Kwa Akili Yangu ya Wanzuki Nikafumaniwa Mchana Kweupe...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
images

Nilikuwa nina kama miezi mitatu tangu kuoa kwangu. Ilikuwa ni Juni 2005. Mke wangu alikuwa akiniamini sana na hata wazazi wake, hasa mama yake, kwani alinifundisha shule ya msingi, wakati akiwa mwalimu. Mwaka huo wa 2005 alishastaafu.

Siku hiyo nilikuwa nyumbani na mke wangu alikuwa meenda kwao. Ilikuwa ni mapema bado, kama saa nane mchana, kwa hiyo sikutegemea angerudi wakati ule kwani tulikubaliana kwamba, angerudi jioni. Nilikuwa nimekaa sebuleni nikiangalia TV.

Mara simu yangu ikaita. Nilipunguza sauti ya TV hadi ziro na kupokea simu. Ilikuwa inatoka kwa msichana ambaye nilikuwa nimeanza uhusiano naye kama mwezi mmoja nyuma. Ukweli hadi leo najiuliza niliweza vipi kufanya jambo kama lile, kwani sikuwa kabisa mpenda wanawake na nilikuwa pia naheshimu ndoa yangu.

Nilipokea simu na kuanza kuzungumza naye. "Usijali mpenzi kesho nitakuona….. Nani, First Lady? Hana neno huyu na wala hawezi kunishtukia, kwani ananizimia sana. Nimemshika kwa kweli. Unajua nini, ulichelewa kidogo tu kujitokeza kwangu, lakini pale madhabahuni miezi mitatu iliyopita ungetakiwa kusimama wewe, siyo yeye……" Niliendelea kubwabwanya mwanaume na maneno yalikuwa yananitoka kama muimba taarabu wa mipasho.

"Lakini hata hivyo halijaharibika neno. Huku nimefungwa pingu za kanisani, lakini moyo wangu uko kwako mpenzi. Nakuhakikishia kwamba, nikiwa nawe, kila kitu kinabadilika, kinakuwa supa mwanawane. Naanza kumchoka wife, kwani hata nikiwa naye naiona sura yako kwake…………" Nilihisi nywele zimenisimama kisogoni ikabidi ninyamaze na kugeuka nyuma.

Nilishtuka kwa njia ambayo ingeweza hata kuniuwa kwa shinikizo.
Nilimwona mke wangu na mama yake wakiwa wamesimama. Nilijifaragua kutaka kuwakaribisha lakini walivyokuwa wananitazama, mwenyewe nilinywea, sauti ikakauka. "Ulikuwa naongea na nani?" mke wangu aliniuliza .

Nilibabaika kabla sijajibu……. "Ni …….ni… kuna jamaa yangu mmoja…." Sikumaliza kwani niliwashwa kibao cha maana shavuni na mke wangu.Halafu alinivaa na kunitupa chini. Nilikuwa sina nguvu kabisa, nilikuwa b.w.e.g.e hasa.

Kweli kufumaniwa ni kubaya.
Mama mkwe aliingilia kati kwa kuamua kumwondoa mwanaye ambaye alikuwa akinitandika kisawasawa pale chini. Wapangaji upande wa pili wa nyumba nao walifika na kutuamulia .Mama mkwe alimshika mkono bintiye na kumwambia, "twende, acha kila kitu humu ndani, usichukue chochote. Inatosha kwa haya tuliyoyaona."

Waliondoka na bintiye wakiniacha pale chini nikijizoa zoa na kusimama huku nikipepesuka.
Wapangaji wa nyumba upande wa pili walicheka kwa pamoja kicheko cha kebehi na kumalizia halo halooooo…..Walioneka wazi kufurahia dhahama ile, kwani tulikuwa tukiwasema sana mimi na mke wangu kwamba ndoa zao ni za kuunga kwa gundi.Najua mnataka kujua ilikuwaje baada ya pale………

Acheni umbea, fanyeni kazi……………


Lakini ngoja nikate kiu yenu ya umbea. Ni kwamba, baada ya pale, tuliyamaliza na mke wangu na alinisamehe baada ya kumweleza ukweli wote.

Kusema kweli tangu siku hiyo nimebadilika sana. Nikiona mwanamke nisiyemjua ananichekea chekea na kujipendekeza kwangu…….. nafunga viatu vizuri na kutimua mbio…………..LOL

Kuna watu najua wataninanga hapa kama nini…………………….!
 
mwanaume wa ukweli maishani mwako sharti ufumaniwe (angalao mara moja),sharti udaiwe (utaishije bila madeni?) na sharti ukumbwe na visanga (kufukuzwa kazi,kuibiwa,kudhulumiwa,kufumwa na hausgel etc),huo ndo uanaume na ukipitia visanga ndo unakomaa ati.
 
mwanaume wa ukweli maishani mwako sharti ufumaniwe (angalao mara moja),sharti udaiwe (utaishije bila madeni?) na sharti ukumbwe na visanga (kufukuzwa kazi,kuibiwa,kudhulumiwa,kufumwa na hausgel etc),huo ndo uanaume na ukipitia visanga ndo unakomaa ati.

duuu mkuu bishanga hahahahah!
 
mwanaume wa ukweli
maishani mwako sharti ufumaniwe (angalao mara moja),sharti udaiwe
(utaishije bila madeni?) na sharti ukumbwe na visanga (kufukuzwa
kazi,kuibiwa,kudhulumiwa,kufumwa na hausgel etc),huo ndo uanaume na
ukipitia visanga ndo unakomaa ati.

Aah! Nilikuwa sijaambiwa hili kwenye kitchen party.
 
HAYA masimu tena sana sana haya ya kichina yametuharibia sana ndoa zetu pamoja na kutupotezea uaminifu
ila mtambuzi ni kweli kichapo ulikisikia maana mm hata maumivu nisinge yasikia mbaya zaidi mama mkwe kashuhudia wapangaji nao. kama ni kweli basi mlihama pale hatakama kodi haijaisha kwani kila wapangaji wakikuona ungesilia

"heheheheeeeeeeeeee halooooooooooooooooooooo halo ya mtambuzi ndani ya fumanizi"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom