Kwa chama tawala CCM baada ya uchaguzi kazi ni moja kupigana vikumbo kueelekea uchaguzi 2015!

Jan 16, 2007
721
176
Tumekua tukishuhudia kila kukicha katika vyombo vya habari minyukano na kupigana vikumbo ndani ya chama tawala CCM kuhusiana na mbio za uraisi 2015.Shughuli zote za kutatua kero za wananchi zimewekwa likizo,hakuna muda wa kuzishugulikia,kwani kwa chama tawala CCM na serikali kero za wananchi HAZIWAHUSU kutokana na mfumo waliojiwekea katika vipindi vya awamu mbili zilizopita.

Kwa utawala huu wa CCM kero kubwa ni kulinda matumbo yao na familia zao,kwa wale ambao hawatagombea nafasi za uongozi ni wakati wa kujiandalia kiinua mgongo kwa ufisadi zaidi na kwa wale wanaotegemea kuwania nafasi za uongozi ni wakati wa kukusanya pesa za ziada kwa ufisadi kwa ajiri ya kununua kura wakati wa uchaguzi ujao.

Kwani wengi bado wanaamini ya kua katika uchaguzi chini ya chama tawala CCM kinachohitajika ni fedha kunua shahada za wapiga kura,fulana,kangha vyakula,ahadi hewa n.k+wizi na kugushi kura.

Wengi bado wanaimani hiyo ingawa nadhani wanakosea.Kwa viongozi wa chama tawala CCM kujinadi kwa kutatua kero za wananchi
HAIWEZEKANI ,kwa sababu zifuatazo kwanza gharama yake ni kubwa na pesa za kutatua kero za wananchi zimeisha tafunwa kifisadi {HAITEKEREZEKI) Na muda hautoshi.

Pili kama katika uchaguzi wa 2010 kwa utamaduni wa chama tawala mgombea urais anagombea kwa vipindi viwili,kwa kipindi cha kwanza cha miaka 5 vikumbo na minyukano ilikua midogo na kama kwa kipindi hicho walishindwa kutatua kero nyingi za Wananchi itakua MIUJIZA AU UWENDAWAZIMUB kutegemea chama tawala CCM kitatue kero za wananchi katika kipindi hiki cha miaka 5.

Muda hautoshi kwa wanaomaliza muda wao kujitenezea viinua mgongo na kwa wanaotegemea kugombea kukusanya pesa kwa ajili ya kampeni zao.TUTENGEMEE MAISHA MAGUMU ZAIDI,ARI NGUMU ZAIDI!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
pole shemeji sijasoma kwa sababu ya kuichukia ccm.

na matatizo ya ccm kama ni mzazi mtoto hafai hata kuchapa ni kuuachia ulimwengu umpe bakora na bakora za ulimwengu si unajua hazikopeshi?

baadae shem.
 
chadema wao baada ya uchaguzi kazi
ni moja tu matokeo yalichakachuliwa na jk si rais halali hadi 2015
 
pinda kasema jana agenda ya urais 2015 sio ya ccm ni ya walafi wachache unataka kauli ipi au ya lowassa
 
vipo vyama baada ya uchaguzi kazi ni moja tu kuzunguka nchi nzima kwa kampeni ya kuing'oa ccm 2015 badala ya kushughulika na maendeleo ya wananchi
 
umesahau na wale ambao baada ya uchaguzi kazi ni moja kuandamana na kususa hadi 2015
 
wewe kibaraka wa ccm unalipwa sh ngapi kupost upupu huku?
mama porojo utabadili id mpaka uchoke lakini jibu ni moja ccm kwishney.
 
Shame on em...waliojawa na uchu wa madaraka kuliko uhai wa watu...tizama tunavyoangamia kwa kukosa huduma za msingi stahiki na kwa wakati...Wagonjwa wanakufa jamani kutaja wishes za hawa jamaa waliokua blinded na ambition ni dhihaka kwa wananchi!
 
Back
Top Bottom