Kwa hili la hujuma kwa gaziti la mwananchi ni umafya.

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
Mwananchi lahujumiwa Dodoma
GAZETI la Mwananchi linalochapwa na Kampuniya Mwananchi Communications Ltd (MCL), juzililigeuka bidhaa adimu mjini Dodoma baada ya
watu wasiojulikana, kulihujumu na kununua nakala zote.

Haijafahamika hasa sababu za mtu au watu hao kukusanya nakala zote za gazeti hilo na
kuziondoa katika mzunguko, lakini taarifa zinadai lilikuwa na habari ambazo zilikuwa
zikitishia masilahi yao.

Katika ukurasa wa kwanza kulikuwapo na habari
tatu kubwa; moja ikihusu kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliomalizika juzi
usiku.

Licha ya habari hiyo, kulikuwapo na habari iliyomhusu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kuhusishwa na kashfa ya uuzaji wa kiwanja kimoja kilichopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.

Habari hizo mbili ndizo ambazo zinahisiwa zilisababisha watu hao kununua magazeti hayo,
wakihisi ama zingevuruga harakati zao za uchaguzi au zingewafunua wabunge kuhusu
kashfa hiyo ya kiwanja.

Waandishi wa habari wa Mwananchi waliokuwapo katika viwanja vya Bunge walikuwa
na wakati mgumu kujibu maswali ya wabunge waliotaka kufahamu sababu ya kutokuwapo kwa gazeti hilo mjini hapa.

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, alihoji sababu ya mtu mmoja kuwanyima Watanzania
wote walioko Dodoma fursa ya kupata habari kutokana na hofu anayoijua mwenyewe.
“Mimi kila nikiuliza naambiwa kuna watu wamelinunua gazeti lote wamekwenda kulichoma, nikawauliza kwani limeandika nini kibaya dhidi yao? Lakini hawanijibu!”alisema
Mrema.

Habari zisizo rasmi zilidai kuwa magazeti hayo yalinunuliwa na mawakala wa kigogo mmoja
ambaye anahusishwa na uuzaji au ununuzi wa kiwanja hicho kilichopo Barabara ya Nyerere.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ukusanyaji wa gazeti hilo ulianzia eneo la usambazaji katikati ya mji na kila muuza magazeti aliyekuwa akiuziwa alikuwa akidakwa na
kutakiwa kuyauza.
 
Alhaji Mkulo mwaka huu ataipata. Ila kwa jinsi alivyo mchawi utashangaa bosi wake anamteua kuwa naibu makamu wa Rais na Waziri wa fedha hata kama katiba haitazingatiwa
 
Si hujuma bali mwananchi waulize Mwananchi wenyewe usiishi kwa matumaini ndugu na kuhisi tu
 
Alhaji Mkulo mwaka huu ataipata. Ila kwa jinsi alivyo mchawi utashangaa bosi wake anamteua kuwa naibu makamu wa Rais na Waziri wa fedha hata kama katiba haitazingatiwa

Duh huyo mzee naona kapwaya maeneo ya kusimamia fedha zetu.
 
si hujuma lakini kwa siku hiyo biashara ilikuwa nzuri sana, tusiishi kwa hisia tu; huenda mwananchi walitoa nakala chache
 
mwananchi lahujumiwa dodoma
gazeti la mwananchi linalochapwa na kampuniya mwananchi communications ltd (mcl), juzililigeuka bidhaa adimu mjini dodoma baada ya
watu wasiojulikana, kulihujumu na kununua nakala zote.

Haijafahamika hasa sababu za mtu au watu hao kukusanya nakala zote za gazeti hilo na
kuziondoa katika mzunguko, lakini taarifa zinadai lilikuwa na habari ambazo zilikuwa
zikitishia masilahi yao.

Katika ukurasa wa kwanza kulikuwapo na habari
tatu kubwa; moja ikihusu kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa wabunge wa bunge la afrika mashariki uliomalizika juzi
usiku.

Licha ya habari hiyo, kulikuwapo na habari iliyomhusu waziri wa fedha na uchumi, mustafa mkullo, kuhusishwa na kashfa ya uuzaji wa kiwanja kimoja kilichopo barabara ya nyerere, dar es salaam.

Habari hizo mbili ndizo ambazo zinahisiwa zilisababisha watu hao kununua magazeti hayo,
wakihisi ama zingevuruga harakati zao za uchaguzi au zingewafunua wabunge kuhusu
kashfa hiyo ya kiwanja.

Waandishi wa habari wa mwananchi waliokuwapo katika viwanja vya bunge walikuwa
na wakati mgumu kujibu maswali ya wabunge waliotaka kufahamu sababu ya kutokuwapo kwa gazeti hilo mjini hapa.

Mbunge wa vunjo, augustine mrema, alihoji sababu ya mtu mmoja kuwanyima watanzania
wote walioko dodoma fursa ya kupata habari kutokana na hofu anayoijua mwenyewe.
“mimi kila nikiuliza naambiwa kuna watu wamelinunua gazeti lote wamekwenda kulichoma, nikawauliza kwani limeandika nini kibaya dhidi yao? Lakini hawanijibu!”alisema
mrema.

Habari zisizo rasmi zilidai kuwa magazeti hayo yalinunuliwa na mawakala wa kigogo mmoja
ambaye anahusishwa na uuzaji au ununuzi wa kiwanja hicho kilichopo barabara ya nyerere.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ukusanyaji wa gazeti hilo ulianzia eneo la usambazaji katikati ya mji na kila muuza magazeti aliyekuwa akiuziwa alikuwa akidakwa na
kutakiwa kuyauza.

dawa ndogo, ni mwananchi kuzirudia habari hizo upya
 
hakuna hujuma hapo kibiashara... hujuma ni kwa walengwa tu, wananyimana habari

Dawa ni mwananchi kutoa special edition ya gazeti hilo na kama inawezekana kuweka edition ya weekly hot topic na waitoe ijumaa au jumamamosi
 
mwananchi lahujumiwa dodoma
gazeti la mwananchi linalochapwa na kampuniya mwananchi communications ltd (mcl), juzililigeuka bidhaa adimu mjini dodoma baada ya
watu wasiojulikana, kulihujumu na kununua nakala zote.

Haijafahamika hasa sababu za mtu au watu hao kukusanya nakala zote za gazeti hilo na
kuziondoa katika mzunguko, lakini taarifa zinadai lilikuwa na habari ambazo zilikuwa
zikitishia masilahi yao.

Katika ukurasa wa kwanza kulikuwapo na habari
tatu kubwa; moja ikihusu kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa wabunge wa bunge la afrika mashariki uliomalizika juzi
usiku.

Licha ya habari hiyo, kulikuwapo na habari iliyomhusu waziri wa fedha na uchumi, mustafa mkullo, kuhusishwa na kashfa ya uuzaji wa kiwanja kimoja kilichopo barabara ya nyerere, dar es salaam.

Habari hizo mbili ndizo ambazo zinahisiwa zilisababisha watu hao kununua magazeti hayo,
wakihisi ama zingevuruga harakati zao za uchaguzi au zingewafunua wabunge kuhusu
kashfa hiyo ya kiwanja.

Waandishi wa habari wa mwananchi waliokuwapo katika viwanja vya bunge walikuwa
na wakati mgumu kujibu maswali ya wabunge waliotaka kufahamu sababu ya kutokuwapo kwa gazeti hilo mjini hapa.

Mbunge wa vunjo, augustine mrema, alihoji sababu ya mtu mmoja kuwanyima watanzania
wote walioko dodoma fursa ya kupata habari kutokana na hofu anayoijua mwenyewe.
"mimi kila nikiuliza naambiwa kuna watu wamelinunua gazeti lote wamekwenda kulichoma, nikawauliza kwani limeandika nini kibaya dhidi yao? Lakini hawanijibu!"alisema
mrema.

Habari zisizo rasmi zilidai kuwa magazeti hayo yalinunuliwa na mawakala wa kigogo mmoja
ambaye anahusishwa na uuzaji au ununuzi wa kiwanja hicho kilichopo barabara ya nyerere.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ukusanyaji wa gazeti hilo ulianzia eneo la usambazaji katikati ya mji na kila muuza magazeti aliyekuwa akiuziwa alikuwa akidakwa na
kutakiwa kuyauza.

mkulo ni mwizi. Mkikumbuka wananchi wa kilosa walisema sio raia lakini ccmafisadi wamemngangania kwa vile wanaiba pmj
 
Back
Top Bottom