Kwa hili naweza kuwashitaki Bodi ya Mikopo?

okonkwo jr

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
2,419
1,737
Wapendwa katika Bwana hamjambo?

Nawasilisha hoja yangu kwenu nikitafuta msaada,

Hawa Bodi ya Mikopo wamekuwa wakifanya makato kwenye mshahara wangu kwa muda mrefu sasa wakati sikuwahi kusoma kwa kutumia pesa zao.

Mwezi wa Agosti niliwatumia vyeti vyangu pamoja na barua ya mwajiri wangu ikiwataka waache mara moja kukata mshahara wangu lakini wamekaidi kwani mpaka sasa bado wanaendelea.

Nimetumia pesa nyingi sana kufuatilia jambo hili, kwani kutoka kituoni kwangu hadi mjini ni mbali, kwa jambo hili uchumi wangu umeyumba sana, hivyo kwayeyote mwenye ushauri namkaribisha, hata kama kuna wakili yeyote
naomba tuwasiliane.
 
Una hoja ya Msingi sana. Wale Bodi hawana data base wanachokifanya ni ku test zari, kwa Mtu ambae yupo mbali na Mjini hasa kwa mtu ishu wa Umma atashangaa Mshahara imepungua lakin hawezi kujua sababu bila ya kupata Salary slip wakat siku hizi Salaru slip ni bidhaa adimu sana kutokana na ukosefu wa karatasi za kudurufu.
Fungus kesi Wanyooke
 
Wataalamu wa masuala ya kisheria naomba msaada wenu tafadhali
 
Andika barua kwa mkurugenzi mkuu wa bodi ya Mikopo ya wanafuni wa elimu ya juu.Elezea tatizo lako na usisahau kuandika kua unaomba kurejeshewa fedha zako zote walizokukata kuanzia mwezi husika kama unaukumbuka utaje account namba yako na benki
Kwenye barua ambatanisha vitu vifuatavyo...
Nakala ya cheti cha form four
Nakala ya kuhitimu chuo kikuu kama unayo .
Copy ya kitambulisho cha kazi
Copy ya kadi yako ya benk
Then tuma viambatanidho hivyo kwa Posta ama kwa uhakika zaidi kea ems. Ila kama upo dar fika makao makuu ya bodi mkuu. Baada ya bodi kujiridhisha kua hujawahi kua mnufaika watarejesha pesa zako zote..Nimeshawahi kua na tatizo kama lako walinisaidia na nikarejeshewa fedha zangu so changamka
 
tafuta mtu pale akusaidie utamlipa bila hivo hata uende mahakama ya kimataifa hawkupi haawa jamaa utamaliza soli yako yakiatu bure
 
tafuta mtu pale akusaidie utamlipa bila hivo hata uende mahakama ya kimataifa hawkupi haawa jamaa utamaliza soli yako yakiatu bure
Acha kupromote rushwa amtafute mtu alipe wa nn hayo ni mazingira ya rushwa utengeneza mkuu ni bora hiyo hela ya kulipa mtu aitumie hiyo nauli aje
 
Andika barua kwa mkurugenzi mkuu wa bodi ya Mikopo ya wanafuni wa elimu ya juu.Elezea tatizo lako na usisahau kuandika kua unaomba kurejeshewa fedha zako zote walizokukata kuanzia mwezi husika kama unaukumbuka utaje account namba yako na benki
Kwenye barua ambatanisha vitu vifuatavyo...
Nakala ya cheti cha form four
Nakala ya kuhitimu chuo kikuu kama unayo .
Copy ya kitambulisho cha kazi
Copy ya kadi yako ya benk
Then tuma viambatanidho hivyo kwa Posta ama kwa uhakika zaidi kea ems. Ila kama upo dar fika makao makuu ya bodi mkuu. Baada ya bodi kujiridhisha kua hujawahi kua mnufaika watarejesha pesa zako zote..Nimeshawahi kua na tatizo kama lako walinisaidia na nikarejeshewa fedha zangu so changamka
Mkuu usemacho nishafanya.lakn bado tu
 
Back
Top Bottom