Kwa hili, JK awaombe radhi Watanzania kisha athibitishe kuwa ni Muongo. Hatutaamini asemacho tena

chuki chuki chuki.kikwete hana tatizo,kinachojitokeza hapa ni jicho la husda kwa baadhi yetu.kwa hiyo mnataka tumwamini lowasa kwa sababu alijiuzulu?tu
ondoe imani kwa kikwete kwa kuwa watendaji wake walimhujum?fahamuni kwamba kila mtu akiwamo mleta thred angependa kuwa mteule wa nafasi flani ila ameikosa ndo mana analalamika.kikwete hana shida anawajibika na anawahudumia watanzania bila ubaguzi.

mtoa mada kuna nafasi kaikosa,si ndiyo hiyo uliyonayo wewe?
 
Wanajamvi nimejaribu kumpima Mkuu wangu wa Kaya nimeshindwa kabisa kupata link na baadae nikawaza nikasema labda mie ndo mjinga. Hebu someni kauli hii ya Jk pale CCM ilipotimiza miaka 34 kule DODOMA.

"Ukweli siwajui wenye Dowans na wala kampuni hiyo siijui...wapo wanaosema
sijasema kuhusu Dowans kwa sababu wanaohusika ni rafiki zangu....sijasema kwa
sababu Chiligati na Pinda wamesema, waliyosema yametokana na kikao changu cha
kamati kuu...." Hii ni kauli ya Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 34 ya
kuzaliwa CCM.JK ameeleza kuwa Wakati waziri wa Nishati na Madini Salum Msabaha
alipomfuata kudai kuwa wizara ya fedha imegoma kuwalipa Dowans, lakini yeye
alimtahadharisha kuwa hii inaweza kuwa kampuni feki.....

Haya aliyasema na niliona mwenyewe na watanzania wengine waliona na kusikia.
Vide hii hapa Hotuba ya JK akiikana Dowans - YouTube

Mbona Dowans na Richmond.Umenichanganya hapo mkuu.

Kama hujui Dowans na Richmond huijui vilevile.......Sheraton na Moven pik.......huijui Tanganyika na Tanzania.......lakini poa. Ilianza Richmond wakachakachua ikawa Dowans sasa hivi ni Symbion
 
mtoa mada kuna nafasi kaikosa,si ndiyo hiyo uliyonayo wewe?

Nafasi niliyoikosa ni mafuta ya taa yenye bei nafuu kijijini kwetu.........umeme......ndugu zangu kukosa mkopo wa elimu.........watumishi hasa walimu kudanganywa kama watoto kwa kutopewa malipo yao....... Tanzania kuwa ya 152 kati ya nchi 178 mwaka huuuuu kwa umaskini............... wagonjwa kukosa huduma iliyobora kwenye zahanati, hospitali na vituo vya afya mbalimbali.......... kukosa meli iliyoahidiwa na Kikwete Huku kagera.....na mengine mengiiiiiiiiiii......hayo ndo niliyoyakosa. Moyo wangu ni kwa wananchi na ndio maana niko pembezoni mwa nchi naihudumia jamiiiii. Sitaki vyeo vya kubebwa. Bora niwe mwenyekiti wa Tawi wa CHADEMA kijijini kuliko kuwa na wadhifa wowote magambani
 
Siku hizi imefikia wakati nikimuona Mh. anautubia basi hapo hapo nahama channel. Swali inakuwaje watu wengi bado wanasikiliza na kumwamini huyu jamaa. Inakuwaje watu wanafunga safari kwenda uwanjani kumsikiliza MH. JK hivi ni kweli wale watu walioudhuria sheree za uhuru ni wafanya kazi wa serikari? na wali lazimishwa?
 
hUWA WANAENDA KUMSHANGAA............. anavyodanganya bila aibu na kuona tabasamu
 
Jaji Lewis Makame na Kiravu ndio wa Kulaumiwa hapa... mi ntaendelea kuwalaumu mpaka mwisho na kwa hili wasidhani hawatajibu siku ya mwisho
 
Wanajamvi nimejaribu kumpima Mkuu wangu wa Kaya nimeshindwa kabisa kupata link na baadae nikawaza nikasema labda mie ndo mjinga. Hebu someni kauli hii ya Jk pale CCM ilipotimiza miaka 34 kule DODOMA.

"Ukweli siwajui wenye Dowans na wala kampuni hiyo siijui...wapo wanaosema
sijasema kuhusu Dowans kwa sababu wanaohusika ni rafiki zangu....sijasema kwa
sababu Chiligati na Pinda wamesema, waliyosema yametokana na kikao changu cha
kamati kuu...." Hii ni kauli ya Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 34 ya
kuzaliwa CCM.JK ameeleza kuwa Wakati waziri wa Nishati na Madini Salum Msabaha
alipomfuata kudai kuwa wizara ya fedha imegoma kuwalipa Dowans, lakini yeye
alimtahadharisha kuwa hii inaweza kuwa kampuni feki.....

Haya aliyasema na niliona mwenyewe na watanzania wengine waliona na kusikia.
Vide hii hapa Hotuba ya JK akiikana Dowans - YouTube

Baadae kidogo kwenye Mkutano wa NEC mwaka huu pale Lowassa alipopewa nafasi ya kuongea Akasema maneno haya kwa Kikwete ambaye hajayakanusha hadi leo kwa sababu alitikisa kichwa kuyakubali.

Lowassa amkumbusha Rais Kikwete

“Lakini Mwenyekiti, naamini utakumbuka jinsi nilivyotaka kuvunja mkataba wa Richmond, nilikupigia simu ukiwa nje ya nchi, lakini ukasikiliza ushauri wa kamati ya makatibu wakuu (Kikwete akatikisa kichwa kukubaliana naye) , mheshimiwa ushauri wa kamati ya makatibu wakuu ndiyo uliopelekea mkataba usivunjwe.
“Pia naomba nikumbushe, nikiwa Waziri wa Maji niliwahi kutuhumiwa kuhusiana na kampuni ya City Water, tena nashukuru Mzee Nimrod Mkono yupo hapa, tukaenda kwenye kesi tukashinda. Sasa katika hili la Richmond kosa langu ni lipi? Je kuwajibika kwa maslahi ya chama changu na ya serikali yangu, utakumbuka ripoti ya Dk. Harrison Mwakyembe wakati anahitimisha Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, alisema kuna aina mbili ya uajibikaji, kwa makosa ya kiongozi mwenyewe na watendaji walioko chini ya kiongozi,

“Dk.Mwakyembe akasema Waziri Mkuu aliyejiuzulu amejiuzulu si kwa makosa yake, bali ni makosa ya watu waliokuwa chini yake (huku akiwa ameshikilia Hansard ya Bunge),”

“Mwenyekiti naomba nikukumbushe kuhusu kashfa zinazohusiana na ‘political perception’, kama si busara za kina Mzee Mkapa mwaka 1997 kule Zanzibar, leo hii usingekuwapo hapo ulipo na ulisema urais ni mipango ya Mungu.

“Unakumbuka kina Mzee Sozigwa jinsi walivyokuja na mafaili kwenye mkutano huo wa NEC kwa ajili ya kukumaliza.

“Hata nilipokutana na Mzee Msekwa pale Dar es Salaam, aliniambia kuna watu wananoa mapanga kwa ajili ya urais wa Lowassa.

“Kibaya zaidi, wanaonitukana ni wana-CCM (Nape, Chilligati na wenzao), lakini hata CHADEMA na wapinzani wengine hawanitukani,” alisema Lowassa.

MY TAKE
Sasa ninachojiuliza na kushangaa ni kuwa Lowassa alipompigia simu JK si kwamba alikuwa anaitambulisha Richmond kwa JK bali alikuwa anataka kuvunja mkataba na Richmond ambayo JK alikuwa akiifahamu!!!!!!!!!!!^$%#* 100%. Kwa nini Watanzania tudanganywe kiasi hiki alafu tuendelee kuchekacheka???? Sasa Jk atuambie vipi tene tuamini anachokisema. Kama ulikuwa huijui Richmond kwa nini Ulikataa mkataba usivunjwe. Hii ni aibu kama pale baba awadanganyavyo wanae kisha wakajua kuwa baba yao muongo. Tuombe radhi vinginevyo hata utakayemrithisha kijiti ni dizaini hiyo hatutamchagua. Nina hasira vibaya sana ninavyoongea hivi ungeniona sura usingeamini.

Usingeamni kama mimi ndiye nilibeba T- Shirt za CCM mwka 2005 na kuwagawia wanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani na kuwasombelea kwenda Diamond Jubilee kukushangilia tukiwa na matumaini makubwa na wewe. Kumbe loo... hadi aibu sasa hivi... kila aliyesema kuwa wewe hutafanya kama ulivyovuma nikambishia sasa hivi namuomba radhi. Na jamaa yangu aliyekuwa akisherekea kunywa soda za wanaharakati wakati anamsaidia Mnyika kuomba kura pale Mabibo Hostel chumaba hadi chumba ili Mnyika ashinde jimbo la Ubungo kisha kura akawapa magamba wote lazima awaombe radhi wanaharakati na zitapike hizo soda. Huyu mzee Jk yaaani...... basi ngoje nilie na kutubu kwa Mungu wangu ninayemjua. Najua waliofanya makosa kama mimi 2005 wako wengi kubalini kisha tusonge mbele. CHADEMA tekelezeni myasemayo kwa wananchi ili na wao wananchi waone tofauti.

Mimi binafsi nakushukuru kwa kutubu makosa na ujinga wako.Huyu jamaa hata akitoa salaam yake huwa naona kama ananidanganya tu sitaki hata kusikia jina lake.
 
kwa kweli huyu katoa kali..........maisha magumu every where mafuta taabu magari kibao kwa sasa Bukoba hapa balaaa...watu wamepaki.

Hii si foleni eti traffic jam......mafuta hakuna Bukoba mjini...ni tabu tupu..Baba riz wala habari hanaga.
 
wananchi tulishamwona mwongo ila usala wa taifa jwtz(shimbo) na tume ya uchaguzi ndio waliomweka madarakani kwa maslahi ya binafsi.
 
Lakini Watanzania mna uelewa wa namna gani. Mimi niko nje ya Tanzania tangu miaka 20 iliyopita, nimekutana na JK mara mbili tu na nilimtathmini vilivyo na kuwakataza familia yangu wote wasimpigie.
Nyie mnaye hapo kila siku, mmeona utendaji wake tangu Waziri wa Nishati, mambo ya Nje, Fedha....halafu mnakuja kusema hamkujua?
Endeleeeni kufikiria mmerogwa, hakuna uchawi ni uelewa mdogo na uvivu wa kufikiri. Mmezoea kufuata mkumbo tu.
Huyu jamaa hata katika ahadi zake za ugombea za kwanza kabisa, alidiriki kusema atatengeneza fursa za kazi milioni 2 katika mwaka wa kwanza tu! Hamkuona huo ulikuwa uwongo mtupu? Hamkuona kuwa alikuwa ataka kufikia madaraka kwa namna yeyote ile, hata kuwatusi watu waliotoa mchango mkubwa kwa TZ (Salim Salim) ili mradi tu? Sasa unajuta hukujua?
Hukusikia hotuba ya Mwl. kwamba ukimwona mtu anapapatikia kuwa rais mkimbie kama ukoma? Yote haya hukuyajua? Kama hukujifunza huko nyuma kuna ushahidi gani kuwa utajifunza 2015? Na wako wengi zaidi yako, au- watu kama wewe ndio majority Tanzania ndiyo maana watu hawa wanapata nafasi. Nina note kuwa ulikwenda Chuo Kikuu kugawa T-shirt, hiyo inamaanisha kwa namna fulani wewe si Mtanzania wa kawaida, ni msomi. Sasa ikiwa msomi yuko hivi......sembuse? Tanzania is a lost case. The only remedy is ....
 
Mkuu malizia basi the only remedy.................. nini sema tuelewa. Pili sema watanzania Tuna uelewa wa namna gani vinginevyo ulishakana uraia wa huku..................tatu aliyesoma siyo Mtanzania wa Kawaida!!!!!!!!!!!! Nnne Asante mkuuu....waambie na Watanzania wengine maana alishinda kwa kishindo!! Mwisho hata iweje nina hasira na Kikwete....kwa alichowafanya Watanzania.
 
Jamani, hivi kwa nini tunapoteza muda kumjadili huyu JK? it means u still don't know that the guy is unreliable and not
strong on his own.........I am sorry 4 u guys.......... that's JK
 
Back
Top Bottom