Kwa hili Chenge hakamatiki

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
MWANASHERIA Mkuu mstaafu, Andrew Chenge, leo amekana mashitaka tisa kati ya 10 likiwemo la kusababisha vifo vya wanawake wawili jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mashitaka aliyoyakana mwanasiasa huyo ni kuendesha gari lisilo na bima.

Kwa mujibu wa Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), David Mwafimbo, Chenge anakabiliwa na mashitaka 10.

Mwanasiasa huyo amekubali shitaka moja kwamba aliendesha gari siku ambayo ajali hiyo ilitokea.

Wakili wa Chenge, Simon Mponda, ameiomba Mahakama itoe kutoa ushahidi wa vielelezo vyote vitakavyotumika katika kesi hiyo.

Vielelezo hivyo ni pamoja taarifa ya ukaguzi wa gari, taarifa ya upelelezi wa vifo vilivyosababishwa na ajali hiyo, na ramani ya eneo la ajali.

Hakimu Mkazi Kwey Rusema, ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 28, mwaka huu wakati mashahidi watakapoanza kutoa ushahidi.

Inadaiwa kwamba, Chenge alitenda makosa hayo Machi 27, mwaka jana saa kumi na nusu alfajiri, katika barabara ya Haile Sellassie, Oysterbay wilayani Kinondoni.

Kwa mujibu wa madai hayo, Chenge aliendesha gari aina ya Toyota Hillux Double Cabin lenye namba za usajili T 513 ACE, hakuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara na akagonga bajaj iliyokuwa na namba ya usajili T 736 AXC, na kusababaisha vifo vya wanawake wawili, Victoria George na Beatrice Constantine.

Inadaiwa kwamba, Chenge alisababisha uharibifu wa bajaj hiyo na kwamba aliendesha gari ambalo halikuwa na bima.

Mbunge huyo wa Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga amewahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri wa Miundombinu.


Maoni yangu: The red highlighted part means that the advocate wants court to take off some supporting documents and to favour his customer for whose interest? LOL


 
Huyu Bwana anasikitisha sana maana fani aliyosomea imemlea mpaka akawa mtu maarufu sasa inamrudi mwenyewe. Sheria! Balaa!
 
Wakili anaweza kuomba vielelezo na ushahidi kutolewa kama haukukusanywa kihalali! Hii habari haijakaa vizuri. Ungetupa sababu za yeye kuomba hayo ndo ingekuwa na maana zaidi!
 
Back
Top Bottom