Jenerali anajaribu tu kumkumbusha Kikwete kuwa dhamana ya kuchaguliwa (hata kama ni kwa kuchakachua - safari hii) kuwa kiongozi wa nchi ni dhamana kubwa amabayo kwa watu wengi ni sawa na kutafsiri kuwa anaonekana kama ni mkombozi. Na kwa mantiki hiyo, viongozi wengi hujisahau na kulewa madaraka, na kusahau dhima nzima ya wao kuwapo madarakani.
Pia amekwenda na dhana ya kunguru mwoga hukimbiza bawa lake; ili itakapotokea na kuonekana ameongea vibaya basi (kwa watu, hususani watawala) na ionekane si kwa dhamira mbaya. Muungwana anaomba radhi mapeeema. Yakiyomkuta huko nyuma yatosha; binadamu akiumwa na nyoka, akiona unyasi anaweweseka.
Labda sehemu ya pili ya hii barua, itatupatia mwanga zaidi. Ila hii iko kifasihi zaidi. Na tuisome tena na tena.