Kwa hili Tanesco wanatupeleka kwenye ulimwengu wa Kidigitali au wa kianalogia???????!!!!!!!!!

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Kwa miezi michache huku nyuma tulisikia mikakati ya Tanesco ni kufunga mita za luku kwa wateja wake kwa nchi nzima.Ili kuondoa wimbi la wadaiwa sugu wa shirika hilo hasa sekta za serikali na viwanda vikubwa. Lakini cha kushangaza na kusikitisha sasa hivi naona wameanza tena kuturudisha kule tulikotoka wanafunga tena yale mamita yao ya kuzunguka ya zamani. Kwa nionavyo mimi hivi shirika linawatendaji wenye akili timamu au ni mambumbmbu ndo wanaliendesha shirika hili Inasikitisha sana umesoma hadi chuo kikuu na umeanza kula matunda mazuri ya elimu yako tena unarudi kutamani kurudi kuanza kusoma chekechea.
 
Kuna nchi inaitwa Tanzania, huko mambo haya wala si ya ajabu.

Nadhani utakuwa ni mgeni, ukiendelea kuwepo hapo utazoea na utagundua wala siyo kitu kikubwa kama unavyodhani.

Watakabahu
 
Mkuu hivi ahadi zinazotolewa kwenye nchi hii unaziamini?
 
Back
Top Bottom