Kwa kauli hii, Je Kikwete ni Dikteta??

mkuu L.justice1 kabla hujamlaumu JK ni Dikteta , naomba unipe definition ya Dikteta ...

Yeye (JK) amedai ni "mvumilivu" kwa watu wenye mawazo tofauti lakini tunashuhudia waandamanaji wakiuawa na wengine kutiwa mbaroni! Watu siku hizi wameshazoea mioshi ya mabomu ya machozi na hawaogopi tena! Wewe kwa akili yako unafikiri hiyo ndio "demokrasia" anayoidai JK?
 
lakini tuliona kwa serikali zilizopita mambo hayo yalitokea ... kipindi cha mkapa enzi zile za " CUF ngangari" na pia serikali ya znz kila mtu anajuwa kwamba kila uchaguzi znz CUF inashinda lakini serikali inatumia nguvu ..

but why JK why Now mnamuona yeye dictator...?! hajaingia madarakani kwa nguvu , haja nga`ng`ania madaraka, kuna freedom of speech ... unadhani nchi kama China mitandao kama Jf ina exist! ??

Nilimsikiliza JK bbc akisema kwamba wapinzani mnadai kuwa amepewa madaraka makubwa mno .. lakini yeye JK sio kosa lake katiba ya sasa inamruhusu kufanya hivo.. subirini katiba mpya iundwe ndio tuione je raisi pia ana madaraka makubwa mule kama anayo au hana .... je uma wa tzn WOTE "sio wale wa arusha TU" unakubali ama unakataa hapo kuna kitu kinaitwa KURA YA MAONI wa tanzania wote watashirikishwa kupiga kura ya ndio au hapana....

Njiwa nakubaliana na wewe kwamba Mkapa naye alitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wapinzani wake. Kwa upande wa JK alianza vizuri sana kwa ku-exercise demokrasia ya hali ya juu lakini muda unavyozidi kusogea rangi halisi ya JK inazidi kujidhihirisha kwa maana kwamba uzalendo unazidi kumshinda.
Kuhusu jinsi alivyoingia madarakani haina ubishi kwamba JK aliingia kwa "nguvu" kwa style ya uchakachuaji kura wa hali ya juu! Again, mfumo uliopo ndio umemwezesha kufanya hivyo kwa kuwa Tume ya Uchaguzi iko chini yake!
 
Naomba:1. Afute kesi zote za kisiasa za wabunge na viongozi wa CHADEMA kwa sababu hata CCM Arusha waliandamana bila kibali lakini hawakuchukuliwa hatua yoyote,2. Asisaini Sheria ya kukusanya maoni juu ya Katiba mpya kwa kuwa ina kifungu cha kuzuia watu kutoa maoni kwa uhuru kinyume na Katiba,3. Aruhusu maandamano yote ya amani badala ya kutoa taarifa feki za kiintelijensia za Polisi ili kuhalalisha kunyima watu uhuru wa kuelezea hisia zao,4. Awachukulie wahalifu wote hatua za kisheria kuliko kuwaacha wengine "wapumzike" huku wengine wakikamatwa kila siku na kufunguliwa mashtaka,5.....Otherwise.....
Kwa kigezo chako chenye makengeza hicho, bora aonekane dikteta.
 
Nikimwangali Rais wetu Jakaya Kikwete, naona sifa moja kuu: uvumilivu wa hali ya juu. Kila mara kukitokea jambo fulani huwa napata taswira ya rais "who has broad shoulders". Mtu anayeweza kuvumilia mengi. Sifa hii ni nzuri na inaruhusu uhuru wa maoni na kupanua wigo wa demokrasia Tanzania.

Kwa upande mwingine, rais wetu anaonekana kuwa dikteta anayetabasamu. Yaani, ukiona anatabasamu utadhani anatoa uhuru wa maoni tofauti lakini pia ukiona jinsi vyombo vya dola vinavyofanya kazi na hasa vinapokabiliana na raia unapata picha ya udikteta. Kuna mifano mingi inayoonekana - kutumia mabavu hata mahali ambapo hapastahili na hili limekuwa likisababisha vifo kwa raia kwa kupigwa risasi za moto, majeraha na kesi mahakamani.

Sheria zetu zinaruhusu wananchi kudai haki zao kwa njia mbalimbali bila kuvunja sheria. Kufanya maandamano ni njia mojawapo ya kikatiba ya kudai haki na njia hii imekuwa ikitumiwa na wanafunzi hasa wa chuo kikuu, wafanyakazi na vyama vya siasa. Lakini taratibu taratibu polisi wamekuwa wakijifanya wao ndio wanaotoa kibali cha kudai haki hasa pale yanapokuwa kwa njia maandamano badala ya kutoa ulinzi kwa wananchi na mali zao. Na mara kadhaa rais amekuwa akisikika akisema: "wataoandamana watakiona... kama wanadhani ninatania waandamane..."

Kuandamana hapa Tanzania kumekuwa kukitafsiriwa "kufanya fujo" ingawa kufanya fujo siyo sawa na kuandamana. Msimamo huu unakinzana na sifa ya kuvumilia wa maoni au misimamo tofauti ya vyama vya siasa. Pili, katika hotuba yake ya hivi karibuni, rais alitumia muda mwingi kuongelea hotuba ya Chadema bungeni. Kama rais anatoa fursa watu watoe maoni yao kuhusu nchi yao kwa nini ana mawazo hasi kuhusu maoni ya Chadema juu ya mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya? Huku ndiko kutoa uhuru wa maoni/mawazo?

Naomba tuelemishane.
 
mnakwenda ikulu kujadili na dikteta mmmmh nani anachochea udikteta? kumtambua dikteta na kwenda kuzungumza naye ni kuchochea udikteta
 
wanafiki ni wale ambao leo wanasema hatumtambui Jk kesho wanasema kawaibia kura na kesho kutwa wanaomba kula na kunywa naye meza moja
 
wanafiki ni wale ambao leo wanasema hatumtambui Jk kesho wanasema kawaibia kura na kesho kutwa wanaomba kula na kunywa naye meza moja

Ukiwa CCM akili unakuwa umepokonywa sijui mnakuwa mnatumia akili za watoto wenu. Tunaangalia katiba inasema nini? ndo maana wastaarabu sana
 
vilaza ni wale wanaoona kwamba ccm kuunda serikali na CUF ni ndoa ya mume na mke lakini yule anayeandika barua ya kuomba uchumba kwa mume wa mtu (CUF) hana nia mbaya ya kuvunja ndoa ya CUF. mbaya zaidi ndoa ya chadema na ccm inakwenda kufanyika Ikulu.
 
Ukiwa CCM akili unakuwa umepokonywa sijui mnakuwa mnatumia akili za watoto wenu. Tunaangalia katiba inasema nini? ndo maana wastaarabu sana

wewe unaniona mimi tu chadema wenzio akaaa? wafuasi wa chama chako wanaacha kujadili hoja wanatukana...... kama mjadala unanoga kwa matusi basi tuendelee. wote tunaharibu JF yetu .....jukwaa huru
 
kumbuka uhuru wa kusema katupa JK kuna nchi kama china na nchi za kiarabu kama Irani na Saudi Arabia wanfunga mitandao kama hii. tumpongeze Jk kwa kuwa baba wa demokrasi ya kweli na ndio inamtafuna.
 
vilaza ni wale wanaoona kwamba ccm kuunda serikali na CUF ni ndoa ya mume na mke lakini yule anayeandika barua ya kuomba uchumba kwa mume wa mtu (CUF) hana nia mbaya ya kuvunja ndoa ya CUF. mbaya zaidi ndoa ya chadema na ccm inakwenda kufanyika Ikulu.

Chadema ni bora imuoe DP ya Mtikila kuliko CCM ya M#kwere
 
Back
Top Bottom