Kuzama majini

KAKA A TAIFA

JF-Expert Member
Apr 27, 2011
566
80
Mtu anapozama majini kwa muda kuanzia dakika 10 kuendela ni muda mrefu ambao unatosha kuzimia na hata kupoteza maisha.ni vizuri wakati wa kumwokoa mtu kama huyo kumlaza kifudufudi.angalia kwenye kinywa kama kuna kitu/vitu vilivyoingia vinavyoweza kumzibia kupata hewa,kama hapumui inamaana kazidiwa,funga pua na umsaidie kumpulizia hewa kama vile unavyopumua yaani kwa nafasi,mlaze kichwa kikiangalia juu.Mtizame kama mapigo ya moyo yanakpiga vizuri,mfunike na kitambaa kizito kwani atakuwa amepatabaridi kali.WAKATI HUO UWE UMEWAFAHAMISHA WATU WA HUDUMA YA KWANZA NA APATIWE MATIBABU HOSPITALI HARAKA.KWA KUZAMA ANATHIRIKA KWA MAPAFU KUINGIA MAJI HIVYO KUMKOSESHA HEWA YA KUTOSHA.KUZUIA MOYO KUFANYA KAZI YAKE VIZURI KWA KUGANDAMIZWA NA MAPAFU.PIA KWA KUKOSA HEWA YA KUTOSHA UBONGO UNAATHIRIKA SANA NA HUWEZA KULETA ULEMAVU WA KUTOWEZA KUONGEA ,KUSIKIA,KUTEMBEA NK.TUWE MAKINI HASA KWA WATOTO WANAPOKWENDA KUOGELA ,SEHEMU ZENYE MAJI,MADIMBWI ILI TUEPUSHE MATATIZO NA VIFO VYA KULAZIMISHWA
 

Attachments

  • KUZAMA-1.jpg
    KUZAMA-1.jpg
    62.8 KB · Views: 108
  • KUZAMA-11.jpg
    KUZAMA-11.jpg
    51.5 KB · Views: 101
  • KUZAMA-111.jpg
    KUZAMA-111.jpg
    70.6 KB · Views: 97
Back
Top Bottom