae atakuja na ukanda, udini na ukabila
 
jussa ,lusinde na magufuli mzee wa mbizi waombe radhi kwanza.waachwa fisadi riz na kina maige,nyalandu ngeleja kupelekwa kortini ,maneno mepesi ya nasary yafatiliwe?ajabu.asiye na kosa awe wa kwanza kumnyooshea kidole nassary.
dogo akomae hakuna kuomba msamaha
 
Polisi mkoani Arusha, wamefikisha jalada kwa Mkurugenzi wa mashataka kulipitia na kuona ikiwa kuna substance tosha kumfikisha mahakamani Nassari na Heche kwa kosa la kusambaza chuki miongoni mwa jamii dhidi ya serikali kwa maneno waliyotamka jukwaani katika mkutano wa hadhara.
Tusubiri na kuona
 
TAARIFA KWA UMMA

Ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala CCM.


Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.


Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.





Joshua Nassari (MB)
Mei 09, 2012.
 
CHADEMA ni chama, Nassari ni mwanachama. Swala la Nassari liko kwenye vyombo vya dola linashughulikiwa akigundulika kakosea ataadhibiwa kwa mjibu wa sheria. Mahakama ikiona adhabu ni kuomba msamaha atafanya hivyo ikitokea vingine sawa. Kelele za nini. Mtu ukikosea unaadhibiwa kwa mjibu wa sheria na sio comments za jamii forums. Hili suala CCM wanalikuza wakifikiri ndio dili la wananchi kurudi kwao. Itakula kwao
 
No kuomba msamaha kama hao magamba wamepoteza sera waache wayachukue hayo maneno waone kama kuna atakaewasikiliza. Watanzania si wajinga tena wanachambua mambo kwa kina. Afterall Mh. Mbowe aliweka sawa sasa huo kuomba msamaha kwa nini tena. Tanzania tuna isuess nyingi za kuzijadili tuachane na hizo habari zinazotolewa kutokana na hamasa tu ya majukwaani
 
Joshua Nassari acha kutuzuga kubali ulimi uliteleza omba msamaha waTanzania.
 
hivi wale wa radio imaan na watendaji vibaka wa serikali si wangekuwa wanaozea jela sasa hivi kama kasi hii ya kuwashughulikia cdm ingetumika?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom