Kuwepo tu hisia ya kuwa mke wa Kaizari alikua akisaliti ndoa yake kulitosha kumtalik

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Tangu ibainike ya kuwa rais mstaafu B.W.Mkapa alitumia ikulu kuendeleza biashara yake, hadhi ya ofisi hiyo machoni mwa baadhi ya raia imeshuka sana kiasi kwamba hivi sasa limekuwa jambo la kawaida kwa rais aliyoko madarakani kushukiwa ya kuwa hata yeye anashiriki katika vitendo vya hujuma kwa nchi yetu. Kwangu mimi hiyo ni hali ya hatari; hatuna budi tuelewe kwamba, rais kama taasisi ndicho kielelezo na kioo cha taifa letu. Hivyo tendo lolote linalo dhalilisha hadhi ya taasisi hiyo alipashwi kuchukuliwa kimzaa mzaa tu. Ni kwasababu hiyo, mimi naaminiya kuwa kauli aliyo itoa rais Kikwete kuikana Dowans haitoshi; kuna haja ya kuunda tume ndogo kuchunguza ni nini chimbuko la msururu wa tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa rais.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom