Kuzuia mkutano wa chadema iringa ni kuvuruga amani tena.

CAT5

Member
Aug 19, 2012
44
12
Wanajamvi kama ni viashiria vya kuvuruga amani ndani ya Nchi basi ni pale Jeshi la Polisi litakapo ingilia na kuvuruga makubaliano ya yao kufanyika mikutano ya CDM huko Iringa, binafsi sioni sababu ya kuzuia hiyo mikutano.
Kuongezwa kwa muda kwa zoezi la sensa hakumaanishi Watz wasifanye shughuri zingine na sidhani eti kuwepo kwa mikutano Nchini ndio chanzo mojawapo cha kutofanikisha zoezi hili hata pale muda wa nyongeza kwa zoezi lenyewe ulipotolewa.
Maelekezo yameishatolewa kwa wale wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuonana na makarani wa sensa wameishaelekezwa cha kufanya,sasa sioni kwa nini Polisi wa Iringa wapanie kusimamisha shughuri za Watz wengine kwa visingizio vya sensa?
Naomba kujuzwa kwa hilo?
Zoezi la sensa lina maana sana kwa Taifa,lakini pale ambapo hatuoni sababu ya kuingizwa vurugu kwa udhaifu wa maamuzi,ambapo karibu Watz wengi wameisha jiandikisha kwenye zoezi hilo.
 
Ningeshauri na CDM nayo ioneshe compromising spirit.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom