Elections 2010 Kwa hili mh.kikwete umewapiga watanzania changa la macho.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Leo, wakati anajibu maswali kutoka kwa wawakilishi wa vituo vya TV, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM rais JK, alisema kwamba sababu iliyomsukuma kuwanadi wagombea wa CCM wanaokabiwa na kesi za ufisadi huko mahakamani, kutokana na ukweli kwamba watu hao bado ni watuhumiwa tu, kwakuwa bado hawaja hukumiwa. Pamoja na kukubaliana na kauli yake hiyo, napenda nimkumbushe rais wangu Kikwete, ya kwamba watuhumiwa hao wako mahakamani, kwakuwa serikali anayeiongoza yeye, ilizifanyia uchunguzi tuhuma zinazowakabili watu hao na kuridhika pasipo shaka lolote kuwa wanayo hatia. Ilikuwa ni kutokana na sababu hiyo, ndipo uamuzi wa kuwafikisha mahakamani ukafikiwa. Ikiwa hivi sasa unautilia mashaka uamuzi huo wa serikali unayoiongaza, unataka umma wa watanzania ukueleweje! Wana JF nisaidie kwa hili. Napenda kuwasilisha.
 
Asante mkuu maana tutakuwa wajinga mpaka lini? Piga kura ondoa mtu. Kazi DPP kuzungusha mafile ya kesi nini kama hawana uhakika na kesi?
 
Labda pengine Kikwete amesahau kwamba ktk uongozi wa serikali kiongozi yeyote anayetuhumiwa na mashataka huwekwa nje ya Uongozi hata kama hukumu haijatolewa..na ndio maana Lowassa na viongozi wengine woote waliohujumu uchumi wetu walijiuzuru lakini hakufikishwa mahakamani kwa kulindwa na serikali yake. Ni swala jingine kabisa kufikishwa mahakamani na kuwaacha viongozi hao kuendelea kutafuta nafasi ya kuongoza kama kweli JK alikuwa na nia nzuri na chama chake.

Siku zote chama chochote kile cha kisiasa hujaribu juu chini kutokuwa na scandals za kisiasa kwani ndizo huviangusha vyama kutokana na tuhuma hivyo wananchi kutoviamini na kutowachagua. Kwa hiyo hukumu ya wananchi ktk kuchagua viongozi wao ni tofauti sana na sheria za mahakama kwani kiongozi mbaya sii lazima awe kisha hukumiwa na bahati yake ni kwamba hakuna kamati inayopitisha mawaziri laa sivyo angejikuta hana baraza la mawaziri.

Kwa maana nyingine huwezi mchagua mwendawazimu kugombea Ubunge kwa sababu tu majibu ya daktari hayajatoka.
Mwendawazi ni mwendawazimu.
 
Swali la mwisho aliliulizwa JK aliulizwa unawaasa nini watanzania . akajibu ..... kisha akasema uchaguzi huu mtu kuiba kura ni ngumu sana.
Kwa usemi huo maana yake CCM wamekuwa wakiiba kura na hata sasa wanaweza kuiba ila kwa ugumu
 
Leo, wakati anajibu maswali kutoka kwa wawakilishi wa vituo vya TV, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM rais JK, alisema kwamba sababu iliyomsukuma kuwanadi wagombea wa CCM wanaokabiwa na kesi za ufisadi huko mahakamani, kutokana na ukweli kwamba watu hao bado ni watuhumiwa tu.

Sitaki nitumie lugha isyofaa kujibu madudu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lkn anakoelekea huenda nikakosa subira na kuanza kumjibu ndivyo sivyo!

Kama aliwanadi akina Mramba kwa sababu ni watuhumiwa tu mbona walituambia wao wenyewe kuwa kamati kuu ya CCM haijamteua Mwakalebela ingawaje alishinda kura za maoni Iringa Mjini kwa sababu tu"katuhumiwa na kufikishwa mahakamani na TAKUKURU"kwa mashtaka ya rushwa?

Kama "kutuhumiwa"na"kufikishwa"mahakamani si lolote ktk teuzi za CCM iweje basi Mwakalebela walimuacha kwa sababu hizo hizo Iringa Mjini lkn wakaja kumpamba kweli kweli majukwaani akina Mramba?

JK ongea na washauri wako wa sheria kabla ya kuanza kuongea na media tafadhali!
 
Kwa majibu ya JK juu ya Ramba, Goda na Gonja!!!!!!!!!!! Mzee Sabodo take futher action!!!!!
Mwalimu Nyerere alisema: " mke wa Kaisari/ Farao kutuhumiwa tu.......... Kunatosha kumuondoa Ikulu ......"
 
Ustaarabu wa siasa wamtaka kiongozi kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii. Pindi mwenendo wake na mahusiano vikiwa vya aibu, sifa za uongozi hukoma. Siku zote mahakamani huenda kuondoa tu ubishi ila wewe unayeshtaki unafahamu kabisa kuwa mshtakiwa wako ni mhalifu. Katika ubishani wa kisheria bado mtuhumiwa awezashinda kesi mahakamani japo kwako aliyekukusea ukweli haubadiliki. Ataachwa huru na mahakama lakini haitabadili vile unavyomfahamu mkosa wako. Utaratibu wetu wa sheria unadai mleta mashtaka aithibitishie mahakama bila wasiwasi kuwa mshtakiwa kweli ni mkosaji. Hata binti aliyebakwa huweza kushindwa kuithibitishia mahakama kuwa mbakaji kafanya hivina vile na pia akidaiwa ushahidi au alete mashahidi akashindwa, kesi hutupiliwa mbali lakini bado haitafuta ubaya wa mbakaji mbele ya binti huyu. Leo Mkwere anampeleka mtuhumiwa mahakamani ili mahakama ikamsaidie kujua kama mtuhumiwa ni mhalifu au laa?! Kuna vituko na matuko na hili ni Tuko.
 
Back
Top Bottom