Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Nakubaliana na mtoa mada, maana mimi kuna mpumbavu mmoja mpaka jana alinipigia kuniambia kuwa yeye anatoka TRA na kwamba anataka kuja kuniona au mimi nimtafuta kwa wakati wangu, kila nikimuuliza uko TRA jengo gani yeey kunijibu hataki, kiduka chenyewe hata miliona kumi hakifiki anataka kunitisha, mimi nishamwambia SIDANGANYIKI:dance::dance::dance::dance:
 
........Matapeli wanawapigia simu za kuwatisha wafanyakazi wa Serikali kwamba wao ni maofisa usalama wa taifa na wameona mafaili yao ni machafu hivyo wanashawishi wawasaidie ili wayasafishe kwa kuwahonga.......

Mbinu ya kizanamani sana. Ilibuniwa na kutumiwa sana na Edgar Hoover, Mkurugenzi wa FBI aliyekalia kiti hiki kwa muda mrefu zaidi kuliko mwingine yeyote yule. Kila ilipoelekea kukumbushwa kustaafu, yeye alikuwa anawa time na kuwa-blackmail wahusika kwa kuwaeleza kuwa alikuwa anapitia mafile yao siku chache na amebaini machafu mengi. Kwa kuogopa kuumbuliwa wakuu wake walikuwa wanagwaya kumstaafisha.
 
Wadau kuna utapeli mpya ambao unafanana na blackmailing kwa wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara na watu wengine.

Matapeli wanawapigia simu za kuwatisha wafanyakazi wa Serikali kwamba wao ni maofisa usalama wa taifa na wameona mafaili yao ni machafu hivyo wanashawishi wawasaidie ili wayasafishe kwa kuwahonga.

Wafanyabiashara wanatishwa kwamba wanakwepa kulipa kodi na wakigundua una fedha wanaweza kukuteka.

Huo ni utapeli wa kizamani, ukipigiwa simu na kuambiwa kuwa faili lako ni chafu so what? Wanaopigiwa simu hizo wanashindwa nini kuwajibu watu hao kuwa utaratibu huo wakupigia watu simu kuwaeleza mambo ya kiofisi ambayo ni confidencial umeanza lini?
 
Mbinu ya kizanamani sana. Ilibuniwa na kutumiwa sana na Edgar Hoover, Mkurugenzi wa FBI aliyekalia kiti hiki kwa muda mrefu zaidi kuliko mwingine yeyote yule. Kila ilipoelekea kukumbushwa kustaafu, yeye alikuwa anawa time na kuwa-blackmail wahusika kwa kuwaeleza kuwa alikuwa anapitia mafile yao siku chache na amebaini machafu mengi. Kwa kuogopa kuumbuliwa wakuu wake walikuwa wanagwaya kumstaafisha.

Eric, J Edgar Hoover alikuwa nayo hasa mafile yao ya kiukweli, alikuwa hadanganyi maana akikusanya taarifa zao ambazo akizitumia kwa kuwablackmail na hasa akina Kennedy. Tafauti na hawa wa kwetu wanakupigia simu kichwa mchungwa tu.
 
Wakikudai hela waambie waje wachukue kisha unawafungashia OMO ya kwenda kusafishia hayo mafaili
 
Hii nzuri sana.
Sasa kama wewe ni mfanyakazi wa serikali mtu akakupigia simu akakwambia ana faili lako chafu na wewe ni msafi unaogopa nini?

kama wewe ni mfanyabiashara mtu anakupigia simu anakwambia unakwepa kodi wakati wewe ni msafi unaogopa nini?

Mimi naona hao matapeli waaendelee kuwepo tu.

Tanzania hakuna mfanyabiashara (acha wachuuzi) aliye msafi, lazima anakwepa kodi ama atachakachua mzigo au huduma ili amaximize faida.
Vivyo hivyo na watumishi wa serikalini, lazima wakutoe kitu kidogo ili upate huduma. Kama huamini nenda katake huduma kwa mtumishi wa umma kisha umtazame usoni, utaona macho yanaomba pesa japo mdomo umefumba!
 
hao jamaa inawezekana kweli wana wajua wanao wapigia simu kuwa ni wachafu na kweli wana data zote na ndio maana inakuwa raisi kupewa pesa, kamwe hawawezi kkumpigia mtu safi samu
 
hao jamaa inawezekana kweli wana wajua wanao wapigia simu kuwa ni wachafu na kweli wana data zote na ndio maana inakuwa raisi kupewa pesa, kamwe hawawezi kkumpigia mtu safi samu
Ni Jerry Moro "amefufuka" nini? Kwa sababu ndio zake hizi...
 
Wana JF, mchana huu nimepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Mr Makombe wa WFP Kigoma na akanieleza kwamba kuna opportunity ya kupata pesa kwa ku-supply madawa ya kunyunyizia nafaka huko WFP Kigoma. Akasema kama niko tayari aniunganishe na bosi wake mzungu, kwa upande mmoja na muuzaji wa hayo madawa. Akazidi kuniambia kwamba yeye hataki kuwasiliana na muuzajio kwani walikorofisha mara ya mwisho - yeye Makombe hakupata mgao wake.

Nikamwambia sawa. Akanipa namba 0717289138 ya muuzaji dr Peter na nilipompigia huyu dr akadai anayo madawa aina ya damoline iliyotengenezwa sweden na anayauza kwa dola 3600 kwa pair moja. Mara nikapigiwa na huyo mzungu aliyesema kafikia Golden Tulip akitaka pair 50 na nimpelekee sample kwanza na akiridhika na ubora wake tutaandikiana mkataba ndipo nimletee pair hamsini kwa bei ya dola 4400 kwa pair (hii ndo bei ambayo mr makombe alisema nimtajie huyo bosi wake mzungu wa wfp!

Kwa kuwa nilikwisha soma katika magazeti fulani juu ya utapeli wa aina hiyo niliamua kuwapigia na kuwambia waache utapeli na wizi utawafikisha pabay. Kusikia hivyo wakakata simu. Kwa tahadhari simu wanazotumia kwa leo ni: 0752565642 na hiyo hapo juu.

Wanachofanya ni kwamba ukikubali dili ukaenda kwa dr ambaye ni mwenzao ukalipa dola 3600 ndo umeliwa hapo - wanazima simu na hutosikia cha mzungu wala nini.
Chukueni tahadhari
 
Back
Top Bottom