Kwa hili CUF na NCCR mnahitaji pongezi

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,482
14,352
Kwanza napenda kukipongeza Chama Changu cha Demokrasia na Maendeleo kwa ushindi katika jimbo la Arumeru Mashariki na pongezi za dhati ziwafikie Makamanda wote Dr Slaa, Mbowe Freeman, Rev Natasye, Vicent Nyerere, John Mrema na bila kumsahau kamanda Lema kwa kusimamia Show yote bila Zengwe..

Nampongeza kamanda Joshua Nassar (Josh Nas) kwa ushindi ulioupata naamini haki haipotei pmoja na kudhulumiwa 2010 lakini haki yako umeipata...

Nitakua mchoyo wa fadhila nisipowashukuru watani wangu wa jadi NCCR na CUF, kwa kutokushiriki katika uchaguzi huu maana wangeshiriki kulikua na uwezekano wa kuzigawa kura na CCM wangeweza kutumia mbinu hii kujitangazia ushindi, nawapongeza sana wana NCCR na CUF..
 
Hilo sahau kabisa, NSSR na CUF wasingefanya tofauti yoyote, na hilo wananlijua sana ndiyo maana waliu-chuna. Kwani umesahu Igunga? CUF ilikuwa tishio kwa nani?
 
Kwanza napenda kukipongeza Chama Changu cha Demokrasia na Maendeleo kwa ushindi katika jimbo la Arumeru Mashariki na pongezi za dhati ziwafikie Makamanda wote Dr Slaa, Mbowe Freeman, Rev Natasye, Vicent Nyerere, John Mrema na bila kumsahau kamanda Lema kwa kusimamia Show yote bila Zengwe..

Nampongeza kamanda Joshua Nassar (Josh Nas) kwa ushindi ulioupata naamini haki haipotei pmoja na kudhulumiwa 2010 lakini haki yako umeipata...

Nitakua mchoyo wa fadhila nisipowashukuru watani wangu wa jadi NCCR na CUF, kwa kutokushiriki katika uchaguzi huu maana wangeshiriki kulikua na uwezekano wa kuzigawa kura na CCM wangeweza kutumia mbinu hii kujitangazia ushindi, nawapongeza sana wana NCCR na CUF..
Watani wa jadi ni Rushwa
 
Ningewapongeza kama tu wangekaa pembeni na kumu-endorse Josh kabla ya kupigwa kura. Bila ya kufanya hivyo ni unafiki ule wa sishangilii yanga wala simba bali atakayeshinda.
 
Back
Top Bottom