Kwa kauli hii, baraza la mawaziri linapashwa kujiuzuru

Lusambara

Member
Oct 31, 2010
38
9
Ndg zangu wana jf, nimefuatilia mjadala wa suala la jairo leo bungeni. Wabunge wengi wa chama tawala, wameishia kusema kwa hofu na kushindwa kuweka wazi tatizo lilipo hasa.

Katibu mkuu kiongozi ambaye ni katibu wa baraza la mawaziri alikiri kwa kusema ‘suala la jairo kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanikisha bajeti ni suala la kawaida kufanywa na wizara na yeye hajaona kosa loloe katika hilo’ hili lina maana kuwa kila wizara inafanya hivyo na kwa hali ilivyo wala haliko kwa jairo tu. ila yeye anatolewa kama kondoo wa kafara kwa ajili ya wengine. Na kama kweli tunaipenda nchi hii, basi baraza lote la mawaziri linatakiwa kujiuzuru.

Nina wasi wasi mkubwa na taarifa ya cag kuhusu na suala la udom ambalo aliambiwa alifanyie ukanguzi pia. Kama la jairo limekuwa hivi, inaonekana hata lile la udom alilichakachua na akatoa ripoti inayopendeza matakwa ya waliompa ugali.

Kwa ushauri wangu ingekuwa vema kama baraza lote lingejiuzuru ili kuweka bayana udhaifu uliopo kuliko kutoa kondoo wa kafara.
 
Serikali hii haiwezi kujiuzulu,kwanza inaendeshwa na viongozi wasio waadilifu (makini) wenye dharau,wsijala utawala bora.
Jibu la hii serikali ni wananchi kuwakataa katika masanduku ya kura basi,tuvumilie tu hadi uchaguzi ujao.
 
Tutavumilia lakini tunafanyaje pale ambapo CCM wanakuwa wameaandaa Katiba ambayo itaendelea kuwaweka madarakani?je uvumuilivu wetu utakuwa na tija?je tunauhakika gani baadhi ya railimali zetu zinazohamishwa kila siku kupelekwa ulaya kama zitakuwa zimebaki bado siku amabpo uvumilivu wetu utakapoleta tija?Mi nadhani tuondoe woga tuungane kudai haki yetu kwa umoja wetu tena kwa vitendo,na njia pekee ni nguvu ya umma
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Katika Nchi Hii japo wanasema wananchi ndo wafanyao maamuzi, lakini maamuzi pekee tuayoweza kufanya kama watanzania ni 'Kulalamikalalamika' kisha mambo yanafunikwafunikwa, life goes on!
 
Kama mmeshindwa waombeni NATO wawasaidie kutatua matatizo yenu halafu baada ya kumaliza kazi mliyowatuma mtawalipa kwa URANIUM mliyogundua huko Songea!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
The Jairo's issue was an organised crime.......

I can imagine how safe r we with such issues being organised before people's faces huku briefing zikifanywa kila iitwapo leo! Alafu wakija sebuleni kila mtu anajidai hajui, so interesting...Hivi kweli unaweza kujiibia mfukoni mwako? The devil is a liar!
 
:A S embarassed:Hawaii ccm Mwishowao unakaribia na wanamacho hawataona na wanamasikio hawata sikia
 
Hawaii ccm Mwishowao unakaribia na wanamacho hawataona na wanamasikio hawata sikia
 
kinachonipa tabu kuamini ni kuwa UTOUH alifanya haya yote kwa ajili ya nini ?? nalazimika kuamini huenda kuna mkono wa rais ndani au Luhanjo ndio uliomfanya apindishe mambo la sivyo sioni kunuifaika kwake na yeye kumlinda Jairo.
 
UTOH hafai tena kuwa mkaguzi mkuu wa serikali ni mwizi pia kama wengine hii ni serious mistake ya pli ameiangusha taaluma yake nani atamwamini tena mwizi
 
Ndg zangu wana jf, nimefuatilia mjadala wa suala la jairo leo bungeni. Wabunge wengi wa chama tawala, wameishia kusema kwa hofu na kushindwa kuweka wazi tatizo lilipo hasa. Katibu mkuu kiongozi ambaye ni katibu wa baraza la mawaziri alikiri kwa kusema ‘suala la jairo kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanikisha bajeti ni suala la kawaida kufanywa na wizara na yeye hajaona kosa loloe katika hilo’ hili lina maana kuwa kila wizara inafanya hivyo na kwa hali ilivyo wala haliko kwa jairo tu. ila yeye anatolewa kama kondoo wa kafara kwa ajili ya wengine. Na kama kweli tunaipenda nchi hii, basi baraza lote la mawaziri linatakiwa kujiuzuru. Nina wasi wasi mkubwa na taarifa ya cag kuhusu na suala la udom ambalo aliambiwa alifanyie ukanguzi pia. Kama la jairo limekuwa hivi, inaonekana hata lile la udom alilichakachua na akatoa ripoti inayopendeza matakwa ya waliompa ugali. Kwa ushauri wangu ingekuwa vema kama baraza lote lingejiuzuru ili kuweka bayana udhaifu uliopo kuliko kutoa kondoo wa kafara.
Hivi uliambiwa kwamba Katibu wa Baraza la Mawaziri akikosea basi baraza zima lina makosa? Mbona reasoning yako haizingatii hali halisi ya mambo? Hivi unajua kazi za katibu wa baraza ni zipi? Rudi shule ukajifunze tena halafu uje tusome ukurasa mmoja!
 
Back
Top Bottom