Kwa hili Waziri Mwakyembe ulipotoka

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Nakumbuka uliposimama na kuishawishi serikali Kuongeza ushuru wa mafuta ya taa kwamba ndo solution ya tatizo la uchakachuaji,niwazi hukufikiri sana ushauri wako kwani Kama ungefanya utafiti kidogo ungegundua athari za ushauri wako huo usio wa kisomi kwa watanzania wa maisha ya chini wengi wao wakiwa pale kyela, mbinga, likuyufusi, turiani, na sehemu Nyingine nyingi.Leo watanzania wanaponunua nusu lita ya mafuta ya taa kwa Tsh 1000. lazima tukukumbuke na tuzidi kuwalaani wanamagamba wote.Wote tunajua uchakachuaji na athari zake, lakini wanaofanya hivyo ni wahuni wachache ambao kama mngekuwa na dhamira ya kweli, mngeweza kuwadhibiti, Tatizo wachakachuaji ni miongoni mwenu wanamagamba,kwani nyie ndo wamiliki wa gas stations.
 
Alipotoka siyo kwa hilo tu bali kawaida yake kuongea upupu pasipo kufanya utafiti.Anafanya hivyo kwa vile ugumu wa maisha tunayoishi yeye haumuhusu.Tangu lini mwenyeshibe atamukumbuka mwenye njaa?
 
Alipotoka siyo kwa hilo tu bali kawaida yake kuongea upupu pasipo kufanya utafiti.Anafanya hivyo kwa vile ugumu wa maisha tunayoishi yeye haumuhusu.Tangu lini mwenyeshibe atamukumbuka mwenye njaa?
Mimi huwa simuelewi huyu mtu, majungu na sifa ndivyo vilivyomjaa. Natamani 2015 ifike mapema tena nashukuru wapiga kura washashtukia usanii wake.
 
Mwakyembe na wenzake ndio wamechangia sana kusababisha nchi kuwa gizani na porojo zao
 
Mwakyembe alilidanganya Bunge sakata la umeme kwa kuwa alikuwa na manufaa binafsi ambayo (haku declare) wakati anawasilisha uchunguzi wake uliopelekea Lowasa kujiuzulu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom