Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,428
- 4,128
Ambao mna mashaka na dhamira ya Ulimwengu jitahidini kuisoma hiyo barua vizuri sana (wengine wanasema"between the lines") na pengine hata kusubiri mwisho wake. Jenerali ni mtu mwenye kufikiri na kutoa mada za kufikirisha sana. Aidha, anao uandishi wa kiswahili sanifu wa kupigiwa mfano. Kwa wanaoijua lugha hii vizuri na kuweza kuiwianisha na nyinginezo wataelewa thamani ya maandishi yake katika uchambuzi wa kimantiki. Hivyo, kuyachambua maandishi yake kirahisirahisi tu na kujaribu kumtumbukiza tu kwenye "box" la ama wenye njaa au wapinga ufisadi, n.k., ni kutotendea haki jitihada za binadamu kufikiri.