Kwa ambao bado wana imani na pinda

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Nina maswali mawili tu kwa leo nilyoyatohoa kwenye gazeti la wiki hii la Mwanahalisi kwa wenye mapenzi bado na Mheshimiwa huyu ambae kwa maoni yangu naona kama vile heshima yake inaanza kushuka.

1. Ni kweli kwamba mheshimiwa huyu ni mmiliki wa mabasi ya Sumri? Maana taarifa zinasema hisa za Pinda zinamilikiwa kupitia kampuni ya One Move Transport.

2. Huko nyuma Pinda aliwahi kunukuliwa akisema hakuna kuiogopa Kagoda. Badae akanukuliwa akisema Kagoda ngumu. Kwa nini mkuu ana kauli mbili tofauti kwenye "inshu" moja???

Naomba kuwasilisha.
 
No news is good news!! If it is true we are heading to to heal.
 
Kama endapo atathibitika kuwa mmiliki wa hayo mabasi Unadhani nani atakaye mchukulia hatua?
Maana kuna usemi usemao Nyani haoni kundule. Au ambaye anajiona mtakatifu awe wa kwanza kumpiga yule mwanamke mzinzi.
In general ni kwamba ndani ya ccm hakuna mtu msafi, hata Magufuli ni walewale.
 
Inawezekana pia maana wafanyakazi wa hawa mabasi wana jeuri sijapata ona hata askari wanawaogopa, mfano, siku moja walitufanyia vurugu nikiwa nipo kwene NAJMUNISA pale mbezi mwisho cha kushangaza kufika maili moja kibaha wakashtaki wao kwa polisi na kuwashurutisha tuchukuliwe hatua la sivyo watatoa taarifa juu, hapo ndo nilichoka! ndo nikaskia jamaa wanasema hayo ni mabasi ya wakubwa plus kampuni ya ALLY'S BUS
 
Alipochaguliwa mara ya kwanza kuwa waziri mkuu alijiita mtoto wa mkulima, sasa hivi sijui anajiitaje???
 
Hakuna kitu pinda mtoto wa mkulima wapi ,si angekuwa sumbawanga akalime
 
Huyu ashatusaliti mazee so hatuna haja ya kumfunika nguo tena!!
mwogaaaaaaaaaa utadhani hatuja mpa ulinzi!!!!
 
Mtu hata akiwa mzuri vipi??? Akiwa ndani ya CCM ni useless!!!! Ni mfumo ndiyo unaofanya kazi na si mtu mmoja.... so provided Pinda is in CCM... is as good as nothing!!!
 
hata wewe tukikuchagua itakuwa hivyo,unadhana posho na mishahala zinaenda wapi kama kununua mabas au unataka awe anazileta kwako?
 
mzito kabwela kwani hujui mambo ya Chukua Chako Mapema, hawa jamaa hakuna mtu msafi hata mmoja sema tu watu wengine madhambi yao yamejificha. Mi naomba Mzee wa wikileaks afichue mazambi hata ya mawaziri.
waziri wabong anaweza kwenda ulaya kutembeza bakuli kwa niaba ya nchi nzima akirudi anajimiminia mwenyewe
 
kumbe ndo walewale halafu anajifunika ngozi ya mtoto wa mkulima!!!daah!kwahiyo kukataa Vx V8 ilikua zuga tu!shame on you Pinda.
 
Kama endapo atathibitika kuwa mmiliki wa hayo mabasi Unadhani nani atakaye mchukulia hatua?
Maana kuna usemi usemao Nyani haoni kundule. Au ambaye anajiona mtakatifu awe wa kwanza kumpiga yule mwanamke mzinzi.
In general ni kwamba ndani ya ccm hakuna mtu msafi, hata Magufuli ni walewale.

Sema kiufupi wana siasa hakuna mtu msafi, Slaa ( kuchukua wake za watu), Mbowe (madanguro)...........................
 
Nina maswali mawili tu kwa leo nilyoyatohoa kwenye gazeti la wiki hii la Mwanahalisi kwa wenye mapenzi bado na Mheshimiwa huyu ambae kwa maoni yangu naona kama vile heshima yake inaanza kushuka.

1. Ni kweli kwamba mheshimiwa huyu ni mmiliki wa mabasi ya Sumri? Maana taarifa zinasema hisa za Pinda zinamilikiwa kupitia kampuni ya One Move Transport.

2. Huko nyuma Pinda aliwahi kunukuliwa akisema hakuna kuiogopa Kagoda. Badae akanukuliwa akisema Kagoda ngumu. Kwa nini mkuu ana kauli mbili tofauti kwenye "inshu" moja???

Naomba kuwasilisha.

1.. SUMRY = Sumry + Pinda + Mama Mkwe wa Mkulu wa Kaya (Mbunge wa Kuteuliwa)!

2.. Kagoda : EL+RA walimketisha chini na kumpa onyo!
 
Kama endapo atathibitika kuwa mmiliki wa hayo mabasi Unadhani nani atakaye mchukulia hatua?
Maana kuna usemi usemao Nyani haoni kundule. Au ambaye anajiona mtakatifu awe wa kwanza kumpiga yule mwanamke mzinzi.
In general ni kwamba ndani ya ccm hakuna mtu msafi, hata Magufuli ni walewale.

Hakuna afadhali humo ndani wote ni walewale kwa rangi mbalimbali..
 
Natamani hii forum ingefungwa. Yaani imekaa kiumbeaumbea tu na kudhalilisha watu. Thread yenyewe inauliza swali lakini tayari watu wamesha mhukumu mzee wa watu. Napata tabu sana kuamini kama wachangiaji wengi humu wanafikiria wakiandikacho. Acheni kutakana watu na pia acheni kudhalilisha watu bila ushahidi. Inaudhi kwa kweli.
 
Back
Top Bottom