Elections 2010 Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA

najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

msimamo wa chadema haujabadilika

by dr. Wilbrod slaa on tuesday, december 14, 2010 at 7:29pm

kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa tbc ilieleza wazi kuwa kamati kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na sekretariat ya chama kuwa chadema imekataa matokeo ya uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo kikwete's presidency ni lawful it is illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, kamati kuu ikasisitiza " kuundwa kwa tume huru" kuchunguza dosari " irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, chadema ni chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "haiko tayari kuingia ikulu kwa kumwaga damu ya watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa katiba na sheria mbovu kama tuliyonayo leo, chadema inasisitiza upatikanaji wa katiba mpya, shirikishi na ya wananchi.

Upatakanaji wa katiba hii utakuwa na mchakato, na kama serikali haitaki, basi chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi katiba ya wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na busara daima huvuta heri.

source: gonga hapa msimamo wa chadema haujabadilika | facebook

nyongeza: kuna thread imewekwa hapa chini na mwanajamii mmoja (chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (lawful na legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi

moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: Legitimate - google search

zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.

Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: Meaning and definitions — infoplease.com.

kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principles

tukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

sheria inasema raisi ni raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.

hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.

kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule georgia

georgiandaily.com - Opposition to picket

saluti.
 
Mkuu...sasa tatizo si ndo hapo. Huoni Chadema wanaweza ku-challenge hii issue directly mahakamani kwa kudai kuwa kitu hakiwezi kuwa lawful kama hakijafuata procedure. Its that simple and its worth the shot kwa upande wa upinzani.
 
Ni kweli kabisa mkuu unachosema. ila hapa taabu itakuwa ni mpambano na system. Jana Kitiila alitoa comment yake moja kwenye mojawapo ya posts za jana akasema "System can be changed by the system". Kinachoweza kutoa possibility hizi ni pale tu ktakapokuwa na system mpya. Hapa tunagusia katiba na ndio maana naamini CHADEMA wanapigania kwa nguvu katiba kwa sababu that will be the only way to change the system.

Out of that itakuwa ni jitihada za bure maana hata hao tunadhani twaweza kwenda kwao (mahakama) ni wateule wa raisi. what do you think here?? Watakachofanya ni kutafuta mwanya wa kisheria na kikatiba (ambao naamini kwa katibu zetu na sheria zetu upo) ili kuhakikisha wanamtoa mkuu na kuendelea kuwa "mteule" wa Tanzania.

So kwa nchi yetu its only the change of consitution that guarantee the change of system and bring justice possible
 
Sisemi kuwa waache kudai katiba mpya. Ninachosema ni kuwa wanaweza kutumia hii kama moja ya njia za kudai na kumuengua kikwete.
 
Ahsante wakuu kwa taarifa.

Kwa lugha nyingine Slaa is a legitimate but not a legal president.
 
Nakubaliana na wana JF wengi kuwa kitu ambacho kinaweza kuwa mkombozi wa mtanzania, kidemokrasia ni katiba mpya ambayo itazingatia mazingira tuliyonayo, tunayoyaendea na maslai ya wengi!
 
Umesomeka mkuu. lazima tuwe makini na propaganda za CCM.

Ni kweli mkuu, propaganda kwa CCM ndio silaha yao kuu. Ila wanajua wazi ya kuwa kwa sasa hivi watanzania sio majuha tena.

Tukipiga kelele kila mahali watajua huu moto hauzimiki. Ni aibu kujikuta uko peke yako.

Waziri mkuu jana katoa kauli na wengi wanahisi propaganda zimeanza, lakini kama tutaamua kutoridhika na propaganda na kukaa kimya, bali tukaendelea na kupiga kelele kudai haki yetu ya msingi namba moja, japo kele za chura hazimsumbui mwenye nyumab kulala, safari hii itakuwa tofauti, akubali matakwa yetu au atoke akalale nje.

Kwa pamoja tutawezesha mambo haya
 
najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

msimamo wa chadema haujabadilika

by dr. Wilbrod slaa on tuesday, december 14, 2010 at 7:29pm

kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa tbc ilieleza wazi kuwa kamati kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na sekretariat ya chama kuwa chadema imekataa matokeo ya uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo kikwete's presidency ni lawful it is illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, kamati kuu ikasisitiza " kuundwa kwa tume huru" kuchunguza dosari " irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, chadema ni chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "haiko tayari kuingia ikulu kwa kumwaga damu ya watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa katiba na sheria mbovu kama tuliyonayo leo, chadema inasisitiza upatikanaji wa katiba mpya, shirikishi na ya wananchi.

Upatakanaji wa katiba hii utakuwa na mchakato, na kama serikali haitaki, basi chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi katiba ya wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na busara daima huvuta heri.

source: gonga hapa msimamo wa chadema haujabadilika | facebook

nyongeza: kuna thread imewekwa hapa chini na mwanajamii mmoja (chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (lawful na legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi

moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: Legitimate - google search

zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.

Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: Meaning and definitions — infoplease.com.

kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principles

tukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

sheria inasema raisi ni raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.

hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.

kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule georgia

georgiandaily.com - Opposition to picket

so what?
 
Nafarijika Sana Kuona watu wengi wamehamasika kudai Katiba.. Hii inaashiria kuwa 'Chama Cha Kudai Katiba' kimekusanya wanachama wengi kuliko hata wa CCM na CHADEMA. Na Hiki ndicho kinachohitajika. Ni jukumu letu wana JF Kuwaeleza hata wananchi wa CHINI ILI WAJUE UMUHIMU WA KUWA na Katiba mpya....Tuongee Lugha Moja!
 
Mkuu...sasa tatizo si ndo hapo. Huoni Chadema wanaweza ku-challenge hii issue directly mahakamani kwa kudai kuwa kitu hakiwezi kuwa lawful kama hakijafuata procedure. Its that simple and its worth the shot kwa upande wa upinzani.
Hakuna mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kitu kama hicho ; Tamko la tume juu ya matokeo ya Rais liko juu ya uwezo wa mahakama zetu ( Can not be challenged ...)
 
that is ur interpretation! For me challenge haina same meaning. kwa hiyo unataka kusema tume ingetangaza tu rais bila uchaguzi...mahakama zisingeweza kutatua?
 
Back
Top Bottom