Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,064
- 7,195
- Thread starter
- #21
Tatizo la kumtegemea Mtu mmoja ndilo hilo.
Katika mapambano yeyote TEAM work ndiyo SIRI kubwa.
Pia siku zote mpambano ni lazima uwe na plan A,B na C
A chain is a strong as its weakest link.
CCM wanalijua sana hili ndiyo maana mara zote humwandama sana kiongozi wa mpambano hata kumzushia uongo wa kufa.
Nia ya kumuandama kiongozi si kwamba wanamchukiaa kuliko wengine ila ni kwa sababu wanajua yeye ndiye strong link na wengine mliobaki ndo weakest.
Wakisha ivunja strong link weakest link mara nyingi huanguka zenyewe kwa woga.
Bend together and learn how to raise spirits and strength of each individual in the team.
Watu wote wanyonge duniani wana nguvu nyingi za ajabu kiasi cha kuweza kufanikisha jambo lolote lile.
Tatizo kubwa ni namna ya kutumia nguvu za wanyonge katika umoja wao na kwa faida yao wenyewe.
Siku zote nguvu nyingi za wanyonge hutumiwa katika kuhakikisha kwamba wanyonge hawatumii nguvu zao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya kuwaondoa katika unyonge wao, bali katika kuongeza mfarakano baina ya wanyonge.
Ukitaka kummaliza mnyonge kiulaini unamtumia mnyonge mwenzake.
If diamond is the hardest natural material on earth, that means it takes a diamond to shape a diamond.
Ukiona Mapambano kati ya wanyonge na wenye nguvu yazidi kupamba moto jua jambo moja tu, wenye nguvu wameshindwa kuwapata wanyonge wa kupambana na wanyonge wenzao.
Wale wapiga virungua FFU na Polisi wakivaa mashati ya Dukani ni CHOKA MBAYA ni wanyonge wa kutupwa.
Ndiyo maana mmoja wa watu wenye Hekima katika karne hii anatambua nguvu kubwa walizo nazo wanyonge na jinsi ambavyo mnyonge yeyote hatakiwi kusahau kwamba nguvu za wanyonge ndiyo hatari yenyewe.
This is a Quote from Nelson Mandela;
"Our deepest fear is not that we are inadequate. Our deepest fear is that we are powerful beyond measure "
tukitumia falsafa hii,twaweza kuushinda utawala huu wa chuo cha mkandara, hakika mgaya anatumia lugha ya vitisho kwenye matangazo yake kutisha watoto wa wakulima akijua ni waoga wa kufukuzwa chuo..
Nazani tukiweza kuunganisha nguvu yetu iliyopotea,na hapa ndipo watu kama akina Al-shabaab wenye moyo wakujitoa..na kusimama bila kuteteleka wanaitajika.. Najua UDSM haiwezi kukubali hali hii ata kidogo..