Kwa Jina la CCM: Mbunge wa Mtera Lusinde aporomosha matusi Arumeru kumwombea kura Siyoi

Ndugu wanaJF
mimi nimesikiliza mwanzo mpaka mwisho na nimeelewa maneno/matusi yote yaliyotajwa na mhe.lusinde isipokuwa hili neno KUDADADEKI . Kama kuna mtu mwenye tafsiri ya hili neno anisaidie........................
 
Ama kweli hizi ni nyakati za mwisho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?
 
Du huyu jamaa kweli kiboko, ndiyo maana Mzee Malecela ameugua sababu ya matusi kama haya!!! Duh kweli Magamba kiboko.
 
Wanafikiri wanajijenga kumbe wanajibomoa, hao watu wa Meru kama huwajui wanachukia matusi kwa sababu si jadi yao!!!!
Kwa hiyo CCM wanazidi kujimaliza, hawana sera ya maana tofauti na matusi, hawana jipya mpe Nassari kura aende kushiriki na wapambanaji wenzake kurudisha mashamba ya Dori Farm yaliyo dhulumiwa na watawala!!!!!!

Kazi kwenu wana Arumeru, sisi tunawatia hamasa songeni mbele kwenye uchaguzi!!!!

 
huyu jamaa ni wakuombewa tuuu!
na Huyu eeeti ndo alimtoa Malecela (Tingatinga)
 
Ndugu wanaJF
mimi nimesikiliza mwanzo mpaka mwisho na nimeelewa maneno/matusi yote yaliyotajwa na mhe.lusinde isipokuwa hili neno KUDADADEKI . Kama kuna mtu mwenye tafsiri ya hili neno anisaidie........................
Mkuu hilo neno linahistoria ndefu!
Linatokana na Tusi k ya mama yake,
likaja k mamaaaye
ndo hilo kudada deki mkuuu,
kwa historia yake ni tusi lilelile.
helufi K linawakilisha kifaa cha mwanamke!
 
huyu jamaa ni wakuombewa tuuu!
na Huyu eeeti ndo alimtoa Malecela (Tingatinga)
Hata mimi najiuliza alimshindaje Malecela?
Hawa ndio baadaye tunasikia Kikwete amemteua ndugu Lusinde kuwa waziri wa nishati na madini.
 
Binafsi sijapendezwa na mwenendo mzima wa siasa za Tanzania. Wakati nikimsikiliza mbunge huyu ambaye sithubutu tena kumwita mheshimiwa , wazo lililoniijia ni kuwa ametumia aina ya kilevi kama bangi kabla ya hotuba yake. Katika hali ya kawaida, maneno kama haya yamezoeleka kwa watu waliokata tamaa na maisha na kugeukia katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Kuyasikia yakitoka kwa mbunge wa nchi masikini kama hii ni ISHARA TOSHA KUWA UMASIKINI WA TAIFA LETU SI WA MALI BALI AKILI. Pamoja na hayo yote bado sijatia akili kuamni kama ALITUMWA NA CHAMA CHAKE AU NI MAAMUZI YAKE BINAFSI.

CCM INATAKIWA ICHUKUE HATUA DHIDI YAKE KAMA MANENO ALIYOYATAMKA mbunge huyu HAYAHUSIANI NA CHAMA
.
Mwisho niwape pole wananchi wa Mutera.
A%20S%20cry.gif
 
Ki-Ccm ccm huyu ni shujaa mkubwa! baada ya kushuka pale alisifiwa sana! usishangae akapewa ile kazi ya Nape!
 
Makubwa...madogo yananafuu..siasa za kupakana matope hizo. Siku zote ukiishiwa maneno basi lolote litakalotoka kinywani mwako waweza kuzani ndo sera. Mungu ibariki Tz na watu wake!
 
jamaa amefanya kweli. audio na video ziko vizuri ila kwa sababu ya net bongo ziko slow its better kama utadownload. nenda kwenye google search for FREE YOUTUBE downloader. ukiipata install halafu ukifungua you tube unacopy URL na kuipeleka kwenye youtube downloader ili uihifadhi kwenye computer ili uziangalie taratibu.

ahsante mkuu
 
Mungu atusamehe kwa uovu huu!Mungu itakase Tanzania, na utusamehe dhambi zetu zote!
 
Wabunge wa aina hii huwezi kuwaona wakichangia hoja nzito bungeni,wanangojea kwenye maneno ya udaku tu ndio utawasikia.Mungu tuepushe na wabunge aina ya lusinde
 
Back
Top Bottom