Kwa Bomu Hili CCM 2015 Kazi mnayo

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,943
Nimekua nikizirekodi kauli na hotuba mbalimbali wanazozitoa wabunge wa CCM pamoja na viongozi wao. Na leo Bungeni ndo nimepata mambo mengi sana ambayo yataiua CCM kwa kasi zaidi 2015. Mwaka 2015 tutaziwakilisha kwa wananchi wazisikilize. Hapo sidhani kama bomu hili litawakosa
 
mambo yepi hayo umeyapata bungeni leo?walau kwa faida ya tusiopata fursa ya kufuatilia kikao cha bunge la 10 live? Tafadhali
 
Tuwekee machache mkuu na sisi tufaidike ambao hatukuwepo.....maana ndio itakuwa vizuri zaidi kuendelea kuchangia thread.
 
Tundu Lissu kaisoma barua bungeni inayoonyesha jinsi Andrew Chenge alivyonufaika na fedha za rada. Mathias Chikawe na Hawa Ghasia wanasema Lissu apeleke ushahidi. Akawajibu kuwa Serikali imepelekewa ushahidi. Ajabu wabunge wa CCM wamejibu sioooooooo.....
 
wanadai mishahara ya wafanyakazi na serikali ni siri yao haitakiwi kuwekwa wazi bungeni
 
Kweli haiingii akilini, wabunge wetu tena asilimia kubwa ni wasomi na wazazi wa taifa lijalo wanafanya maamuzi ya vitu vigumu na vikubwa kwa mzaha namna ile, eti wanaulizwa:

''wanaosema SIYO waseme NDIYOOO...wanajibu NDIYOOOO'', wanaulizwa tena ''wanaosema NDIYO waseme NDIYOOO....wanajibu NDIYOOO'' alafu spika anajumlisha kirahisi kabisa, ''haya waliosema NDIYO wameshinda'' na wao bila woga WANAPONGEZA kwa kupiga makofi. Kweli naamini vizazi vijavyo vitawahukumu kwa maamuzi yao.
 
Siku inakuja wabunge waadilifu watoke na hao wengine ije gharika iwasombe
 
Mimi binafsi naiona serikali ya Tanzania kama, ZEMBE, GOIGOI, YENYE WATU HAWAJAELIMIKA, ILA KWENYE DILI ZA WIZI WAMO. Hii ni kwa sababu wengi wao hawafikirii maendeleo ya tanzania baadae. Ni serikali ya Tanzania inapaswa kutafuta ushahidi uhusu CHENGE, na si mtu mwingine. Waziri gani aliye Mpuuzi namna hii, hii ni kukwepa majukumu, kuto kuwajibika, au kulindana. HUKU NI KUSOMA BILA KUELIMIKA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom