Kwa Hili, 2015 ni Mbali sana....

Well said, lakini uzalendo ulikufa na azimio la Zenj, "ponda mali kufa kwaja". Tupo kwenye pre-bolshevik/yelstin USSR.
 
Sikumbuki Wafaransa walipoambiwa 'kama hakua mkate wale keki na siagi' walifanya nini, au kule Romania kwa Nolascus Caescescu(?)
 
Huu msamiati nimetokea kuupenda sana "Impossible its a word found only on the dictionary of fools". Tukilazimisha upatikanaji wa katiba mpya na tume mpya na huru ya uchaguzi hawa jamaa wanang'oka tu tena kirahisi kuliko watu tunavyofikiria.

Gharama ya mapinduzi ya nje ya sanduku la kura ni kubwa na athari zake ni kwa vizazi vingi. Angalia ni kwa nini jirani zetu wa kongo hawamalizi vita vyao. Libya hakutokaa kuwe na amani na nigeria pia kadhalika kutokana na utajiri wao. Nchi hii ni tajiri ni kila mzungu aliye na akili timamu anasali huko waliko sie tupigane na ndio sababu wanazidi kuisupport ccm ili tupate hasira tuzichape wao waingie kuchukua utajiri wetu kama kawaida yao. Lets leave our eyes open.
 
STK One mada yako ni nzuri sana na nakupa heshima yako. Problem kubwa tuliyo nayo Tanzania ni kukosekana kwa uelewa wa tofauti ya uongozi wa kiserikali na wa kichama. Maana yangu ni kwamba kwa sababu tulikuwa nchi ya chama kimoja kwa muda mrefu, watu including viongozi wa juu hawajui tofauti ya administration ya serikali na ile ya chama tawala. Hili hasa ni tatizo kubwa kwa sababu wale viongozi wengi tulio nao wamekuzwa kwenye one-party state na wameingia kwenye uongozi wa siasa wakati nchi ilipokuwa chini ya chama kimoja. Ndiyo maana utakuta anayeteuliwa na rais kuwa mkuu wa wilaya kama ya Same (for example) anaweza kuwa ni mbunge wa Mbulu akiwakilisha chama tawala. Hapo hapo kuna mwenyekiti wa chama wa wilaya hiyo na katibu wake. Tunashindwa kutenganisha cheo cha kiserikali na vile vya chama. Relevance ya ninachosema ni hii. Wewe umeshauri vizuri sana kuwa ifanyike mass education ili kuwaelimisha raia regardless ya chama chao, kuhusu umuhimu wa kuyaangalia matatizo yao na kuwapigia kura watu walio na uwezo wa kuyatatua. Sasa hiyo elimu itatolewa na nani? Kibali cha kuwakutanisha watu atanipa nani? Hata kama nikisema mimi sina chama, mkuu wa wilaya ambaye alitakiwa kuwa kiongozi wa serikali na kwa hivyo asiyependelea, ndiye alitakiwa anisaidie kukutanisha watu kwa sababu tunaloongelea ni maendeleo ya wilaya yake. Askari ambao hawatakiwi kupendelea sehemu yeyote ndio walitakiwa wanipe kibali cha mkutano, ili wananchi waongelee maendeleo ya sehemu yao, including vitu kama hali ya nyumba wanazoishi askari. Nakupa guarantee kuwa kwa hali ya sasa polisi hawatanipa kibali kama wakijua nina lengo la kuwaelimisha raia. Hata kama nikimpata OCD ambaye ana mwamko na uchungu wa maendeleo, ataogopa kutoa kibali kwa sababu wakubwa zake ambao hawana uelewa wa kazi zao na uhusiano wa vyeo vyao na siasa, watamwadhibu.

Tuna tatizo kubwa ambalo linatakiwa kiongozi mwenye ujasiri wa hali ya juu. Tunataka kiongozi wa juu ambaye yuko beyond reproach, ambaye hana skeleton kwenye closet yake, kiongozi ambaye hataogopa kumkemea mwizi kwa sababu ana uhakika yule mwizi hatageuka nyuma aseme na wewe si ulikuwepo nilivyokuwa naiba na nilikugawia kidogo?

Sasa mawazo yangu katika kusupport point yako ni haya: Kitu ambacho tunaweza kufanya kwa sasa quite frankly, ni kukazania katiba ibadilike. Katiba pamoja na mambo mengine, itaondoa uwezekano wa raisi kumteua mbunge wa Rombo kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya. Na sisi watanzania sijui kwa nini tunakubaliana na mambo yasiyokuwa na logic kabisa. Kama mbunge wangu ni mkuu wa mkoa kule Mbeya, ananiwakilishaje bungeni? Na kama ananiwakilisha, wale watu wa Mbeya wanaongozwa na nani wakati kiongozi wao wa serikali ananiwakilisha mimi mrombo kule bungeni? Hii shughuli ya kuwateua wabunge wachukue vyeo vya serikali ilianza wakati nchi zetu zimepata uhuru out of necessity. Viongozi wapya waliochukua nchi zao walikuwa hawana pool ya kutosha ya kuwapata viongozi bora kwa hiyo wale wachache waliokuwa tayari wamesha-prove wana uwezo na wanakubalika na wananchi walipewa vyeo kama hivyo kwa sababu ilikuwa ni muhimu.KATIBA NDIYO SOLUTION! Nakuhakikishia kuwa kama watu wote (wewe na mimi included) tutapigania mabadiliko ya katiba na kuhakikisha kwamba vyama havitupotoshi kwa manufaa binafsi, katiba mpya itatupa nchi mpya ifikapo 2015. Chama chochote kitakachochukua hatamu ifikapo 2015 kitatuongoza ipasavyo na wananchi watakuwa na sauti kama inavyotakiwa. Tatizo ninaloliona kwa sasa hivi ni kuwa Watanzania tutatukanana sana na tutauana sana kabla ya 2015.
 
mawazo mazuri na yanahitaji udhubutu wa hali ya juu sana kutokana na aina ya jamii tuliyonayo japokuwa inakwenda kwa mabadiliko kwa sasa
 
Kura ni kipande cha karatasi tu kama karatasi ya chooni (toilet paper)
Namconsult Joseph Kony (R.I.P Jonas Savimbi, Che Guavara, John Garang, Osama bin Laden)
Nitarudi..
 
Back
Top Bottom