Kwa ambao hawajaoa, walimu ni wake wazuri...

mh kwa kigezo cha mtu mmoja?
kuna mdada mmoja ivi jaman mweupe anafundsha sheria yaani ana components zote za kuwa mama bora....SO NAWEZA NIKASEMA WANASHERIA WOOOOOOOTE NI WAMAMA WAZURI?
TABIA YA MTU HAIZINGATII FANI.NI INDVDUALY.
NB MUME/MKE BORA ATOKA KWA BWANA
Sikujua siku moja moja huwa unamwaga sera za kiroho. BTW digidigi hajambo?
 
Haka ka msemo kalimfanya bro wangu awe anashinda kanisani kusaka mke matokeo yake akaokota balaa akidahni mke mwema kumbe mama hafai kabisa alikuwa naye anasaka mume alivyofunga ndoa tu misukosuko ikaanza mama hatulii, kwa iyo bwana kupata mke mzuri zali tu likuangukie manake kwangu mimi ndoa ni kama kamari kuna kuliwa na kula hivyo ikitokea vyote poa tu...unajilipua kama kandahar.

Samahani mkuu, kuna tofauti ya kupata kitu kwa Mungu na kukipata kanisani. huyu bro wako hakumpata kwa Mungu huyo dada, bali alimpata kanisani. Angalia vizuri mama huyu naye alikuwa anasaka mume, kumbe wote walikuwa kwene mawindo, kwa hiyo walipokutana ikiwa hivo.

Kwa sababu hiyo basi tukubalieni kwamba wote walikuwa hawaombi/hawamwombi Mungu awape mwenza wao, Ila walikuwa wanashinda kanisani huku wakisubiri ni nani atasema anataka kunioa au nina nitakaemwambia nataka kuoa anikubalie.

Na hiyo ipo kabisa nataka kuoa Mlokole nikaa kwene kanisa fulani hata miaka miwili then nampata huko naoa. Nataka kuolewa na mlokole nashinda huko church akitokea naolewa.

Lakini mke/mume anayetoka kwa Mungu sio lazima atoke kanisani, wala Msikitini wala nyumba yoyote ya Ibada.
Hata muuza baa, kama huyo ndo mke wako uliyeandikiwa wakati ukifika Mungu anambadisha anakuwa mtu mwingine kabisa na unamuoa.

Wakati mwingine anaweza akawa anafanya kazi ktk mazingira magumu na hatarishi lakini kwa sababu wewe unaomba mke mwema Mungu anamlinda huko huko wala baya halimpati.

Njia Za Mungu sio kama Zetu na Mawazo yake sio kama yetu.
 
SWALI: Mke/mme asiye mwema anatoka kwa nani? Nadhani sio kusali tu kunamfanya mtu apate mke/mme mwema; kama ilivyo sahihi kuwa taaluma ya mtu pekee haimfanyi awe mwanandoa mzuri. Historia ndiyo inadhibitisha kuwa taaluma fulani wako hivi, kabila fulani wako vile, n.k
 
Samahani mkuu, naomba nijibu hivi. Hakuna mke mbaya wala mume mbaya.
ILa kila mtu ana mke wake na kila mtu ana mume wake.

Wanadamu hatupo sawa,tupo tofauti, kiroho,kimwili, nafsi, kiakili, na kila kitu.
Ambacho tunakikosea tunawachagua wenza ambao sio wa kwetu, hamatch/halandani na wewe, hawezi kuchukuliana na matakwa yako,
haendani na wewe ulivyo. ILa mtu huyo huyo angekaa na mwingine wangeendana vizuri tu, wangeweza kuchukuliana, kumaliza tofauti zao, kujaliana na mambo kama hayo.

Kwa maana hio sasa, huwezi kumpata mtu unae endana nae kama hujamshirikisha Mungu kwa asilimia zote. Kwa sababu moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu, siku zote. NItakubali kuolewa na ww coz nimechelewa kuolewa, naona una pesa na kazi so maisha yataendelea, unasali na unakwenda kanisani, nakuona mzuri wa rangi sura nk nk, unatoka kwene familia bora, ni bikra, hunywi pombe au sio mlevi.

Lakini nasahau haya, hivi huyu akikasirika naweza kuchukuliana na hio hali, hivi huyu akiwa na mastress naweza kuikabidhi hio hali au na mi nayaongezea mara mbili zaidi, hivi huyu mi nikikosea jambo ananisahihisha vipi, au yy akikosea anakubali je kosa na anachukua hatua gani nk nk nk nk nk

Maneno yanazidi kuwa mengi, lakini nahisi utakuwa umenipata walau kidogo.
Naishia hapo.
 
Mtoa mada hitimisha basi, kwa mtazamo wako umegundua nini kutoka kwa wachangiaji? Mimi kama mume wa Mwalimu aliyechagua kuwa Mwalimu kwa hiari yake, naamini taaluma ya ualimu kwake ni added advantage ya kuwa Mke bora sio mwema kama mnavyotaka iwe. Aidha tofauti na wa fani zingine at least ninao uhakika kwamba anayo nafasi pia ya kuwa mwalimu kwa watoto wake as anaingia ofisini saa 1.30 asubuhi na kurudi nyumbani saa 9.30. Na mengineyo mengi ambayo mwaweza kuongeza. Hata hivyo ni kwa Mwalimu aliyelimika akaelewa maadili ya taaluma yenyewe, saikolojia, filosofia na muhimu zaidi anayeelewa zana nzima ya ndoa. Hili mwisho ndilo linalowafanya na wa fani/kazi zingine kuwa bora hata kama sio Walimu. So Akili za taaluma changanya na za kwako. MY TAKE; MOST TEACHERS CAN BE GOOD WIVES>
 
uzuri wa mwalimu ni kwamba watoto wako watasoma, watahamasishwa kusoma sana shule, na watafika mbali kielimu...ila kwa habari zingine, hamna kitu, akili zao ni ngumu kuelewa, wana kiburu, na wanahitaji kuelekezwa vitu vilivyo vingi.
 
Hahahaha mkuu na wewe umeoa mwalimu?
 
Mnavyoongelea walimu ni wa level gani? Wa vyuo vikuu nao mnasemaje kama wanafaa kuwa wake na mama wema? Am just curious
 
Back
Top Bottom