Kwa hili la NSSF na mifuko ya jamii serikali imechemsha

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Sipendi kuingia kwa undani ili nifahamu kama hazina aina pesa. Kitu ambacho naamini serikali kwa wafanya kazi ni tabaka la mwisho kwao. Napenda kuamini pia kura za wafanyakazi azina umuhimu kwa taifa.

Hili la Mifuko ya jamii ni pigo kubwa sana hasa kwa vijana wakosao fursa za kuwa wajasiriamali. Kuna baadhi ya vijana kuajiriwa ni swala la kujiwekezea mitaji ili wakichanganya na NSSF ambazo kimsingi ni pesa zao, upata fursa ya kujiajiri.

Sitopenda kufahamu kama ni chadema au vyama vyote vimeshiriki kwa pamoja kupitisha sheria hii na kufanya kusainiwa na Rais. Ila ni maumivu tupatayo vijana ambayo tunanyanyaswa na serikali pamoja na waajiri wetu. Wafanyakazi tutasulubika miaka nenda rudi. Sioni mikakati yeyote ya kumsaidia mfanyakazi wa Tanzania

Nawawakilisha watu wote waliopata maumivu ndani ya mioyo yao, nikiwa moja wapo.
Poleni sana.

Mungu ibariki Tanzania, ibariki Africa.
Ameeni
 
Hivi sababu ya uundwaji wa mifuko hii ni nini? mimi nilidhani ni mifuko ya akiba ambapo ifikapo kile kipindi mtu hana uwezo wa kufanya kazi kutokana na umri au kuumwa mtu hulipwa kiasi fulani cha pesa hadi mwisho wa uhai wake.
kama ni kweli, tatizo nini?? utalipwaje mafao hayo kabla [ingawa ni pesa zako] mimi ninadhani ni utaratibu mzuri kwani jeuri yetu sisi huishia uzeeni na kama huna kipato ndiyo basi. kama walivyotangaza kutakuwa na mikopo ya nyumba kwa wanachama tatizo ni nini? Hata ughaibuni sijasikia kijana mbichi akalipwa pesa za aina ya mifuko hiyo sembuse sisi?
 
Tatizo mishahara ya wafanyakazi wengi aiukutani, na sio kila mtu anapenda kuajiriwa. Alafu tambua kwamba interest yao ni ndogo sana. Mikopo kwa vijana kwa ajili ya ujasiria mali ni amna, dhamana tutapata wapi, ardhi atuna, nyumba atuna. Lingine kinga za ajira kwa wafanyakazi ni kama amna. Ukifukuzwa kazi leo, utaenya. Je kipindi kazi imeisha utafanya nini. Wewe uliye comment upo upande wa serikali, si vema kujitetea na kuwakandamiza wengi. Uzeeni kitu kani, maisha leo, siyo kesho.
 
ishu kubwa ambayo nimeiona ni tatizo.
  • Ulipwaji wake ni wa utata,iwapo mashirika uliyofanyia kazi yamekufa.
  • Inflation say for 20 yrs ,thamani ya hela yetu inashuka kila leo
  • Life expectancy ni 55 yrs,ni wangapi wanafika huko.
  • kwa nini iwe ni lazima kujiunga.
  • Kwa wanaoacha kazi kuwa wajasiriamali utasubiri mpaka ifike hiyo miaka
nimesikitika sana juu ya hili.
 
Hii ndio silaha ya kuiondoa CCM madarakani maana hadi leo haijajitambua kujua kuwa Private sector kwa sasa imekua sana. Private sector ndio wanufaika wakubwa na withdrawal benefits, wao wanafikiri nchi hii bado wafanyakazi ni wale wa Public wanaolipwa average la laki nne kwa mwezi na ambao hawana uwezo wa kujiajiri na huendelea na utumishi wa umma hadi walazimishwe kustaafu. Private sector hakuna mtu anayesubiri afikishe miaka 60 ndio aanze kutumia hela zake, anahitaji hela sasa ili awekeze na kuzalisha faida. Alama za nyakati hazisomeki CCM
 
Hivi hili swala wabunge linawahusu au ni sisi wafanyakazi tu? Au wenzetu ubunge ukiisha ruksa kuchukua pesa yao?
Tusije tukawa tunaonewa sisi akina yakhe tu!
 
Mimi nadhani CCM imefika mwisho wao wanataka tugome nchi nzima(sijui wabunge wa upinzani mnalijua hili nadhani hili ni zaidi ya katiba ya nchi kwa umuhimu wake mnyika,tindulisu na mboe mpo0).mimi naiomba serekali wasifananishe wafanyakazi wa sekta binafsi na wa serekali.hakuna mtu wa sekta binafsi anaweza kufanya kazi mpaka afike 55yrs kama wapo ni wachache my be 20% ya wafanyakazi wote,pili naomba serekali isifananishe PPF na NSSF wachangiaji wake ni tofauti kabisa.kama wamekula pesa zetu za NSSF watuambie kabisa iweje baada ya mkaguzi mkuu kusema NSSF inafilisika ndio wazuie sisi kuchukua pesa zetu?sekta binafsi tuna taabika sana (tunafukuzwa kazi ,tunanyanyasika,tunapunguzwa kazi kuvumilia hivi ni ngumu huwzi fika 55yrs) Naomba hii sherea iwe kwa wafanyakazi wa serekali tuu sio wa Binafsi
 
Hii ndio silaha ya kuiondoa CCM madarakani maana hadi leo haijajitambua kujua kuwa Private sector kwa sasa imekua sana. Private sector ndio wanufaika wakubwa na withdrawal benefits, wao wanafikiri nchi hii bado wafanyakazi ni wale wa Public wanaolipwa average la laki nne kwa mwezi na ambao hawana uwezo wa kujiajiri na huendelea na utumishi wa umma hadi walazimishwe kustaafu. Private sector hakuna mtu anayesubiri afikishe miaka 60 ndio aanze kutumia hela zake, anahitaji hela sasa ili awekeze na kuzalisha faida. Alama za nyakati hazisomeki CCM

very true mkuu..:israel:
 
CHADEMA pia wametuangusha kwa hili. Mbona sikuzisikia kelele za hata mbunge moja akilipinga hili, angalau ziwe kelele kama za mbwa ko ko, zingemwogopesha mwizi. Bali imepitishwa na wabunge wote

Shame on you CHADEMA!
 
hatuna uhakika kama hili limepita bungeni mkuu...hakika makamanda wetu hawawezi pitisha huu *****...kunauwezekano imepitishwa mlango wa nyuma....
 
Inabidi wabunge watetezi muangalie ili sula kwa kina kutokana na yafuatayo:
1.Kwa maisha yalivyo kwa siku hizi huo umri wa pension kuufikia ni majaliwa,wengi hawafikii huo umri.
2.Kazi za siku hizi hasa sekta binafsi hazina security,kufukuzana kila siku na serikali haiprotect wananchi wake,wawekezaji wana hire na ku fire wapendavyo,sasa kama umefanya miaka miwili na hawakulipi heti usubiri miaka 55 hiyo pension ya miaka 2 itakusaidia nini kama sio kudanganyana?
3.Mtu kazi inapoisha sehemu moja hakuna uhakika kama atapata kazi sehemu nyingine,hizo hela alizotunza kama NSSF ndizo umsaidia kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali ,matibabu,kulipa ada za watoto etc sasa kuzizuia hadi mtu uzeeke ina maana gani,kwanini mtu asipewe hela yake wakati bado ana nguvu achachalike na kukabiliana na maisha?
 
Mimi nadhani hata wanaokaa nakupeleka mswada kama huu wawe wnapimwa akili. kwani wezetu wanapewa wakizeeka kwa sababu wao wanaposho ya kutokuwa na ajira. Ambao sisi hatuna. pia kwetu hapa mtu alikuwa anapata hiyo hela yake anaanzisha biashara ambayo ndani yake alikuwa anauwezo wa kuajiri watu wengine hivyo anatoa ajira kwa watanzania. sasa unapitisha hiyo sheria ili watu wapeleke pesa hiyo uswizi wakapate ajira watu wengine kwa pesa yetu. na muda huo umewekwa wkati wakijua utakufa bila kuchukua chochote na hao watu watakula hela na taifa litaendelea kuwa la watu masikini. tukubaliane watu wote nchi hii tugome naninadhani hat raisi wa nchi hii haelewi kama kuna watu wamekaa kutengeneza miswaada ya kula pesa ya watu tu. kwa hili mimi sikubali. ama wabunge wote watoke na bunge livunjwe.
 
hatuna uhakika kama hili limepita bungeni mkuu...hakika makamanda wetu hawawezi pitisha huu *****...kunauwezekano imepitishwa mlango wa nyuma....

Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

Chadema pia wamo ndani ya hiki kipengele. Kama awajaipitisha, wajitokeze kwenye vyombo vya habari wakanushe. Au kama kuna uwezekano, wapeleke ojaa. Sipendi kuikumu CCM tu kwa hili.
 
Sipendi kuingia kwa undani ili nifahamu kama hazina aina pesa. Kitu ambacho naamini serikali kwa wafanya kazi ni tabaka la mwisho kwao. Napenda kuamini pia kura za wafanyakazi azina umuhimu kwa taifa.

Hili la Mifuko ya jamii ni pigo kubwa sana hasa kwa vijana wakosao fursa za kuwa wajasiriamali. Kuna baadhi ya vijana kuajiriwa ni swala la kujiwekezea mitaji ili wakichanganya na NSSF ambazo kimsingi ni pesa zao, upata fursa ya kujiajiri.

Sitopenda kufahamu kama ni chadema au vyama vyote vimeshiriki kwa pamoja kupitisha sheria hii na kufanya kusainiwa na Rais. Ila ni maumivu tupatayo vijana ambayo tunanyanyaswa na serikali pamoja na waajiri wetu. Wafanyakazi tutasulubika miaka nenda rudi. Sioni mikakati yeyote ya kumsaidia mfanyakazi wa Tanzania

Nawawakilisha watu wote waliopata maumivu ndani ya mioyo yao, nikiwa moja wapo.
Poleni sana.

Mungu ibariki Tanzania, ibariki Africa.
Ameeni

Haitawaathiri tuu wanaotaka kuachana na ajira na kujiajiri bali hata wale wanaohama utumishi wa sekta binafsi na kujiunga na sekta ya umma baada ya kupata uzoefu huku sekta binafsi. Hata hivyo kwa waajiri ni afueni kwani wimbi la waajiriwa kubadilisha mwajiri ili waweze kuchukua mafao yao lilikuwa na athari hasi kwa ufanisi wa kampuni
 
Wanachi Hima Hima, Bunge livunjwe. Awajui wanawawakilisha kina nani. Mafisadi wanachi
 
ishu kubwa ambayo nimeiona ni tatizo.
  • Ulipwaji wake ni wa utata,iwapo mashirika uliyofanyia kazi yamekufa.
  • Inflation say for 20 yrs ,thamani ya hela yetu inashuka kila leo
  • Life expectancy ni 55 yrs,ni wangapi wanafika huko.
  • kwa nini iwe ni lazima kujiunga.
  • Kwa wanaoacha kazi kuwa wajasiriamali utasubiri mpaka ifike hiyo miaka
nimesikitika sana juu ya hili.

Hapa umeeleza vizuri sana, take 5.

Serikali imeamua hivi kwa ajili ya uhitaji wa pesa uliopo Serikalini. Serikali inatumia pesa za mifuko ya jamii, hivyo kama zitakaa kwa muda mrefu ina maana serikali wataweza kuzitumia kwa mipango ya maendeleo ya muda mrefu zile pesa kabla ya wanachama kuzihitaji kwa mafao.

Hii ni janja ya serikali katika kutudhurumu pesa zetu; kwani mfano mimi nikianza kazi nina miaka 20, hadi kutimiza miaka 55 nitakuwa nimefanya kazi katika waajiri zaidi ya 10. Kwani wote tunajua ajira zetu za siku hizi katika makampuni binafsi mtu ukimaliza miaka 2, basi umedumu muda mrefu.

Sasa kwa mtiririko huu wa kuajiriwa na kuacha hadi nitimize miaka 55, hata yale makampuni niliyofanya kazi mengi yatakuwa yamefunga biashara.

Mimi binafsi nimeshafanya kazi katika makampuni mawili ya kigeni na kwa sasa hawapo tena Tanzania, Je, hapo kama ndio pesa yangu ya makato walikuwa hawapeleki NSSF, baada ya miaka 10 ijayo nitamdai nani????

Serikali inapaswa walifikirie hili, ikizingatiwa kuwa zile ni pesa zetu na siyo fadhira ya Serikali ya mwajiri.

Ile ni haki yetu, vinginevyo isiwe lazima kujiunga na hii mifuko kwani hakutakuwa na faida zaidi ya njama za kutudhurumu pesa zetu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hawa SSRA pamoja na Serikali wangefanya la maana kama wangelipitisha na sheria kuwa "Mfanyakazi akiajiriwa basi mwajiri wake haruhusiwi kumuachisha kazi hadi atimize umri wa kustaafu"

Hapo binafsi nigewaelewa.

lAKINI KWA hili MMMMMMHHH WIZI MTUUUUPU!!!!!![/B]

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
  • Thanks
Reactions: rom
halafu haya mambo mbona wamepeleka kimya kimya au walijua wananchi watakataaa, dah kwa hili haliwezekani.....nataka hela yangu.....yaani nisubiri miaka 55 haiwezekani. Maisha nitayaendeshaje, pesa hii ingenisaidia kujikwamua kimaisha japo ni ndogo au ingenipeleka shule niongeze elimu......................... wabunge na serikali kwa hili haiwezekani ....mnatuuumizaa
 
kinachoniuma mimi ni kukukatalia kuchukua haki yako pale unapoihitaji, mfano sitaki tena kufanya kazi nataka kufanya biashara zangu sasa nahitaji hela yangu niliyoihifadhi, eti sipewi hadi nizeeke. wapi jamani haki ya mfanyakaze kwa hela yake mwenyewe?
 
Back
Top Bottom