Kwa hili KKKT hapa kuna walakini...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Baada ya Babu wa Loliondo aliyekuwa Mchungaji mstaafu wa KKKT Mch.Mwasapile kuanza kutoa tiba kupitia dawa aliyodai ameoteshwa na Mungu...Kanisa lilimrudisha kazini haraka...Je?

  1. Kwanini kanisa limemrudisha kazini huyu Mchungaji baada ya kuanza kutoa hiyo dawa na si kabla ya hapo?
  2. Kanisa lina maslahi gani na hii dawa?
 
Only83 , kama una imani njema basi hata majibu ya maswali yako utakuwa unayo mwenyewe.
 
Sijui kama umefanya utafiti wa kutosha juu ya uliyoyaandika. Lakini jinsi ninavyojua juu ya kustaafu kwa wachungaji wa KKKT ni kama formalities lakini kwa hakika wanakuwa bado wapo katika huduma hata mavazi ya kichungaji huwa wanazikwa nayo.Mfano ninaye baba yangu mdogo amestaafu toka 1999 lakini toka wakati huwo amekuwa akipelekwa na kanisa kuhudumia sehemu mbalimbali kama mchungaji wa usharika na hata akirudi kijijini kwetu bado anaendelea kutoa huduma za kiroho.Na amewahi sema toka astaafu ndio wakati ambao amekuwa na kazi nyingi za kanisa kuliko wakati mwingine wa utumishi wake. Na hata sasa hayupo kijijini kwetu kapangiwa usharika anaendelea kuhudumia. Hivyo ndivyo itakuwa hata kwa mchungaji Mwaisapile kwani wote wapo KKKT na si kama unavyotaka watu waamini vinginevyo.Ingawa si msemaji wa KKKT wala Mwaisapile lakini kama muumini nimetimiza wajibu wangu.Kwani neno linasema mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachche...Ndio maana hawa wazee wanaendelea kutumika.
 
kazi ya uchungaji japo mtu anaenda kusoma theolojia ili kumshape, ni kazi ya wito. Once you are in you are in for life.
 
sawa na madaktari and the same huwezi kulala home ati we ni mstaafu unless uzee umekubana haswa
 
wewe unaonekana huna taarifa, tomas laiza alipokua anamrudisha kwenye huduma alisema anachofanya mwasapile ni zaidi hata ya uchungaji so kwa kuzingatia huduma anayoitoa tunamrudisha kwenye utumishi na tutampa ushirikiano which means atapewa mshahara na huduma zingine za kitumishi. Sasa wewe ulitaka arudishwe lini?
 
Thanx nimewapata jamani...msije makanitoa roho wadau wa Babu...........
 
sijawaelewa KKKT kwa kuunga mkono huduma hii hadi watakapotueleza vizuri sababu za kuamini ufunuo kama huu bila kuujaribu kama umetoka kwa Mungu. kama wameoishaujaribu na kujiridhisha, kwa nini wasifundishe makanisani na kutoa elimu kwa watu wote? si ndio maana ya injili na wito walioitiwa?

hayo ya kutoa ushirikiano na eti anafanya zaidi ya wachungaji kwa kweli kauli kama hizi zinasikitisha sana zinapotolewa na watumishi wa Mungu.

Mungu atainuliwa daima katika nchi na miisho ya dunia itauona utukufu wake

utukufu una yeye hata milele na milele
 
Huyu miss hata mimi namshangaa. Kwani ameambiwa ile ni elimu kama physics kwamba utamfundisha kila mtu jinsi ya kutemgeneza mashine ya kusaga ili nao pia wafundishane baadae!.
 
sijawaelewa KKKT kwa kuunga mkono huduma hii hadi watakapotueleza vizuri sababu za kuamini ufunuo kama huu bila kuujaribu kama umetoka kwa Mungu. kama wameoishaujaribu na kujiridhisha, kwa nini wasifundishe makanisani na kutoa elimu kwa watu wote? si ndio maana ya injili na wito walioitiwa?

hayo ya kutoa ushirikiano na eti anafanya zaidi ya wachungaji kwa kweli kauli kama hizi zinasikitisha sana zinapotolewa na watumishi wa Mungu.

Mungu atainuliwa daima katika nchi na miisho ya dunia itauona utukufu wake

utukufu una yeye hata milele na milele
Kitu kinachotoka kwa Mungu hakina majaribio. Nuhu alipoambiwa ajenge lile safina kuna watu walimwona chizi, mpaka maji ya mvua yalipowafika kifuani wakaanza kumpigia kelele awafungulie. It was too late.
 
Naomba nijuzwe...

Nimeelezwa na kuwa kwa kawaida wachungaji ni watu wenye elimu kubwa katika masuala mbalimbali pia na mishahara yao ni mikubwa. Pia wanatunzwa vizuri sana na Kanisa.

Swali: Iweje kwa utumishi uliotukuka wa Mwasapila aishie kuishi kwenye kibanda kile?

Kanisa lilikuwa wapi siku zote?

Alitengwa?

Kwa nini?
 
Kuna mambo yakufundishana ila kwa hili nadhani likowazi halipo katika mfumo huo.
 
Naomba nijuzwe...

Nimeelezwa na kuwa kwa kawaida wachungaji ni watu wenye elimu kubwa katika masuala mbalimbali pia na mishahara yao ni mikubwa. Pia wanatunzwa vizuri sana na Kanisa.

Swali: Iweje kwa utumishi uliotukuka wa Mwasapila aishie kuishi kwenye kibanda kile?

Kanisa lilikuwa wapi siku zote?

Alitengwa?

Kwa nini?

inasikitisha sana kwa kweli, ndiyo maana madhehebu mengine yameweka utaratibu kuwa mchungaji akisha tumikia kanisa kwa kipindi fulani ni lazima waumini waunde utaratibu wa kuchangishana fedha ili wamjengee mchungaji wao nyumba.
 
Back
Top Bottom