Kwa hili la Mtwara na Lindi, Je Chadema ni chama cha Kaskazini na Ukristo?

cc wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara tunawaomba msaada tunakwisha jamani....tumelala lakini nchi hii ni moja tupeni ushirikiano, tufungueni! elimu zetu duni jamani matatizo ya kila aina kuanzia uongozi..tuelimisheni...Mwenekiti Taifa na Vijana wako njooni huko tutawalinda, Peopleeeeeeeeeeeeeez Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!
 
Anzia hapo ulipo, fanya kuelimisha watu!! Lakini pia, unganisha nguvu na wenzako muweze kuwasaidia wasiotaka kubadilika kifikra.
 
CHADEMA bado tuna kazi kubwa sana ya kuhakisha tunapata majimbo kusini, naomba tusibweteke. Kwa mfano; Jimbo la uchaguzi Mtwara mjini.

Wakati timu ya M4C ilipopita hapa, mtazamo wa haraka haraka unaweza kusema mafanikio yalikuwa makubwa, lkn tatizo mojawapo litakalo iangusha CDM ni kukosa mtu atakaesimama kwa kofia ya CDM ambae atakuwa na mvuto wa ki-hoja ambaye ataweza kushindana na nguvu ya CCM ambayo inafanyiwa kazi sasa hivi ili kufanya maandalizi ya kumpa Mhe. Hawa Gasia jimbo hili ifikapo 2015.

Tatizo hili sio kwa Mtwara mjini tu, hiki ni kidonda ambacho CDM inatakiwa kukitafutia dawa kama inataka kupata matokeo mazuri 2015 kwa mikoa ya kusini, hasa Mtwara.
 
cc wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara tunawaomba msaada tunakwisha jamani....tumelala lakini nchi hii ni moja tupeni ushirikiano, tufungueni! elimu zetu duni jamani matatizo ya kila aina kuanzia uongozi..tuelimisheni...Mwenekiti Taifa na Vijana wako njooni huko tutawalinda, Peopleeeeeeeeeeeeeez Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!

wewe ndio umelala,wenzako wana akii na wameamka kwa kuchagua ccm
 
Hizo ni porojo za wafa maji.. Ila Cdm ina kazi kubwa huko,inahitaji kufanya sasa maandalizi ya kumpata mtu makin na ni vzr kumtambua ss ili aweze kujengwa mapema.
 
Back
Top Bottom