Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 10,037
- 12,509
Hello JF, Sijui ni kwangu peke yangu au ni kwa wengi.
Katika kazi nyingi nilizo APPLY online kwa mtandao wa ZOOM, BAADA ya siku chache tu unapata meseji kutoka kwa mtu mmoja, tena kwa kujirudia katika kazi tofauti tofauti, akisema yeye ni mmoja wa wanao shortlist applicants kwa kutumia CV zilizotumwa na kwamba yuko tayari kukusaidia kupata kazi hiyo kwa masharti, utampa kiasi kadhaa katika mshahara wako wa kwanza (anakutajia kiasi chake), ila umtumie kiasi fulani kwanza kwa no yake ifikapo jioni siku hiyo ili aweze kukupa maswali ya enterview.
Imenitokea hivyo kwa kazi 3 tofauti, moja ni shule, nyingine ni NGO na nyingine ni Kampuni; ila anayenitumia msg ni mmoja tu huyohuyo. no 0719 734458. Sijui ni nani? nilipo mwuliza yeye ni nani katika hayo mashirika yote matatu,,,, duh aliniporomoshea matusi mengi sana, nikaachana nae.
Haya kazi kwenu, usiamini kirahisi kazo za Zoom, bora kuwacheki wenye kazi kwa mtandao ili uone uhalisi wa kazi husika, badala ya kutuma Cv online.
Na huu utapeli umejenga kiburi sana kwa vijana kwani hawataki kabisa kujiweka sawa kwa interview wanategemea dili. Vijana wengi cv mbovu na hawataki kujifunza wanawategemea matapeli.