Kwa hili sikubaliani na Kikwete kuhusu mchakato wa Katiba Mpya

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Ndugu wana JF,Wazalendo wa nchi hii na wote wanaoipenda Tanzania,kwanza nianze kwa kuishukru Jamii Forums kwa kuanzisha ukumbi huu ambao unatuwezesha hata walala hoi ambao hatuwezi kuingia Bungeni au kwenye Baraza la Mawaziri kuweza kutoa maoni yetu.

Kwa leo napenda nigusie kidogo kuhusu Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa juzi wakti akiongea na Wazee wa Darisalama na hasa akiwalenga Watanzania wote kuwafikishia ujumbe wake kuhusu Mchakato wa Muswada wa Katiba Mpya. Katika hotuba yake hiyo iliyodumu kwa masaa 2 Mhe. Kiwete alitetea kwa nguvu zote kuhusu mchakato huo na kupinga hoja zote za wapinzani wakiongozwa na CHADEMA pamoja NCCR-Mageuzi. Kuna watu na hasa wafuasi wa CCM huwa wanapenda kumwagia sifa Kiwete kuwa ni Rais msikivu, lakini katika hili la Katiba mpya inaonekana Mhe. Kiwete si msikivu na ni Rais anayetumia ubabe na udikteta wa hali ya juu.

Katika hotuba hiyo alijitetea kuwa yeye ndiye Rais aliyeko madarakani kwa sasa kwa hiyo kwanamna yoyote ile hawezi kutengwa katika mchakato huu wa kuipatia Tanzania Katiba mpya baada ya miaka 50. Kwamba hata Marais waliomtangulia akiwemo Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere,Ali Hassani Mwinyi na Mkapa. Kwamba katika mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika mwaka 1964,mwaka 1977 na mwaka 1992 Marais wa awamu zote hizo walihusika moja kwa moja katika kusimamia mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.

Napenda nimkumbushe Mhe. Jakaya kwamba mabadiliko yote anayozungumzia yalifanyika katika mazingira ya Mfumo wa Chama Kimoja enzi za TANU kwa Tanganyika na ASP kwa Visiwani. Mwaka 1977 ikaundwa CCM huku ikiendelea kushika hatamu(utamu) na mpaka 1992 wakti wa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bado CCM ilikuwa ndiyo chama chenye maamuzi ya mwisho kwa maana ya Mwenyekiti wake ambaye huyohuyo ndiye Mkuu wa Nchi.

Napenda pia nimkumbushe Mhe. Jakaya kwamba katika Mchakato wa Tanzania ama kuwa na Vyama vingi au kuendelea na mfumo wa Chama kimoja Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere aliweza kuonyesha kipaji chake cha uongozi alichopewa na Mungu kwa KUAMUA KWAMBA PAMOJA NA KURA ZA MAONI YA WATANZANIA WENGI KUTAKA KUENDELEA NA MFUMO WA CHAMA KIMOJA,MWALIMU ALISEMA LAZIMA TANZANIA IFUATE MFUMO WA VYAMA VINGI. Kwa hiyo wale Watanzania wachache waliotaka mfumo wa vyama vingi ndiyo waliosikilizwa na kupewa nafasi ya Kwanza.

Napenda pia nimkumbushe Mhe.Jakaya kuwa WAZO LA KUWA NA KATIBA MPYA LILIANZISHWA NA WAPINZANI YAANI CHAMA CHA CHADEMA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA 2010 KUONEKANA YALICHAKACHULIWA NA KUMWEZESHA YEYE KIWETE KUBAKIA IKULU WAKTI UHALISIA ULIKUWA UNAONYESHA ALISHINDWA VIBAYA AU ALISHINDWA KWA KURA CHACHE MNO. HILI WATU WA UWT WANALIJUA NA KIWETE ANALIJUA HILO. Sasa basi kama CHADEMA waliweza kupiga kelele za kupinga mfumo wa Katiba iliyopo ambayo ilimwezesha yeye Kiwete kuingia madarakani pasipo halali na wakadai Katiba mpya na yeye Kikwete baadaye akaliona hilo na KUAMUA KUANZA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA! Mhe. Kiwete lazima akumbuke kuwa swala la KATIBA MPYA halikuwepo kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010. Lazima akubali kuwa lilianzishwa na wapinzani wakiongozwa na CHADEMA. Je, inakuwaje leo Kikwete ANAKATAA KUWASIKILIZA CHADEMA AMBAO NDIYO WAANZILISHI WA KUDAI KATIBA MPYA? Kwanini ameshindwa kutumia busara kidogo tu kama hiyo aliyoitumia kukubaliana na CHADEMA kuanzisha mchakato wa Katiba mpya???

Napenda pia kumkumbusha Mhe. Jakaya kwamba si kweli kwamba Katiba hiii tuliyonayo ni NZURI SANA na iliundwa kwa mtindo huhuu anaotaka kuutumia yeye kwa sasa. Kama ni nzuri sana kwanini CHADEMA na Watanzania walio wengi wameikataa na kuanza madai ya Katiba mpya?Katiba tuliyo nayo SI NZURI HATA KIDOGO. Katiba tuliyo nayo IMEUNDWA KATIKA MAZINGIRA YA MFUMO WA CHAMA KIMOJA. Ndiyo maana ukiisoma kwa undani utakuta IMEJAA UDIKTETA WA CHAMA KIMOJA,CHAMA TAWALA CHA CCM TANGU UHURU. Kwamba kwa Katiba hii ndiyo maana yeye KIKWETE AMEPEWA MAMLAKA YA UFALME NA USULTANI KIASI KWAMBA YEYE ANAONEKANA YUKO JUU YA KATIBA NA SHERIA. Hiki ndicho Watanzania tulio wengi pamoja na CHADEMA tunakikataa kwa nguvu zote.

Kwa hiyo basi napenda nimwambie Mhe. Kiwete kwamba kwa mazingira tuliyonayo kwa sasa, ya VYAMA VINGI NA UFAHAMU MKUBWA WA WATANZANIA KUHUSU KATIBA NA NAMNA DEMOKRASIA INAVYOENDESHWA HAPA TANZANIA NA DUNIA NZIMA KWA UJUMLA kuna haja ya KUBADILISHA MCHAKATO WA NAMNA YA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA ITAKAYOENDESHA TANZANIA KWA MIAKA MINGINE 50 IJAYO. Kiwete lazima ajue kuwa Katiba wanayoitaka Watanzania si ya CCM,si ya CUF, si ya CHADEMA,si ya NCCR-Mageuzi wala ya chama chochote cha upinzani. Tunataka KATIBA MPYA NA BORA KWA AJILI YA WATANZANIA WOTE!

Mimi naamini kabisa kuwa maadamu Rais Kiwete ndiye MWENYE MAMLAKA YA KUTEUA KAMATI TEULE ITAKAYO ANDAA RASIMU YA KATIBA MPYA basi hataweza kutenda HAKI. Kiwete ni binadamu kama wanadamu wengine kwa hiyo hataweza kwenda kinyume na maslahi ya CHAMA CHAKE CHA CCM. LAZIMA KUNA MAHALI ATACHOMEKEA NA KUCHAKACHUA VIPENGELE FULANI FULANI KWENYE RASIMU HIYO KWA VILE YEYE NDIYO MWENYE CHAMA TAWALA NA RAIS WA NCHI HII. Pale atakapoona kuwa kuna vipengele vina hatarisha madaraka yake na Chama chake lazima atapindisha taratibu. Wale wote atakaowateua kushiriki kwenye mchakato huo wengi watakuwa NI WANA CCM,MASWAHIBA WAKE NA JAMAA ZAKE. Tunajua kabisa Kiwete amedhihirisha kuwa ni Rais aliye mwoga KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU KAMA TULIVYO MNUKUU ALIYEKUWA WAZIRI WAKE MKUU Mhe. EDWARD LOWASSA. Ni dhahiri kabisa kuwa Kiwete ame-prove kuwa ni Rais mwoga anayetaka kumfurahisha kila mtu kitu ambacho katika utawala hakikubaliki. Tuna mifano mingi ya kuthibitisha udhaifu wa Kiwete katika kuchukua maamuzi magumu kwa mfano: Swala la EPA, TAKUKURU, RICHMOND/DOWANS,MGOGORO NDANI YA CCM,KUDORORA KWA UCHUMI,SWALA LA USHOGA n.k. na n.k.

Napenda pia nimkumbushe Mhe. Kiwete kuwa kuna maoni yametolewa na watu muhimu na maarufu waliokuwa viongozi waandamizi wa Serikali na Chama chake cha CCM miaka ya nyuma lakini Kiwete ameyapuuza au kuyapotezea. Tumemsikia Salim Ahmed Salim,mtu ambaye ana heshima kubwa katika medani za uongozi wa kitaifa na kimataifa akisema kwamba: KWA HILI LA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NI LAZIMA CCM NA CHADEMA WAKAE PAMOJA. Tumemsikia pia Hassy Kitine Mkurugenzi wa Zamani wa Mashtaka enzi za Mwalimu naye akitoa maoni yanayofanana na ya SAS. Lakini Kiwete amejifanya hamnazo. Akakomaa na ubabe wake kuwa lazima mchakato uendelee baada ya kupitishwa na Bunge kwa shinikizo huku akidai hoja za Wapinzani hazina maana na zinawapotosha Watanzania! Kama CCM wamekubali kufunga NDOA na CUF na sasa wanatawala pamoja huko Visiwani, kuna la AJABU GANI CHADEMA wakikaa na CCM ili kupata mstakabali wa namna ya upatikanaji wa Katiba mpya???CCM wanaogopa nini kwa CDM!!

Bila shaka Mhe. Kiwete anajua analolifanya. Kwamba pengine Kiwete anajidanganya aidha kwa akili yake mwenyewe au kwa ushauri wa kijinga toka kwa wasaidizi wake kuwa CCM ndicho chenye wabunge wengi Bungeni na kwa hiyo basi HOJA YOYOTE ITAKAYO PELEKWA BUNGENI ILI IPITISHWE KWA KUPIGA KURA,LAZIMA CCM WATASHINDA MAANA WAO NI WENGI NDANI YA BUNGE. Lakini Mhe. Kiwete akumbuke kuwa WABUNGE 270 AU 300 SIYO SAWA NA WATANZANIA MILIONI 45 AMBAO NDIYO WENYE NCHI HII,NDIYO WENYE KATIBA,NDIYO WALIOWAPA WABUNGE WA CCM DHAMANA YA KWENDA BUNGENI INGAWA TUNAJUA SI WOTE MAANA KUNA WALIOINGIA BUNGENI KWA MLANGO WA NYUMA KWA MAANA YA KURA ZA WIZI,RUSHWA NA KUCHAKACHUA. Tunajua ni some very few MPs walioshinda kihalali. Sasa kama Kiwete hataki kukubaliana na CHADEMA,WANAHARAKATI,WATANZANIA WALIO WENGI na BAADHI YA MAONI YA WALIOKUWA VIONGOZI WENZAKE NDANI YA CHAMA NA SERIKALI BASI tuna conclude kuwa Mhe. Kiwete haitakii mema nchi hii kwa siku za usoni.

Nimalize kwa kusema kuwa HII NCHI SI YA CCM NA CUF peke yao. Hii nchi ni ya Watanzania wote wa Bara na Visiwani.Lazima kuheshimu maoni hata kama ni ya wachache. Mwalimu aliamua kuwapa haki wale waliotaka mfumo wa vyama vingi ingawa walikuwa wachache. Hii ni kwasababu Mwalimu alikuwa na kipawa cha Uongozi na alikuwa akiona mbali kwa kusoma ALAMA ZA NYAKATI. Inasikitisha Kiwete anashindwa kutumia busara kidogo za uongozi kwa kusoma alama za nyakati. HII NI HATARI SANA KWA MSTAKABALI WA TAIFA LETU TANZANIA. Namwomba Mhe. Kiwete akubali kukutana na CHADEMA pamoja na NCCR-Mageuzi ili kupata mwafaka wa namna mchakato wa upatikanaji wa KATIBA MPYA NA ILIYO BORA.Vinginevyo Mhe. Kiwete haitakii mema nchi yetu Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki Afrika.
 
chadmea imetoa tamo na nini cha kufanya usioteze mda na kikwete hana lolote yule mzee
 
Inasikitisha Kikwete anashindwa kutumia busara kidogo za uongozi kwa kusoma alama za nyakati. .
Madaraka aliyopewa katika sheria ya mchakato wa katiba yanalevya sana; ni makubwa mno kiasi kwamba haoni madhara yake:
Kifungu cha 5: Raisi ataanzisha hiyo tume
Kifungu cha 6(1): Raisi atawateua wajumbe wa hiyo tume
Pamoja na vigezo vya kuteua wajumbe wa tume kuwekwa, bado kifungu 6(3)(e) kinamruhusu huyo raisi kuweka vigezo atakavyoona inafaa! Ukisoma vyema kifungu hiki cha 6 ni wazi tume itakuwa ni ya rais; ni vyema ingeitwa the presidential commission of...
Kifungu cha 8 raisi ndiye ataiambia hiyo tume nini cha kufanya (hadidu za rejea). Hakuna wa kuhoji!
Kifungu cha 13 kinaanzisha secretariat ya tume, katika kifungu cha 13(2) raisi anamteua katibu.
Madaraka ya hatari ni kifungu cha 20:
20(1) raisi atateua bunge la katiba (constituent assembly), wajumbe wa bunge hili tunaowajua ni mawaziri wa masuala ya sheria na katiba wa Tanzania (mteule wa raisi) na yule wa Zanzibar na mwanasheria wa serikali ya Tanzania (mteule wa raisi) na yule wa Zanzibar-20(2). Wajumbe wengine wote watateuliwa na raisi kwa mujibu wa 20(3) -Hakuna wa kuhoji uteuzi wa mtu yeyote! Ina maana wajumbe wote wanateuliwa na raisi isipokua wale wawili kutoka zanzibar
Kifungu cha 27: kura ya maoni itaendeshwa na tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti wake huteuliwa na raisi!

Katika hali hii kwa nini mtu asilewe madaraka na kusema chochote! Kama mlikuwa hamjui kwa nini alisema hayo aliyosema kwenye mkutano basi tafakari hayo madaraka utapata jibu.
 
rais wetu mfalme wa magogoni,
jina lako ni kikwete,
utuache sisi wenye nchi tujiandikie katiba yetu kwa kuwa sissi ndio wenye nguvu na mamlaka na hayo uliyonayo kiduchu tulikupa sisi na tunaweza kuyachukua wakati wowote ule tupendao,
jitahidi kusoma alama za nyakati na daima ukumbuke kizazi hiki is not beepable hata kidogo na ukijaribu kubip tunakupigia,
tukipata katiba bora hata vitukuu vyako vitafaidi nchi yenye maziwa na asali. amina
 
Ndugu wana JF,Wazalendo wa nchi hii na wote wanaoipenda Tanzania,kwanza nianze kwa kuishukru Jamii Forums kwa kuanzisha ukumbi huu ambao unatuwezesha hata walala hoi ambao hatuwezi kuingia Bungeni au kwenye Baraza la Mawaziri kuweza kutoa maoni yetu.

Kwa leo napenda nigusie kidogo kuhusu Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa juzi wakti akiongea na Wazee wa Darisalama na hasa akiwalenga Watanzania wote kuwafikishia ujumbe wake kuhusu Mchakato wa Muswada wa Katiba Mpya. Katika hotuba yake hiyo iliyodumu kwa masaa 2 Mhe. Kiwete alitetea kwa nguvu zote kuhusu mchakato huo na kupinga hoja zote za wapinzani wakiongozwa na CHADEMA pamoja NCCR-Mageuzi. Kuna watu na hasa wafuasi wa CCM huwa wanapenda kumwagia sifa Kiwete kuwa ni Rais msikivu, lakini katika hili la Katiba mpya inaonekana Mhe. Kiwete si msikivu na ni Rais anayetumia ubabe na udikteta wa hali ya juu.

Katika hotuba hiyo alijitetea kuwa yeye ndiye Rais aliyeko madarakani kwa sasa kwa hiyo kwanamna yoyote ile hawezi kutengwa katika mchakato huu wa kuipatia Tanzania Katiba mpya baada ya miaka 50. Kwamba hata Marais waliomtangulia akiwemo Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere,Ali Hassani Mwinyi na Mkapa. Kwamba katika mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika mwaka 1964,mwaka 1977 na mwaka 1992 Marais wa awamu zote hizo walihusika moja kwa moja katika kusimamia mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.

Napenda nimkumbushe Mhe. Jakaya kwamba mabadiliko yote anayozungumzia yalifanyika katika mazingira ya Mfumo wa Chama Kimoja enzi za TANU kwa Tanganyika na ASP kwa Visiwani. Mwaka 1977 ikaundwa CCM huku ikiendelea kushika hatamu(utamu) na mpaka 1992 wakti wa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bado CCM ilikuwa ndiyo chama chenye maamuzi ya mwisho kwa maana ya Mwenyekiti wake ambaye huyohuyo ndiye Mkuu wa Nchi.

Napenda pia nimkumbushe Mhe. Jakaya kwamba katika Mchakato wa Tanzania ama kuwa na Vyama vingi au kuendelea na mfumo wa Chama kimoja Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere aliweza kuonyesha kipaji chake cha uongozi alichopewa na Mungu kwa KUAMUA KWAMBA PAMOJA NA KURA ZA MAONI YA WATANZANIA WENGI KUTAKA KUENDELEA NA MFUMO WA CHAMA KIMOJA,MWALIMU ALISEMA LAZIMA TANZANIA IFUATE MFUMO WA VYAMA VINGI. Kwa hiyo wale Watanzania wachache waliotaka mfumo wa vyama vingi ndiyo waliosikilizwa na kupewa nafasi ya Kwanza.

Napenda pia nimkumbushe Mhe.Jakaya kuwa WAZO LA KUWA NA KATIBA MPYA LILIANZISHWA NA WAPINZANI YAANI CHAMA CHA CHADEMA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA 2010 KUONEKANA YALICHAKACHULIWA NA KUMWEZESHA YEYE KIWETE KUBAKIA IKULU WAKTI UHALISIA ULIKUWA UNAONYESHA ALISHINDWA VIBAYA AU ALISHINDWA KWA KURA CHACHE MNO. HILI WATU WA UWT WANALIJUA NA KIWETE ANALIJUA HILO. Sasa basi kama CHADEMA waliweza kupiga kelele za kupinga mfumo wa Katiba iliyopo ambayo ilimwezesha yeye Kiwete kuingia madarakani pasipo halali na wakadai Katiba mpya na yeye Kikwete baadaye akaliona hilo na KUAMUA KUANZA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA! Mhe. Kiwete lazima akumbuke kuwa swala la KATIBA MPYA halikuwepo kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010. Lazima akubali kuwa lilianzishwa na wapinzani wakiongozwa na CHADEMA. Je, inakuwaje leo Kikwete ANAKATAA KUWASIKILIZA CHADEMA AMBAO NDIYO WAANZILISHI WA KUDAI KATIBA MPYA? Kwanini ameshindwa kutumia busara kidogo tu kama hiyo aliyoitumia kukubaliana na CHADEMA kuanzisha mchakato wa Katiba mpya???

Napenda pia kumkumbusha Mhe. Jakaya kwamba si kweli kwamba Katiba hiii tuliyonayo ni NZURI SANA na iliundwa kwa mtindo huhuu anaotaka kuutumia yeye kwa sasa. Kama ni nzuri sana kwanini CHADEMA na Watanzania walio wengi wameikataa na kuanza madai ya Katiba mpya?Katiba tuliyo nayo SI NZURI HATA KIDOGO. Katiba tuliyo nayo IMEUNDWA KATIKA MAZINGIRA YA MFUMO WA CHAMA KIMOJA. Ndiyo maana ukiisoma kwa undani utakuta IMEJAA UDIKTETA WA CHAMA KIMOJA,CHAMA TAWALA CHA CCM TANGU UHURU. Kwamba kwa Katiba hii ndiyo maana yeye KIKWETE AMEPEWA MAMLAKA YA UFALME NA USULTANI KIASI KWAMBA YEYE ANAONEKANA YUKO JUU YA KATIBA NA SHERIA. Hiki ndicho Watanzania tulio wengi pamoja na CHADEMA tunakikataa kwa nguvu zote.

Kwa hiyo basi napenda nimwambie Mhe. Kiwete kwamba kwa mazingira tuliyonayo kwa sasa, ya VYAMA VINGI NA UFAHAMU MKUBWA WA WATANZANIA KUHUSU KATIBA NA NAMNA DEMOKRASIA INAVYOENDESHWA HAPA TANZANIA NA DUNIA NZIMA KWA UJUMLA kuna haja ya KUBADILISHA MCHAKATO WA NAMNA YA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA ITAKAYOENDESHA TANZANIA KWA MIAKA MINGINE 50 IJAYO. Kiwete lazima ajue kuwa Katiba wanayoitaka Watanzania si ya CCM,si ya CUF, si ya CHADEMA,si ya NCCR-Mageuzi wala ya chama chochote cha upinzani. Tunataka KATIBA MPYA NA BORA KWA AJILI YA WATANZANIA WOTE!

Mimi naamini kabisa kuwa maadamu Rais Kiwete ndiye MWENYE MAMLAKA YA KUTEUA KAMATI TEULE ITAKAYO ANDAA RASIMU YA KATIBA MPYA basi hataweza kutenda HAKI. Kiwete ni binadamu kama wanadamu wengine kwa hiyo hataweza kwenda kinyume na maslahi ya CHAMA CHAKE CHA CCM. LAZIMA KUNA MAHALI ATACHOMEKEA NA KUCHAKACHUA VIPENGELE FULANI FULANI KWENYE RASIMU HIYO KWA VILE YEYE NDIYO MWENYE CHAMA TAWALA NA RAIS WA NCHI HII. Pale atakapoona kuwa kuna vipengele vina hatarisha madaraka yake na Chama chake lazima atapindisha taratibu. Wale wote atakaowateua kushiriki kwenye mchakato huo wengi watakuwa NI WANA CCM,MASWAHIBA WAKE NA JAMAA ZAKE. Tunajua kabisa Kiwete amedhihirisha kuwa ni Rais aliye mwoga KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU KAMA TULIVYO MNUKUU ALIYEKUWA WAZIRI WAKE MKUU Mhe. EDWARD LOWASSA. Ni dhahiri kabisa kuwa Kiwete ame-prove kuwa ni Rais mwoga anayetaka kumfurahisha kila mtu kitu ambacho katika utawala hakikubaliki. Tuna mifano mingi ya kuthibitisha udhaifu wa Kiwete katika kuchukua maamuzi magumu kwa mfano: Swala la EPA, TAKUKURU, RICHMOND/DOWANS,MGOGORO NDANI YA CCM,KUDORORA KWA UCHUMI,SWALA LA USHOGA n.k. na n.k.

Napenda pia nimkumbushe Mhe. Kiwete kuwa kuna maoni yametolewa na watu muhimu na maarufu waliokuwa viongozi waandamizi wa Serikali na Chama chake cha CCM miaka ya nyuma lakini Kiwete ameyapuuza au kuyapotezea. Tumemsikia Salim Ahmed Salim,mtu ambaye ana heshima kubwa katika medani za uongozi wa kitaifa na kimataifa akisema kwamba: KWA HILI LA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NI LAZIMA CCM NA CHADEMA WAKAE PAMOJA. Tumemsikia pia Hassy Kitine Mkurugenzi wa Zamani wa Mashtaka enzi za Mwalimu naye akitoa maoni yanayofanana na ya SAS. Lakini Kiwete amejifanya hamnazo. Akakomaa na ubabe wake kuwa lazima mchakato uendelee baada ya kupitishwa na Bunge kwa shinikizo huku akidai hoja za Wapinzani hazina maana na zinawapotosha Watanzania! Kama CCM wamekubali kufunga NDOA na CUF na sasa wanatawala pamoja huko Visiwani, kuna la AJABU GANI CHADEMA wakikaa na CCM ili kupata mstakabali wa namna ya upatikanaji wa Katiba mpya???CCM wanaogopa nini kwa CDM!!

Bila shaka Mhe. Kiwete anajua analolifanya. Kwamba pengine Kiwete anajidanganya aidha kwa akili yake mwenyewe au kwa ushauri wa kijinga toka kwa wasaidizi wake kuwa CCM ndicho chenye wabunge wengi Bungeni na kwa hiyo basi HOJA YOYOTE ITAKAYO PELEKWA BUNGENI ILI IPITISHWE KWA KUPIGA KURA,LAZIMA CCM WATASHINDA MAANA WAO NI WENGI NDANI YA BUNGE. Lakini Mhe. Kiwete akumbuke kuwa WABUNGE 270 AU 300 SIYO SAWA NA WATANZANIA MILIONI 45 AMBAO NDIYO WENYE NCHI HII,NDIYO WENYE KATIBA,NDIYO WALIOWAPA WABUNGE WA CCM DHAMANA YA KWENDA BUNGENI INGAWA TUNAJUA SI WOTE MAANA KUNA WALIOINGIA BUNGENI KWA MLANGO WA NYUMA KWA MAANA YA KURA ZA WIZI,RUSHWA NA KUCHAKACHUA. Tunajua ni some very few MPs walioshinda kihalali. Sasa kama Kiwete hataki kukubaliana na CHADEMA,WANAHARAKATI,WATANZANIA WALIO WENGI na BAADHI YA MAONI YA WALIOKUWA VIONGOZI WENZAKE NDANI YA CHAMA NA SERIKALI BASI tuna conclude kuwa Mhe. Kiwete haitakii mema nchi hii kwa siku za usoni.

Nimalize kwa kusema kuwa HII NCHI SI YA CCM NA CUF peke yao. Hii nchi ni ya Watanzania wote wa Bara na Visiwani.Lazima kuheshimu maoni hata kama ni ya wachache. Mwalimu aliamua kuwapa haki wale waliotaka mfumo wa vyama vingi ingawa walikuwa wachache. Hii ni kwasababu Mwalimu alikuwa na kipawa cha Uongozi na alikuwa akiona mbali kwa kusoma ALAMA ZA NYAKATI. Inasikitisha Kiwete anashindwa kutumia busara kidogo za uongozi kwa kusoma alama za nyakati. HII NI HATARI SANA KWA MSTAKABALI WA TAIFA LETU TANZANIA. Namwomba Mhe. Kiwete akubali kukutana na CHADEMA pamoja na NCCR-Mageuzi ili kupata mwafaka wa namna mchakato wa upatikanaji wa KATIBA MPYA NA ILIYO BORA.Vinginevyo Mhe. Kiwete haitakii mema nchi yetu Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki Afrika.
Mimi nawapongeza chadema kwa kazi nzuri wanayofanya kwani bila kuhoji baadhi ya Mambo tungekuwa bado gizani!!!
Kwa mtanzamo wangu najua hata wabunge wa CCM hawana imani na utendendaji wa Rais Kikwete na ndiyo maana wanataka kumuondoa katika nafasi ya Uenyekiti Taifa!!!

Naomba wananchi kokote mliko ondoeni uoga tuseme kweli!!!
Hapa sio madaraka makubwa aliyopewa Rais Kikwete lakini ni uadilifu wa JAKAYA MRISHO KIKWETE sio Mzuri kabisa!!

Je ,Kwenye sakata hili la katiba , angepewa madaraka hayo SLAA wananchi wangelalamika ???
Je , angepewa Mwakyembe ,au Mangufuli, au Shivji wananchi Wange lalamika??
Angalia mawazo ya SALIMU ,KITINE, WARIOBA je, Kunatatizo???

Angekuwa Nyerere Kuna tatizo ???

Hapa Kikwete kama kikwete anapaswa kujua kuwa Wananchi hawamtaki kutokea ndani ya CCM ,serikali hadi upinzani !!!

Hata hao CUF nao hawamtaki Kikwete angalia tayari ndani ya CUF kumetokea mpasuko wa Kutaka kumutoa SEIF issue kubwa ni Ndoa ya Mkeka!!!

Nataka Watanzani wote tujadili mambo ya maana kuwa , Kikwete hawezi kusimamia mchakato wa Katiba mpya bali atafutwe mtu mwingine!!!

Jambo hili linajulikana hata ndani ya CCM!!!

Hofu iliyopo ndani ya CCM ni Mchakato wa kumupata mgombea Urais Mwaka 2015, wanajua Kikwete hawezi kusimamia sasa kama hawezi kusimamia Mchakato wa Kumupata mgombea ndani ya CCM anaweza kusimamia mchakato wa Katiba mpya unao husisha vyama vyote???

Tafakari !!! uwe mkweli!!! Ogopa MUNGU!!!! Usijilimbikizie Mali!!! kumbuka kunasafari ya kwenda India!!!
 
jaman mimi nalia tu sina raha kwa sababu kikwete simpendi najua atatuangamiza
 
Jamani acheni kukoti habari lote hili mnatuumiza vidole tunaotumia simu. Tunasema hamsikii, anayefuatilia thread yake ataona tu maoni yako.
 
Back
Top Bottom