WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda, amehoji sababu ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kutokuwa na mchezaji kutoka Tanzania Visiwani.
Pinda alihoji hali hiyo jana bungeni akiunga mkono kauli ya Mbunge wa Dimani, Zanzibar, Hafidhi Ali Tahir, aliyelalamikia kitendo cha Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), chini ya Rais wake Leodegar Tenga, kuwa amekuwa ikiibagua Zanzibar katika mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Mimi naunga mkono kauli ya Tahir, kuna tatizo gani ukimchukua mchezaji mmoja kutoka Zanzibar na kuleta kwenye timu ya taifa, lazima tuhakikishe tunaimaliza Muungano kwa kuondoa malalamiko madogo madogo kama hayo, alisema Pinda.
Pinda alitoa kauli hiyo jana, akifanya majumuisho ya mjadala wa hoja bajeti ya ofisi yake, mjini Dodoma.
Juzi, Tahir ambaye amepata kuwa refa aliyevaa beji ya Fifa, alimshambulia Tenga kuwa ni mbabe na mbaguzi kwa kutoishirikisha Shirikisho la soka Zanziabr (ZFA) katika mambo ya kimataifa.
Alisema, ubabe wa Tenga umesababisha Zanzibar ishindwe kushiriki mashindano ya Copa CocaCola nchini Afrika Kusini na kutoingizwa katika timu ya soka ya taifa inayonolewa na Brazil Marcio Maximo.
Source: Tanzania Daima

Last edited: