Kwa hili la Madereva, Zitto na Filikunjombe siwaungi mkono

Wewe una wananchi wangapi jimboni kwako wanaokupigia simu kila siku kutaka kutatuliwa matatizo yao? wewe una wasiliana na wizara na idara ngapi kwa siku kufatilia matatuzi ya wananchi wa jimbo lako? wewe una safari ngapi kwa mwaka kwenda majimboni kusikiliza wananchi wako?

Nyie ndi mnaona kuwa kuwapa madereva ni "luxury", haujui maana ya productivity, mawazo kama yako ndio yalikuwa ya Nyerere na matokeo katuwacha maskini wa mwisho duniani.

Productivity? what productivity? Let me tell ugonjwa unatumaliza Tanzania - ni kitu kinaitwa 'structural unemployment' meaning tuna wafanyakazi wengi kwa kazi chache hivyo muda mwingi watu hawana kitu cha kufanya. Dereva wa Viky Kamata anafanya nini? Dereva wa Lucinde, au Christine Magige wanafanya nini? ni lini tutajifunza 'kufanya kazi kwa bidii' na kuondokana na huu mkundikano wa 'wasaidizi?

Mbona tunaona wabunge wa nchi nyingine wakijiendesha? Au hawa watanzania wana upungufu fulani - maybe? Still, anayeona hawezi aandae utaratibu wake binafsi. Narudia Tanzania bado tuna kasumba mbaya sana, hapo bungeni wana wahudumu mpaka wa kuwawekea maji kwenye glass! Nenda kwenye maofisi, kuna msururu wa wahudumu utafikiri ni ofisi ya wafalme.
 
Infrastructure ya nchi zingine usiifananiishe na ya Tanzania, nje huko wengi wanamua kutumia Public Transport kwa sababu imefikia efficiency ya hali ya juu, kwetu ndio kwanza Kikwete katutoa kutoka nchi ya umaskini wa mwisho duniani na kutufikisha mpaka juu ya namba 20, bado tuna muda mrefu kabla hatujachukulia mifano ya wenzetu.

Una target majina ya wabunge kama vile unakuwa nao saa zote, nasema, madereva kwa wabunge ni muhimu sana kwa kwetu. Hujui maana ya "productivity".
 
Likija swala la mikopo tunajilinganisha na nchi zingine including Marekani na Japan, likija swala la kujiendesha wenyewe unataka tusijilinganishe! Ukiamua kuiga basi iga yote mema. Wakati mwinge inabidi uishi dhiki ndipo utapambana na tatizo. Kama wabunge wote wangelazimishwa kupanda treni kwenda Dodoma, ndani ya mwaka mmoja ungeona mapinduzi kwenye kwenye usafiri wa reli.

NB: Naelewa vizuri kabisa maana ya productivity, sihitahi lecture toka zomba. Thanks!
 
Infrastructure ya nchi zingine usiifananiishe na ya Tanzania, nje huko wengi wanamua kutumia Public Transport kwa sababu imefikia efficiency ya hali ya juu, kwetu ndio kwanza Kikwete katutoa kutoka nchi ya umaskini wa mwisho duniani na kutufikisha mpaka juu ya namba 20, bado tuna muda mrefu kabla hatujachukulia mifano ya wenzetu.

Una target majina ya wabunge kama vile unakuwa nao saa zote, nasema, madereva kwa wabunge ni muhimu sana kwa kwetu. Hujui maana ya "productivity".

Wewe Zomba acha kuchafua hali ya hewa mkuu.
 
Kwanza ni gazeti gani?

Pili hao madereva kwa sasa hivi wanalipwa na nani? Na je, hao wanaowalipa wanapata wapi pesa kwa kuwalipa hao madereva?
 
Wewe Zomba acha kuchafua hali ya hewa mkuu.

Huo ndio ukweli. Hata uwiano wa umri wa kuishi umepanda wakati wa Kikwete mpaka kufikia miaka 55, Nyerere alituacha na uwiano wa miaka 45, Mwinyi na Mkapa wakatufikisha 48, Kikwete kwa maiaka 7 tu katuandisha tuko kwenye miaka 55. Katutoa kwenye umaskini wa mwisho duniani aliotuacha nao Nyerere mpaka sasa tuko juu ya 20. Ni hatua kubwa sana kwa miaka yake saba tu, na huu mpango wake wa Malaria ukiendelea nadhani mpaka 2015 tutafika miaka 60. Maana chanzo kikubwa cha vifo ni Malaria.

Wacheni Wabunge wapewe madereva.
 
Mbona mimi sijafeel hiyo upward drift? Zomba isije kuwa tuko pale pale ila kunavijinchi vimemess up na kutupita kwa kwenda chini zaidi.

Naunga Mkono Wabunge kupewa Madereva na Malipo ya Madereva kuongezwa zaidi.
 
Aaaaah,,,walipwe na serikali?????ili iweje,,,,,wanatania haoooo,,,,HAWAPO SIRIAZ,NADHAN WANAENDELEZA SILLY SEASON
 
Imekuwa vigumu sana kwa Bunge kuwadhibiti hawa Waheshimiwa hasa kuhusu mapato. Hata matumizi ya Consistuency Development Fund yana utata kibao! Wabunge wanapewa fedha za malipo ya madereva (mishahara na posho) hata hivyo wengi hawawalipi madereva.

Kwahiyo nahisi Zitto na Filikunjobe (ambao kwa hakika ni wapiganaji wazuri bungeni) wana maana iliyofichika kwavile wanaijua hali halisi. Wanachomaanisha ni kuwepo mfumo wa namna ya kuwalipa madereva direct. Njia iliyopata kupendekezwa ni kwamba OFISI YA MBUNGE katika jimbo iwe ni taasisi yenye wafanyakazi ambao ni independent of the Parliamentarian kwavile hawa Waheshimiwa wanatumikia miaka mitano kisheria. Mfumo huu ungewezesha Bunge kuajiri dereva na mchumi kwa ajili ya ofisi ya Mbunge. Lakini utekelezaji wa hili umekuwa unasuasua. Kwa sababu uongozi wa Bunge umekuwa dhaifu basi hilo jukumu lihamishiwe kwenye mamlaka inayohusika na utumishi na katika bajeti ya Bunge lile fungu la mishahara ya watumishi wa ofisi ya BUNGE imegwe na kubaki Serikalini.

Huo ndio mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom