Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Kikwete ataka kuziona ndege za ATCL angani
Mwandishi Maalumu
Daily News; Saturday,January 17, 2009 @21:15
"Ningependa hata tuanze kuruka Jumatatu kwa sababu ni dhahiri hatuwezi kuendelea kufanya kazi namna hii," alisema Rais Kikwete alipokutana na uongozi wa Wizara ya Miundombinu wakiwamo wakuu wa ATCL.
"Kutaneni haraka sana, yaani nyie ATCL, Wizara ya Miundombinu, na Wizara ya Fedha, ili kupata ufumbuzi wa mara moja utakaotuwezesha kuanza kutoa huduma zetu tena," Rais Kikwete aliwaambia viongozi hao juzi usiku katika mikutano yake na wizara mbalimbali kutathmini utendaji wa Serikali yake na mashirika yaliyoko chini ya wizara hizo kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ATCL inakabiliwa na changamoto mbili kubwa: moja ni kuhakikisha kuwa ndege zake zinarudi hewani mara moja, na pili ni kutafakari kwa kina nini hali ya baadaye ya kampuni hiyo ya ndege inayomilikiwa na Serikali.
"Tumepoteza nafasi na mapato. Hatuwezi kuendelea kusubiri tena. Je ni msaada gani na kiasi gani cha fedha mnahitaji kuweza kuanza tena kutoa huduma?," aliuliza Rais Kikwete katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na viongozi wa taasisi nyingine zilizoko chini ya Wizara ya Miundombinu, ikiwamo Mamlaka ya Usalama wa Anga (TCAA).
Rais alitoa maelekezo baada ya kuwa amepata maelezo ya kina kutoka kwa uongozi wa ATCL kuhusu matatizo ya karibuni ya kampuni hiyo, ambayo yalisababisha kuamriwa kusimamisha huduma kwa sababu ya kushindwa kutimiza masharti ya TCAA. "Nataka kujua kiini cha matatizo yetu ya karibuni mpaka tukasimamisha kurusha ndege zetu? Tulifikaje hapo?
Je tumetoka na kama tumetoka, tunafanya nini ili tusirudi kwenye matatizo hayo? Pili, nataka mnielezee mipango na hali ya baadaye ya shirika letu la ndege kibiashara," aliwaambia. Uongozi wa ATCL ulitoa maelezo ya kina na kufuatia mjadala ambao hatimaye ulifikia ukingoni mwa kikao kukubaliana kuhakikisha kuwa ATCL inaanza kutoa tena huduma zake haraka iwezekanavyo. Pamoja na kwamba ATCL imefunguliwa kuanza kutoa huduma zake, ndege zake hazijaanza kuruka kwa sababu mbalimbali ambazo ndizo Rais aliagiza zitafutiwe majawabu na ndege zianze kuruka tena haraka iwezekanavyo.
Pendekezo:
Kama tatizo lao ni pesa (kama Rais anavyoonesha kufikiria) napendekeza Serikali iwape ATCL bilioni 500!!! wataanza kuruka Jumatatu!