Kuweni makini na nafasi zinazotangazwa na ZOOM, kuna utapeli

Ahsante ndugu. Nawashauri ukiona mtu amekutext ishu za hela hata kama anajitambulisha kuwa anatoka kampuni kubwa futa futa kabisa. Ukiendelea naye atakutapeli. Ni wazi kuwa kuna ambao wameshatapeliwa, ila cha msingi anza ukurasa mpya wa kutotapeliwa tena" Jiamini kuwa utapata kazi au opportunity". Ndugu mtumiaji na ambao sio watumiaji wa jfasta.com, nawaalika wote kufatilia matangazo yetu ya kazi kila siku kupitia Jfasta.com | Ultimate fast information portal in East Africa| Get updated Job Opportunity & More. Kama unatatizo lolote kuhusiana na kuangalia na kutuma maombi katika kazi zinazorushwa kwenye mtandao wetu tupigie simu:+255 714 992 972 au tutumie ujumbe: info@jfasta.com

Pia kama una maoni juu ya maboresho tutumie ujumbe wako:
 
Habari,

Tunashukuru kwa kuona maoni yenu kuhusu Zoomtanzania.com. Kwanza napenda kuwatoa hofu na kuwahakikishia kuwa Nafasi za kazi tunazozitangaza ni za ukweli na nyingi huwa wanaotangaza ni waajiri wenyewe na recruiting agencies. Na kuna watu wengi wanafanikiwa kupata kazi kupitia zoomtanzania.
Zoomtanzania.com ni website inayowapa fursa watumiaji wake kuomba na kutangaza kazi bure. (post and apply for free). Hataivyo kuna watu wachache wanatumia vibaya fursa hiyo kwa kutangaza kazi za uongo au kutapeli watu. Zoomtanzania inalipa uzito swala hili na kuchukua hatua za kisheria kwasababu watu kama hawa wanachafua jina la Zoom na hadi sasa tumeshafanya mawasiliano na vyombo vya sheria husika katika kutatua hili swala.
Hataivyo tunawasihi watumiaji wa Zoomtanzania kutokubali kutoa pesa au kutuma pesa ili kupata ajira kupitia matangazo ya zoomtanzania kwa njia yeyote ile. Tunawaomba kusoma kipengele chetu cha terms of use chenye link ifuatayo

ZoomTanzania | Terms of Use. kuna kipengele d,g,i,j. vinaweka wazi kabisa kuhusiana na matumizi kwa watumiaji wetu

Zoomtanzania
 
Hello JF, Sijui ni kwangu peke yangu au ni kwa wengi.

Katika kazi nyingi nilizo APPLY online kwa mtandao wa ZOOM, BAADA ya siku chache tu unapata meseji kutoka kwa mtu mmoja, tena kwa kujirudia katika kazi tofauti tofauti, akisema yeye ni mmoja wa wanao shortlist applicants kwa kutumia CV zilizotumwa na kwamba yuko tayari kukusaidia kupata kazi hiyo kwa masharti, utampa kiasi kadhaa katika mshahara wako wa kwanza (anakutajia kiasi chake), ila umtumie kiasi fulani kwanza kwa no yake ifikapo jioni siku hiyo ili aweze kukupa maswali ya enterview.

Imenitokea hivyo kwa kazi 3 tofauti, moja ni shule, nyingine ni NGO na nyingine ni Kampuni; ila anayenitumia msg ni mmoja tu huyohuyo. no 0719 734458. Sijui ni nani? nilipo mwuliza yeye ni nani katika hayo mashirika yote matatu,,,, duh aliniporomoshea matusi mengi sana, nikaachana nae.

Haya kazi kwenu, usiamini kirahisi kazo za Zoom, bora kuwacheki wenye kazi kwa mtandao ili uone uhalisi wa kazi husika, badala ya kutuma Cv online.
 
Jinale limeandikwa Stephen Maganga kwa kutumia tiGO PESA
 
Mimi hiyo no ilinipigia nikapotezea baada yakuniambia eti tufanye dili na Hr, niitwe kwenye interview.
 
Unapoona tangazo la kazi fuatilia kwenye kampuni husika,tafuta kama kuna website yao pata contacts wasiliana nao kujua kama ni kweli kuna nafasi ulizoziona.Kitu kingine muwe mnaangalia hata tangazo lilivyokaa,mbona matangazo mengine yanajionyesha kabisa kwamba hilo kampuni inawezekana ni dogo au hawajui wanachokifanya au ni matapeli.
Usipende kutoa details zako kwa vikampuni ambavyo hata hujawahi kuvisikia,fuatilia kwanza ujue kama vipo au la.
Angalia hapa chini

"XYZ technologies services in searching for an I.T. officer to join our team of professionals.must be a diploma or degree holder, both experienced and new graduates are welcome to apply "
Nimebadili jina lakini la kampuni,lakini ukiangalia hilo tangazo kuanzia lugha ilivyo,uvivu wa kuandaa kwa makini,then hizi kazi ambazo hata job descripton hazina muwe nazo makini.Tapeli kama hajazikopi sehemu hawezi kuzitengeneza mwenyewe.Sijasema hilo kampuni halipo ila ninaona mapungufu na siwezi kuomba kazi huko.
 
Unapoona tangazo la kazi fuatilia kwenye kampuni husika,tafuta kama kuna website yao pata contacts wasiliana nao kujua kama ni kweli kuna nafasi ulizoziona.Kitu kingine muwe mnaangalia hata tangazo lilivyokaa,mbona matangazo mengine yanajionyesha kabisa kwamba hilo kampuni inawezekana ni dogo au hawajui wanachokifanya au ni matapeli.
Usipende kutoa details zako kwa vikampuni ambavyo hata hujawahi kuvisikia,fuatilia kwanza ujue kama vipo au la.

Hili nalo neno....mi nlishawahi kuona tangazo la kazi zoom nikaifuatilia kwenye website ya shirika husika sikuona chochote ila nliapply hivyohivyo.....nimejifunza
 
Nakumbuka kuna siku nliona message ikisambazwa kwenye group moja la whatsapp kuhusu huyo mtu kuwa ni tapeli..Jina lake si geni ntafuatilia then ntaileta hiyo message
 
Jinale limeandikwa Stephen Maganga kwa kutumia tiGO PESA

huyo stephen nae alinitumia msg anataka nimrushie 35000 kwa tigopesa anadai anafanya kazi RAITH NGO, haki ya nani nilimtukana sana aisee
 
huyo stephen nae alinitumia msg anataka nimrushie 35000 kwa tigopesa anadai anafanya kazi RAITH NGO, haki ya nani nilimtukana sana aisee

Hiyo 35 si bora tukale bia tutakate, au wasemaje Mtende?
 
Last edited by a moderator:
Iwe ni ZOOM au sehemu nyingine yoyote,unayoapply kazi,ukiombwa rushwa eti ndo upate kazi achana nao maana utaliwa tu!
 
huyo stephen nae alinitumia msg anataka nimrushie 35000 kwa tigopesa anadai anafanya kazi RAITH NGO, haki ya nani nilimtukana sana aisee
Kampuni ya tigo hawajui tu lakini kwangu naona kuna udhaifu,ukiangalia utakuta matapeli wengi wanatumia tigopesa ,kwa nini hawatumii M-pesa kutapeli watu?Voda hawana mchezo na mambo ya fraud.Tigo mnahitaji kulinda heshima yenu ,mtandao wenu unapotumiwa na matapeli wakati information zote mnazo na mnaweza fanya chochote ikiwemo kublock au kufreeze asiweze kutoa hizo pesa lakini ,mpo tu.
 
Kweli watu wana athirika na haya matapeli. Mimi bado nalia na jingine No. 0753162892- SHOMARI MHUNZI, Ni tapeli mambo ya magari ya minada, Tusaidiane kwa anaye mfahamu huyu, au ashawahi sikia habari zake. Amenitenda sana wandugu, sema hapatikani tena kwa simu hii.
 
Kampuni ya tigo hawajui tu lakini kwangu naona kuna udhaifu,ukiangalia utakuta matapeli wengi wanatumia tigopesa ,kwa nini hawatumii M-pesa kutapeli watu?Voda hawana mchezo na mambo ya fraud.Tigo mnahitaji kulinda heshima yenu ,mtandao wenu unapotumiwa na matapeli wakati information zote mnazo na mnaweza fanya chochote ikiwemo kublock au kufreeze asiweze kutoa hizo pesa lakini ,mpo tu.

nadhani huumchezo utakua unaanzia ndani ya management maana malalamiko ni mengi na ni ya muda mrefu ila cha kushangaza hakuna hatua inayochukuliwa
 
Ushauri wa bure ulimpa, teh teh! Na jinsi watu walivyokuwa na shida na uoga wa ajira wanaingia mkenge... Jamaa yangu juzi kati kapigwa Laki mbili.

Naye zilimuwasha tu hzo kilo 2, yani ana uwezo wa kufight laki mbili kumpa tapeli anashindwa kukoroga kichwa kubuni business?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom