Kwa hili la Madereva, Zitto na Filikunjombe siwaungi mkono

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Gazeti moja leo limeripoti kwa urefu maoni ya wabunge hawa wawili machachari, wakitetea madereva wa wabunge walipwe na serikali.
Kwa maoni yangu siwaungi mkono hata kidogo. Ni wakati huu ambapo tunapigia serikali kelele kuwa ipunguze matumizi kwenye magari ya watendaji wake ikiwemo kuondolewa kwa madereva binafsi kwenye payroll ya serikali. Ni wakati huu ambapo napendekeza kuwa katika nchi hii, wawepo watu watano tu wenye madereva binafsi, yaani raisi na makamu wake, waziri mkuu, spika na jaji mkuu. Watendaji na viongozi wengine wote, wajiendeshe wenyewe au waajiri madereva wenyewe katika safari zao za kila siku, isipokuwa kwa safari za kikazi nje ya maeneo yao ya kazi ambapo watatumia madereva wa ofisi na gari za ofisi (maximum cruiser-mkonga).
Kwa hiyo wakati tayari tukiona kuwa mzigo wa mamia ya magari na madereva serikalini ni mkubwa, itakuwa ni ajabu kama tukiamua kujiongezea tena mzigo wa madereva 320 wa kulipwa na serikali!!!

Makamanda Zitto, na Deo nawakubali sana, but katika hili... no no no...
 
Zitto na Filikunjombe wamekurupuka au wanafanya kusudi tu! Serikali inashinikizwa kwa sasa kupunguza gharama za matumizi ktk uendeshaji, leo iweje hawa jamaa wanakurupuka kutaka madereva walipwe na serikali? Hawa jamaa wanajiona wao kuwa wabunge wana hijati kila aina ya upendeleo? Kwa kazi gani hasa wabunge wote wanafanya zaidi ya kupigana vijembe na mipasho ndani ya bunge
 
Kwa hiyo wakati tayari tukiona kuwa mzigo wa mamia ya magari na madereva serikalini ni mkubwa, itakuwa ni ajabu kama tukiamua kujiongezea tena mzigo wa madereva 320 wa kulipwa na serikali!!!

Makamanda Zitto, na Deo nawakubali sana, but katika hili... no no no...

Kuna kitu hujakielewa hapa. Hoja siyo kwamba hawa madereva walipwe au wasilipwe. Bunge linatoa fedha kwaajili ya madereva. Kila mbunge anapewa tshs. Laki 100,000/= kwa mwezi kama mshahara wa dereva na ths. 300,000/= kama posho ya dereva. Pesa hii ya dereva anapewa kila mbunge ili amlipe kwa derevva wake.

Kinachofanyika wabunge wanaziminya zike pesa na hazifiki kwa madereva. Tatizo ndo linaanzia hapo. Kakam bunge linatoa pesa, kwaaji ya madereva ni haki yao madereva kupewa pesa zao.
 
Kitu muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa madereva hawa wanalipwa stahili zao na wabunge. Hili ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa raia wake hawanyonywi!
 
Hili la madereva nawaunga mkono, badala ya watu muhimu kukaa wakaendesha wenyewe, ule muda wataoutumia wakiwa ndani ya gari kwa mawasiliano na shughuli zingine ni muhimu sana kuliko mishahara ya madereva.

Walipiwe madereva, unless kama mnataka kuona yaliompata yule Mbunge wa chadema.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi hususan vijana hawa, wameyajulia magari baada ya kuingia bungeni, kama mnapenda usalama wao muweke sheria kabisa kuwa hawaruhusiwi kuendesha wenyewe na wapeni madereva.
 
kazi rahisi toa posho za wabunge ili kufidia ajira ya madereva

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Kuna kitu hujakielewa hapa. Hoja siyo kwamba hawa madereva walipwe au wasilipwe. Bunge linatoa fedha kwaajili ya madereva. Kila mbunge anapewa tshs. Laki 100,000/= kwa mwezi kama mshahara wa dereva na ths. 300,000/= kama posho ya dereva. Pesa hii ya dereva anapewa kila mbunge ili amlipe kwa derevva wake.

Kinachofanyika wabunge wanaziminya zike pesa na hazifiki kwa madereva. Tatizo ndo linaanzia hapo. Kakam bunge linatoa pesa, kwaaji ya madereva ni haki yao madereva kupewa pesa zao.

Laki 1??? Huo ni mshahara kima gani? Ngapi atapewa dereva, ngapi zitanda PAYE, ngapi pension nk??? Sasa hapo ndipo tatizo linapoanzia. Mbunge makini hawezi na hathubutu kuajiri dereva mwenye thamani ya laki 1, + laki 3 posho.
Msimamo wangu, and I stand for this ni kuwa hata hizo laki nne ziondolewe. Wabunge wajiendeshe wenyewe na kama hawawezi, waajiri madereva kwa hela yao. Majority ya hawa wabunge walikuwa wanajiendesha wenyewe kabla ya kuwa wabunge na watajiendesha wenyewe baada ya ubunge wao kuisha..
 
Dawa hapa ni wabunge kupewa magari tu na wala si posho wala mshahara wa hao madereva....atakayehitaji dereva amuajiri kwa hela yake otherwise ajifunze kuendesha gari kwani halina ugumu wowote ni umwinyi tu unawasumbua
 
Penye red, sio ukweli unless uje na data za kitafiti kuwa 'watu muhimu' wanakuwa na shughuli zenye tija zaidi wakiwa kwenye magari zaidi ya mishahara ya madereva.
Penye blue, sio kweli maana tulishawahi kushudia viongozi wengi wakihusika katika ajali japokuwa walikuwa wanaendeshwa na madereva waliofuzu
Penye dark red, sio kwenye kuwa wabunge 'wengi' wamayajulia magari baada ya kuingia bungeni..
 
Ndio maana unaona kila siku bajeti ni matrilioni lakini maendeleo hakuna..kumbe mijihela inapotoea kijinga jinga namna hii....ngoja niwe rais wenu...hakuna cha posho wala nini..kama hutaki kazi serikalini badili uraia....hamia nchi nyingine kabisa ambayo inaendekeza ukondoo
 
Kwani wakiendesha hao madereva ndio hawawezi kupata Ajali hebu ondoa ushabiki wako wa Kizombi hapa

Dereva kazi yake ni udereva. Mbunge ana mawasiliano mengi ya kufanya, mifano tumeona kwa wabunge wawili waliopata ajali, mmoja amepoteza maisha (alikuwa anaendesha mwenyewe na hajui gari vizuri), mwingine alipakia wazee wake (kuwaringishia shangingi jipya) na matokeo tunayajuwa. Hawa ni watunga sheria, na udereva wapi na wapi? saa ngapi waongee na simu? saa ngapi waendeshe?
 
Penye red, sio ukweli unless uje na data za kitafiti kuwa 'watu muhimu' wanakuwa na shughuli zenye tija zaidi wakiwa kwenye magari zaidi ya mishahara ya madereva.
Penye blue, sio kweli maana tulishawahi kushudia viongozi wengi wakihusika katika ajali japokuwa walikuwa wanaendeshwa na madereva waliofuzu
Penye dark red, sio kwenye kuwa wabunge 'wengi' wamayajulia magari baada ya kuingia bungeni..

Haihitaji utafiti, tunajuwa wanasafiri safari ndefu na fupi muda wote na inabidi wawasiliane na wananchi na shughuli zingine kwenye vi Ipad, sasa fikiria usalama wao hapo. Isitoshe, Mbunge mmoja analipwa fedha nyingi sana, na kutwa moja ukimuacha aendeshe kwa masaa average ya masaa 4 kwa mwaka, ni fedha ngapi hapo umemlipa kwa kuendesha tu? kwani akiendesha ujuwe hata mawasiliano amekata.

Madereva ni muhimu sana kwa hawa waunga sheria, hiyo tukipenda tusipende.

Lets think of productivity and safety for a while.
 
sio hoja dhaifu bali posho/mshahara wa dereva unalipwa na serikali kupitia kwa mbunge ,nadhani wazo litakuwa na mashiko kama huo mshahara utaenda moja kwa moja kwa dereva na sio kupitia kwa mbunge.
 
Dereva kazi yake ni udereva. Mbunge ana mawasiliano mengi ya kufanya, mifano tumeona kwa wabunge wawili waliopata ajali, mmoja amepoteza maisha (alikuwa anaendesha mwenyewe na hajui gari vizuri), mwingine alipakia wazee wake (kuwaringishia shangingi jipya) na matokeo tunayajuwa. Hawa ni watunga sheria, na udereva wapi na wapi? saa ngapi waongee na simu? saa ngapi waendeshe?

zomba, wabunge ni binadamu kama walivyo watu wengine. Na si kweli kwamba wabunge wana mambo mengi kutushinda sisi tunaofanya kazi na kujiendesha wenyewe. Tuachane na tabia za kitumwa, anayetaka dereva amwajiri yeye mwenyewe na siyo haya mambo ya kusema kuwa wabunge wana mambo mengi? Hivi Vicky Kamata na Lucinde wana mambo gani?
 
Wewe una wananchi wangapi jimboni kwako wanaokupigia simu kila siku kutaka kutatuliwa matatizo yao? wewe una wasiliana na wizara na idara ngapi kwa siku kufatilia matatuzi ya wananchi wa jimbo lako? wewe una safari ngapi kwa mwaka kwenda majimboni kusikiliza wananchi wako?

Nyie ndi mnaona kuwa kuwapa madereva ni "luxury", haujui maana ya productivity, mawazo kama yako ndio yalikuwa ya Nyerere na matokeo katuwacha maskini wa mwisho duniani.
 
Charity begins at home.
Mtu unateteaje hoja za kupinga ufisadi wakati hata dereva wako unamnyonga!
Hili suala ndio linaonyesha unafiki wa wabunge wengine kudhani good governance iko serikalini tu, na haiko kwa mtu mmoja mmoja.
Mbunge anaye pewa fungu la kumlipa dereva wake, naye hafanyi hivyo, basi huyo ni fisadi tu na hafai kupewa madaraka yoyote nchini.
 
Hilo ni suala lingine kabisa.
 
Back
Top Bottom