Kwa hili la TBA Mhe. Magufuli umekosea!

hakuna mkamilifu lakini serikali yetu ina madudu mengi japo kwa kiasi fulani magufuli anajitahidi
 
Ni kama wengi wanatilia shaka ukweli wa habari hii, mimi nilisimuliwa na mfanyakazi wa TBA siku ile ile Waziri alipofanya vioja hivyo katika ofisi za TBA. Yote hayo ni kweli kabisa, japo ni ngumu kuamini kama Magufuli ndo angeweza fanya hivo.

Hata hivyo nasikia kuna kigogo mmoja ambaye ndo anatafutwa sana na Magufuli hapo TBA naye huenda siku si nyingi akafurushwa. Sitetei usafi wa Kimweri na wengine, ila napingana na udhalilishaji wa Waziri hasa ikizingatiwa hakuna hata tuhuma moja aliyoiweka wazi achilia mbali kuwa na uthibitisho.
 
Kwa mtajii huu naona watu wa CAG watakuwa wameneemeka sana huenda kila wanapokwenda kufanya uchunguzi bahasha nene wanatoka nazo.
Ila yaonekana dhahiri hizi tuhuma zina ukweli ndani yake...
 
Nichangie kwa ujumla wake.
Mahali popote penye mafanikio lazima kuwe na nidhamu. Nidhamu haiji kama mvua bali inajengwa. Katika mambo ambayo Watanzania hawayakubali ni pamoja na ukweli kuwa nidhamu yetu hasa katika utendaji serikalini haipo. Mfumo tuliokuwa nao umekwisha na sasa tupo katika mfumo tofauti.Kwa mantiki hiyo tunadhani kuwa utawala bora na wa sheria ni kuendeleza mlolongo wa hadithi. Utawala bora na washeria ni pamoja na mtendaji kuufuata sio yeye kutendewa tu.

Tanzania inahitaji madikteta kusema ukweli. Kuna mambo yanayofanyika ambayo huwezi kuyazuia kwa utawala bora au washeria.
Utawala bora na wa sheria ndio unahalalisha maovu kama ya umeme na scandal zisizo na mwisho. Utawala bora na washeria Tanzania maana yake ni ' buy the time'. Hatuwezi kujikwamua kama hatutaanza na ka udikteta japo kidogo, nidhamu ikisharudi tuendelee na utawala bora.

Kwa Tanzania kiongozi mbaya ni yule anayezuia alawansi, marupu rupu na ufujaji mwingine. Huyu atakuwa na maadui na mengi yatasemwa kuhusu yeye. Ni nadra mazuri yake kuandikwa.

Magufuli ana udhaifu wake kama mwanadamu lakini hatuwezi kupima mapungufu yake bila kuweka katika mizani na mazuri kama ufuatiliaji wa karibu. Hii haina maana ni mwadilifu, la hasha! EL tunajua mambo yake ya 'uadilifu' lakini ni ukweli kuwa ni mfuatiliaji.
Kwa maana hiyo mapungufu ya magufuli yawekwe wazi bila hisia ili tuyapime.

Endapo kuna tuhuma dhidi yake basi zithibitishwe. Kama ana maghorofa uwepo uthibitisho kama ule wa PPF au NSSF. Tukianza kuamini tu atatokea mtu na kusema jengo la mafuta house ni mali ya Magufuli, sijui tuamini au. Sikatai tuhuma ila ni wajibu ziambatane na vielelezo.
Moja ya sifa kuu za JF ni tuhuma ima zenye vielelezo au zenye maelezo yasiyo na shaka. Sio tuhuma zinazotanguliwa na hukumu.

Mleta mada ameanza kwa kutoa hukumu kuwa ni 'dikteta', inaniwia vigumu kuendelea kuamini mengine kwasababu tayari ameshahukumu.
Huyu Ephraim alilalamikiwa sana kuwa ni mfujaji na shauri lake lilifika hadi Ikulu na sisi hapa tukanyooshea vidole Ikulu kuwa ilikuwa na namna, sasa wema wake umetokea wapi ghafla? na kwanini jambo lililokuwepo kabla ya magufuli na sisi kulishupalia kwa serikali magufuli abebeshwe lawama?

Tuelewe kuwa Magufuli alipopigwa 'stop' na Rais na Waziri mkuu tulilalamika kuwa hakutendewa haki. Kama kuna mapungufu ya utendaji wake ni lazima tuangalie kuwa ni yeye au anakwazwa?

Hao wote waliotajwa kutotendewa haki hatujui utendaji wao, je ni vema tukaunga mkono hoja bila kujua upande wa pili wa shilingi.
Na kwa vile mleta mada hana vithibitisho zaidi ya kauli, tutajiridhishaje kuwa hana mahusiano au masilahi na 'wasiotendewa haki'! au ni mmoja wa alionufaika na mfumo uliokuwepo kabla ya kusambaratishwa.

Kwanini tudhani Magufuli hana utawala bora na tushindwe kumhoji waziri mkuu aliyeshindwa kufuata utawala bora na kujua Kagoda ni ya nani.
Kwanini Magufuli na si DCI au PCCB wanaotupiana mpira wa wapi yalipo mafaili ya watuhumiwa?
Kwanini iwe kwake na si Rais aliyeshindwa kuwawajisha waliotakiwa kuadhibiwa kwa mujibu wa Bunge.
Kwanini hakuna utawala bora wa kumkamata Vithlani uwepo wa kukamata wezi wa kuku.

Ninachotaka kusema ni kuwa nchi yetu imeoza na si magufuli (kama ni kweli) na hakuna nidhamu, utawala bora au wa sheria. Pengine tunachokiona au kukisikia ni sehemu ya uozo mkubwa na hatuna sababu ya kutahamaki.

Utawala bora unatiririka kutoka juu hadi chini na si kutoka katikati kwenda chini. Je wakwetu unatirika hivyo? na kwanini hatupigi kelele.
 
Nimeshindwa kuhilight kila neno. Ila nilichogundua kuondoka kwa hao watu hata wewe kumekugusa. Huwenda hata wwe ulikuwa unafaidika na uwepo wa hao watu.

Uwakilishi wako umejaa majungu na fitina juu ya dk. Magufuli. Ninachojua mimi, magufuli ni mwiba kwa wezi na mafisadi.
Siku zote wezi na mafisadi huwa wanapenda kutumia maneno kama hakufauata sheria au utawala wa sheria pale wanaposhikwa pabaya.
Kwa mtu aliyewahi fanya kazi serikalini au anayefanya kazi serikalini, atakubaliana nami kwamba viongozi waandamizi huwa wanajichotea pesa kwa njia mbali mbali kama 10%, semina za kipumbavu, safari za kijinga, kufoji allowance mbali mbali.

Viongozi kama hawa wakishikwa pabaya, wanyewe au wapambe wao (wanaofaidika na uozo) wanajitokeza kuwatetea kwa njia mbali mbali hasa jamii forums(people's voice). Utasikia hakufuata sheria ,kawatoa wale viongozi lakini waliiletea taasisi miradi mingi( hata kama alikuwa mwizi),naye ni fisadi .

Tanzania ya leo kama dk. Magufuli ni fisadi tutamjua tu ila kama ni majungu. Ni sawa sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Kuna watu huwa wanasema dk. Magufuli aliuza nyumba za serikali, mimi huwa najiuliza , je ni waziri yupi aliyekuwa awamu ya tatu hakushiriki? Maamuzi mazito kama hayo, hufanywa na baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wa raisi. Ni sawa sawa na ishu ya richmond nk.

Binafsi namkubali magufuli ukilinganisha na wana magamba wengine ambao kazi yao ni kupiga kelele kwenye majukwaa kwamba ni wanafunzi wa mwalimu wakati ikija kama posho za wabunge zipunguzwe, utasikia jinsi wanavyo zitetea.

Dk. Magufuli ni mtu wa kuthubutu kufanya mambo ambayo wana magamba wengine hawawezi fanya hata kidogo. Kama binadamu ana mapungufu yake.
Kwa jinsi ulivyo present mada yako,nakushauri uanzishe bendi ya taarabu. Utakuwa mwimbaji bora sana tanzania

nawasilisha
 
whistle blower! Endelea kutupa detail hata km watu watakuwa wagumu kuamini lakini kuna ukweli ktk baadhi ya mambo uliyosema. Me sio mara ya kwanza kusikia hizo habari. Ya jairo yanafanyika hata kwa magufuli kila idara inatenga 20 ml kusaidia kupitisha budget so hakuna msafi ccm wote wezi tu.

Mkuu mengine yooote waseme lakini hili si kweli kwa magufuli. Hii kitu magufuli hataki hata kuisikia tangia zamani. Ni waziri pekee ambaye mimi nafahamu kuwa hataki kusiakia hii kitu ya kuchangia eti budget ipite!! Fanya utafiti wa kina
 
tatizo letu watanzania kiongozi akiwa anatoa matamko makali makali basi huyo huhesabiwa kama kiongozi mchapa kazi. Hebu niambie kwa sasa hivi kuna tofauti gani kiutendaji (impact kwa wananchi wa tz) wakati kawambwa ni waziri na sasa magufuli. Sijaona tofauti yoyote, foleni ni ile ile, barabara ya mandela haijaisha, barabara ya kilwa vile vile. Ila magufuli kisha ongea mengi(kupiga mkwara) bila matokeo yoyote.

Naunga mkono hoja ya dr. Kitila
kama huoni kasi ya ujenzi/umaliziaji wa mandela road utakuwa muongo
 
Tusaidie kutueleza ile style ya kimweri ya blowjob na mama luoga na jinsi alivyompaisha kimamlaka ndani ya tba,lete hizo nyeti hapa jamvini ili tukuone kuwa wewe ni mpenda maendeleo
 
Wabongo wamekaririshwa nchi hii fisadi ni EL na Chenge na RA,


Sio wabongo ila ni wale wabongo wavivu wa kufikiri wananaosoma magazeti na kugeuza ujumbe huo kama umetoka kwa Mungu bila kuuchambua. Richmond iliyomtoa EL hata kama service charge ya mitambo ingegeuzwa ndo hasara unaweza kucompare na ufedhuli wa kuuza nyumba zetu?

Mtu analipa 60m nyumba ya Masaki next day anapewa 5 bilion na kuingia kwenye development contract ya kiwanja kama share holder. Kwa msiomjua huyu jamaa ambao habari zake mzijuazo ni zile za kwenye magazeti na TV lazima mtapata taabu sana. Tunaomjua huyu jamaa mpenda sifa za wajinga wasiojua si ndo wanaopiga kura. Fuatilia hasara ya wale samaki.

Nasikia alilipa karibu sh. 600 milioni kwa mvuvi mmoja ili aestablish cost ya samaki, yule mvuvi hakuwa na utaalam wowote akapiga longolongo akavuta hela. Nasikia watendaji wizarani wakaomba wataalam wa hapahapa wakaandaa ripoti safi ya kitaalam ikapelekwa mahakamani. Nasikia gharama ya hao wabongo haikuzidi 10 mil. Msiomjua mtapata tabu tumjuao tunajua.

By the way hoja ya kuuza nyumba za serikali bado iko valid ni suala la wakati tu. Nasikia bei ya nyumba ilikuwa ilizingatia thamani ya majengo tu ambayo ni chakavu kwahiyo unadepreciate lakini thamani ya ardhi haikujukuishwa na ndo maana nyumba oysterbay iliuzwa mil 30. Kazi kweli kweli!
 
Tba ndio chanzo cha madudu ya uuzwaji wa nyumba za serikali na mkwamo wa ujenzi wa nyumba mpya, kimweri alishajitwalia u mungu mtu pale..., watumishi wa umma walishindwa kupata nyumba za serikali na kikwazo ni huyu jamaa.

Mimi nina taarifa makini kuwa alichukua mlungura kwa mheshimiwa mmoja na akashindwa kumpatia nyumba ya serikali ili aishi mpaka ananyofolewa tba, kibaya zaidi amekuwa mtu wa mapenzi zaidi kuliko ceo, alikuwa hafanyi lolote mbele ya mmama mmoja fedha na mama wa utumishi luoga.....hafai huyu bwana acha aende zake
 
mtoa mada
moja: Article yako umeiandika kwa jazba.
Mbili: Maelezo yako yamekaa kimajungu pia.
Tatu: Tba haijawahi kuwa na mafanikio kama unavyoinadi!! Haiyumkini hata humu jamvini kuna wachache saana wanaofahamu kazi za tba!!!
Kwa hayo matatu:- si huyo lyatuu wala hao unaowasema wameisogeza tba!! Kwa jinsi ninavyofahamu kazi za tba nathubutu kusema kuwa utendaji wa taasisi hiyo ni mzigo kwa walipa kodi wa nchi hii!!!



nimesoma article vizuri kama vile mwandishi uko karibu sana na waathirika lakini je ukweli ndio huo? Au msongo wa kukosa hadithi yako ni ya upande wa nyerere ngoja tusubiri ya upande wa sungura.
 
Naamini Magufuli yupo sahihi kwa alichokifanya. Nilisoma ktk MwanaHalisi Mwezi April mwaka huu habari yenye kichwa cha Habari NYUMBA YA jk YAZUA UTATA. ndani ya habari hii kulikuwa na barua alizoandika BW Kimweri ambazo zilikuwa na upungufu mkubwa wa kimaamuzi na mbaya zaidi zilikuwa zikitofautiana na zile zilizoandikwa toka Ardhi. hii ni kipimo tosha kuwa aidha jamaa alikuwa mwizi au alivaa viatu vikubwa kuliko mguu wake.

Big up Magufuli.
 
unaweza kufupisha mkuu? all in all Magufuli ni mtu makini sana
I dont think as you explained
anyway wakuu watasema
Magufuli hana umakini wowote. hata alipokuwa Wizara ya Mifugo alitaka kufanya uteuzi wa mkuu mmoja wa kitengo cha idara ya samaki bila ya kufuata utaratibu ukapita mvutano mkubwa kweli keli.
 
Nimeshindwa kuhilight kila neno. Ila nilichogundua kuondoka kwa hao watu hata wewe kumekugusa. Huwenda hata wwe ulikuwa unafaidika na uwepo wa hao watu.

Uwakilishi wako umejaa majungu na fitina juu ya dk. Magufuli. Ninachojua mimi, magufuli ni mwiba kwa wezi na mafisadi.
Siku zote wezi na mafisadi huwa wanapenda kutumia maneno kama hakufauata sheria au utawala wa sheria pale wanaposhikwa pabaya.
Kwa mtu aliyewahi fanya kazi serikalini au anayefanya kazi serikalini, atakubaliana nami kwamba viongozi waandamizi huwa wanajichotea pesa kwa njia mbali mbali kama 10%, semina za kipumbavu, safari za kijinga, kufoji allowance mbali mbali.

Viongozi kama hawa wakishikwa pabaya, wanyewe au wapambe wao (wanaofaidika na uozo) wanajitokeza kuwatetea kwa njia mbali mbali hasa jamii forums(people's voice). Utasikia hakufuata sheria ,kawatoa wale viongozi lakini waliiletea taasisi miradi mingi( hata kama alikuwa mwizi),naye ni fisadi .

Tanzania ya leo kama dk. Magufuli ni fisadi tutamjua tu ila kama ni majungu. Ni sawa sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Kuna watu huwa wanasema dk. Magufuli aliuza nyumba za serikali, mimi huwa najiuliza , je ni waziri yupi aliyekuwa awamu ya tatu hakushiriki? Maamuzi mazito kama hayo, hufanywa na baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wa raisi. Ni sawa sawa na ishu ya richmond nk.

Binafsi namkubali magufuli ukilinganisha na wana magamba wengine ambao kazi yao ni kupiga kelele kwenye majukwaa kwamba ni wanafunzi wa mwalimu wakati ikija kama posho za wabunge zipunguzwe, utasikia jinsi wanavyo zitetea.

Dk. Magufuli ni mtu wa kuthubutu kufanya mambo ambayo wana magamba wengine hawawezi fanya hata kidogo. Kama binadamu ana mapungufu yake.
Kwa jinsi ulivyo present mada yako,nakushauri uanzishe bendi ya taarabu. Utakuwa mwimbaji bora sana tanzania

nawasilisha
Magufuli mwenyewe mwizi tu, ndio maana aliweza kusimamia uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei poa na hivi sasa mawaziri wanalipiwa hoteli,
 
unaweza kufupisha mkuu? all in all Magufuli ni mtu makini sana
I dont think as you explained
anyway wakuu watasema

Magufuli hana umakini wowote! ni fisadi tu...................
Kashiriki kujiuzia nyumba za serikali.......na kujigawia nyumba za National Housing Boko......
Umakini uko wapi? sema anajua kukremu!
 
Inawezekana mhusika ametoa maneno ambayo yanaweza kuonekana kama chuki binafsi au hana uelewano vizuri na Mhe.Magufuli.. Lakin kabla sijasema pointi yanguniulize hivi ni kweli Magufuli anaaminika? je Magufuli ni msafi? au watu wengi ni washabiki wake kwa sababu ya kusoma vizuri takwimu bungeni kwa njia ya kukariri hili ndo linawafanya watanzania tumuone ni mtu safi? sikatai magufuli amejitahidi kwa kiasi chake na amefanya mambo mengi tu ambayo yanaonekana lakin nataka wadau wajue kuwa Magufuli si kama anavyoonekana machoni pa watu si msafi hata kidogo..na kuna mambo mengi yako nyuma ya pazia lakini magufuli si mtu ambaye anaweza kuaminiwa ila naweza kusema yuko smart kwa mambo yake anayoyafanya . Haonekani kama mmilikiwa wa kitu lakin anatumia jamaa zake na rafiki zake katika idara nyingi katika makampuni mbalimbali.
 
Back
Top Bottom