Kwa hilo Nagu kachemka!

Hata mm hiyo kauli imenistua sana!!! Kiukweli nimeogopa!!!! Kumbe wanafanya makusudi ee! Na kodi zetu wanazitumia watakavyo! Kuchelewesha miradi kisa tumechagua wapinzani...hii kauli nimeinukuu na nitaifanyia kazi. Imenipa sababu nyingine ya kuwachukia magamba!
 
Huyu kachanganyikiwa!!!Kwanza anatakiwa achunguzwe kwa kujilimbikizia mali!!
 
Eti kadai mkichagua mpinzani Arumeru,miradi ya maendeleo itakwamishwa na wao kwa makusudi! Siasa gani hizo? Source itv.

Nami nimemsikia na kusikitika sana. Inapasa kutoa kodi kisiasa/kijimbo manake serikali tuliyonayo inapeleka maendeleo kwenye majimbo yaliyochini ya ccm!! Madness..
 
Ni ukweli usiyo fichika sasa CCM kazi kwisha, kama ata watendaji wa Serekali wanaongea wazi kwamba watakwamisha miradi ya maendeleo kama wapinzani wakichukua jimbo, ujue wamekosa sera za kuzungumza na wameamua liwalo liwe, but wajue kwamba wanatangaza vita ambayo ikianza wenyewe watakua wakwanza ku exit.
Uyu mama ajue nae tutaanza kumshushia mvua ya kashfa zake, Pls Mama Nagu tunakweshimu sana naomba tafadhali ukae kimya usije umbuka apa.
ukiwa ccm unaweza ukawa chizi na bado ukawa na hadhi ya 'Dokta'
 
Mary Nagu kafanya nini la maana jimboni kwake licha ya kuwa Waziri kwa miaka? Kashindwa hata kuwatetea wakulima wa vitunguu wanaonyanyaswa na wanunuzi toka Kenya. Wakenya hawa wanapanga bei wanayotaka na mkulima asipouza imekula kwao. Leo hii huyu mama anapata ujasiri wa kwenda kuengelea miradi ya maendeleo Maru?
 
Kweli serikali yetu
ina laana
kila waziri wa jk
anaongea pumba.
Alianza mkapa kwa
kutukana akafata
wasira na sasa nagu
hujaweka wabunge
wao kazi yao kuongea
urojo 2. Mmesha
laaniwa na bado.
 
Kweli serikali yetu
ina laana
kila waziri wa jk
anaongea pumba.
Alianza mkapa kwa
kutukana akafata
wasira na sasa nagu
hujaweka wabunge
wao kazi yao kuongea
urojo 2. Mmesha
laaniwa na bado.
Mkuu ccm ndio tatizo la nchi hii!!
Get rid of these crooks as fast as possible!!
 
Alilaaniwa toka alipowazuia watu wasiwaombee wenye ukimwi kwa jina la Yesu. Eti kufanya hivyo kutasababisha kasi ya maambukizi. Hivi huyu mama anavyosema watachelewesha miradi ya maendeleo hajui kwamba hizo pesa za maendeleo ni kodi za wanye vyama na wasio na vyama? Wapinzani na wasio wapinzani?

Basi sasa anatoa fursa ya wapinzani kukosa imani na serikali na kitendo cha watendaji wake kinahalalisha wapinzani kuwaeleza wafuasi wao kwamba wana haki ya kutokulipa kodi. Wapinzani tuelezeni haraka kama bado serikali hii ina uhalali wa kukusanya kodi zetu au la.
 
Siamini kua katamka hivo wazi kabisa kweny TV... Labda kama ana Kichaa....
 
Hii kauli ni nzito, ni mtu mwenye kuchanganyikiwa tu ndo anaweza kutamka hadharani kauli kama hii. Watu wa aina hii ni hatari na wasipokemewa inaweza kuleta machafuko. Kama kweli jimbo hili likachukuliwa na chadema na haya aliyoyasema wakamua kuyafanya na wananchi wakaamua kuipiga stop serikali kukanyaga jimboni humo kufanya chochote mambo yatakaaje?

Nadhnai huyu mama amelewa madaraka na hajui kama watu wanajua kuwa serikali ni ya wananchi na kwa ajili ya kutimiza yale wananchi wanayotaka na si kama viongizi wanavyotaka.

Huyu mama anadhani nchi hii bado iko mwaka 47 ambako wananchi hawatambui haki yao na kuwatetemekea viongozi.

Huyu mama anasahau kuwa cheo ni dhamana tu leo yeye kesho siyo yeye na Watu watamkumbusha maneno haya Yakujivuana kuwa yeye ndiyo serikali na ameshikilia maisha ya watanzania wote. Huyu mama nilikuwa namheshimu na mama mkwe wa rafiki yangu lakini amenichefua sana kwa kauli hii.

Natamani wana Arumeru wangekuwa na uelwa wa nini wajiu wa serikali kwa watu wake wangemjibu palepale kuwa hunaubavu wa kufanya unayosema maana sisi wananchi ndiyo maboss wako.
Angeona aibu na kushuka jukwaani. Hawa watu wanawadharau sana wananchi na wanadhani hawajui kati yao na serikali nani boss wa mwingine.

Chadema wasaidie kulitolea ufafanuzi swala hili haraka iwezekanavyo ili kumwaibisha huyu mama akimbie Arumeru. Nakama ndivyo seerikali inafikiria kuwaadhibu Arumeru kwa kuchagua chadema basi na wameru waipige stop serikali kukusanya kodi pale wajifanyie wenyewe mambo yao na mbunge wao.
 
Kwa nilichokiona ccm wamebaki na majirani na ndugu kutoka majumbani mwao katika mikutano yao ama kweli Arumeru wameamua kuisulubu kiukweli,nafikiri hawana zaidi ya siku2 wote watakuwa wamerudi dar kuipisha CDM imalize kazi,kwa umati niliouona kwa CDM na makumi niliyoyaona kwa magamba naamini wenye macho hamhitaji kuwa na miwani tena
 
Wivu tuuu unawasumbua mwaacheni mama yetu!!
Wewe ni she/he kama ni she nakusamehe kwani yawezekana ni wakati wako kwenda kwenye apolo kama ni he basi unaiga USB port kwa kupenda kuingiziwa device.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom