Kuweni makini na facebook

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
6,130
6,963
Wakuu kuna kisa cha ukweli mke wa rafiki yangu kalala na mwanaume amekutana nae facebook tena kwa aibu kubwa mana wameanza kuchat ndani ya mwezi mmoja tayari wakasex na kibaya zaidi huyu demu mke wa rafiki yangu alikua na mimba ya miezi 5!!!...kiukweli huyu dada kafanya tukio la aibu sana mana hata mume wake anashindwa kumwelewa mtu mzima kuwa na tabia chafu kiasi hiki...

Ukiangalia watu walioko Facebook hakuna kitu cha maana wanachoweza kujadili kwa maana ya Issues!!! pale watu wanaandika pumba tu mara nimechoka,naumwa,nina hasira na mambo mengine meengi ya kienyeji..

kama mkeo ama mumeo yuko facebook kuwa makini sana...
 
Kama mtu hajiheshimu na hayuko committed hata kanisani wanaweza wakakutana na wakafanya uzinzi....facebook is a very useful media na ina manufaa mengi....huwezi judge facebook kwa event ya mpumbavu mmoja....wapo waliokutana facebook na wameoana na wapo waliopata business networks,information za vitu tofauti via facebook....ni jinsi mtu anavyoitumia....personally marafiki zangu wanaitumia vizuri na nafurahi na kujifunza kitu everytime nafungua facebook.....

Na ulivyosema kama mkeo yuko facebook kuwa makini,huyo mwanamke alifanya huo uzinzi na mwanamke mwenzie?unachojaribu kusema hapa ni kuwa wanawake hawana uwezo wa kuji-control,so kuwa facebook ni rahisi kwao kudanganyika? huyo mwanamke ni mtu mzima na angeweza kufanya uamuzi tofauti na huo,kwa tamaa zake au kwa akili zake aliamua kufanya hayo...it has got nothing to do with yeye kuwa mwanamke.
 
Acha kugeneralise watu na tabia zao!Mi nawajua watu facebook wanaoongea mambo ya maana!Na hata hayo ya kusema naumwa..nimechoka kama yana umuhimu kwao kwanini wewe useme ni ujinga!Na mtu kusema naumwa..nnahasira vinahusiana vipi na mtu kua na tabia chafu!Huyo dada hata isingekua fb bado angeweza kufanya madudu yake kwasababu ndivyo alivyo!Acheni kusingizia fb kwa tabia binafsi kama mnavyomsingiziaga shetani!Hata angekua hapa JF angeweza kupata hapahapa na akafanya hayo hayo!
 
Si wote wanaongea upuuzi kwenye face book. Mimi niko face book na ninaconnect na watu ninaowafahamu na wenye heshima zao kwani they are my friends. I don't expect any of them to write rubbish. Sasa huyo wife inawezekana ni teenager. Hata asingekuwa facebook angecheat tu. Na inawezekana hata hiyo mimba si ya jamaa. Sijawahi sikia mja mzito anatoka nje ya ndoa.

Nakubali kabisa wanafunzi na teenagers kwa ujumla wana misuse facebook. Ushauri wangu "dont connect na watu usowajua kwenye facebook wanaweza wakaandia upuuzi kwenye wall yako ukapata aibu"
 
Kama mtu hajiheshimu na hayuko committed hata kanisani wanaweza wakakutana na wakafanya uzinzi....facebook is a very useful media na ina manufaa mengi....huwezi judge facebook kwa event ya mpumbavu mmoja....wapo waliokutana facebook na wameoana na wapo waliopata business networks,information za vitu tofauti via facebook....ni jinsi mtu anavyoitumia....personally marafiki zangu wanaitumia vizuri na nafurahi na kujifunza kitu everytime nafungua facebook.....

Na ulivyosema kama mkeo yuko facebook kuwa makini,huyo mwanamke alifanya huo uzinzi na mwanamke mwenzie?unachojaribu kusema hapa ni kuwa wanawake hawana uwezo wa kuji-control,so kuwa facebook ni rahisi kwao kudanganyika? huyo mwanamke ni mtu mzima na angeweza kufanya uamuzi tofauti na huo,kwa tamaa zake au kwa akili zake aliamua kufanya hayo...it has got nothing to do with yeye kuwa mwanamke.

The Following User Thanked You Michelle For This Useful Post:

Mr. Cool(Today)


hehe hii temporary solution nimeipenda
 
Hivi kile kitufe cha Thanks kimeondolewa!? Tangu jana sikioni au ni kwangu tu?. Samahani kwa kutoka nje ya mada.
 
Michelle rudia kusoma vizuri nilichoandika,maana unanishambulia kama nimesema wanawaje tu.!!!! nimesema wenye waume na wake walioko fb nkuweni makini hili limemtokea rafiki yangu na he is down kwa kweli sijalenga jinsia ya mtu hapa ww unaongea as if mm nimesema hilo kwa jinsia ya kike sio sawa ndugu!!!
 
Huku ni wana JF ss FB inatafuta nn katupe au post huko kwenye FB yenu huku tunajadili mambo ya maana jamani hebu Model tafadhali ondoa hii tuna mambo mengi ya kujadili huku plzzzzzzz!
 
Biashara zangu zote, natangaza Facebook.

Wateja wengi napata huko. Ile ni DUNIA ndugu yetu na huko kama ilivyo duniani, kuna kila Mabaya na Mazuri.

Cha muhimu na kutumia kwa uangalifu. Hata maji yanauwa ingawa MAJI NI UHAI.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa ujumla mambo ya mahusiano, uzinzi, na uzinifu hayajasalimika na mapinduzi yaliyoletwa na maendeleo ya dotcom. Siku hizi ni rahisi sana kuchiti na unaweza kuchiti bila mwenzio kujua au kuhisi kuwa unachiti.

Unaweza uka hook up na mtu aliye mbali na wewe. Mkapanga mambo mengi sana. Mkapanga mkutane wapi na lini. Mnaweza mkanunua tiketi zenu za ndege kupitia mtandaoni. Mkabook na hata chumba cha hoteli kupitia mtandao. Mtu unaweza ukawa na email accounts kibao kila moja ikiwa na dhumuni lake. Na hata kama umeoa au kuolewa bado unaweza kufanya haya yote bila mwenzio kujua na huyo mwenzio akabaki kujua wewe u mwaminifu kwake kumbe wapi.

Siku hizi kuna hadi tovuti za kutafutia infidelity. Yaani wote mnaokuwa wanachama wa hiyo tovuti na kwa ujumla hali zenu na malengo yenu yanakuwa yamefanana. Wote mnakuwa mko kwenye ndoa na wote mnakuwa mnatafuta infidelity kwa siri. Mkikutana huko na kuongea na kukubaliana yanayofuata ni kitu na boksi.

Kwa hiyo kwa ujumla mtandao (iwe facebook, twitter, gmail, yahoo, JF, n.k.) umekuwa kiungo muhimu sana katika kurahisisha uzinzi wa watu. Inasikitisha lakini ndo ukweli wenyewe huo.
 
Huyo ana tabia ya uhuni,tofauti na hapo tuangalie upande wa rafiki yako kama alikuwa anawajibika ipasavyo.
 
uyo alitaka mwenyewe kumengwa inaonyesha alizimika na photo za huyo shalobaro ndo mana kamengwa hii inaonyesha waz kuwa huyo mwanamke hajieshimu hata kama angekuwa huku jamii forums bado angemengwa kwan angetokea mjanja akaandika comment akaipenda akamtokea kwny PM bado angemengwa hvyo tatzo co fb bal ni yeye mwenyewe huyo mwanamke hajiheshmu
 
Jamani tusimshambulie huyu bwana kwa kusema hilo alosema, FB, JF, DHW, Marafiki siyo sehemu ya kuendekeza jamani. Humu ndani ningekuwa kiwembe ningeshawanyonyoa mtu kibao, nashukuru Mungu sana nina hofu na Mungu.

Ki ukweli unakuta mtu ana stress zake ameudhiana na mke/mume akifika hapa akakutana na mtu anampa faraja kwa maneno bila hata kumjua anatamani angekutana nae akamaliza hasira zake. Hiyo nimeona FB, si hivyo tu watu wanatumia vibaya hiizi media

Tuweni makini sana wenye waume na wake tuombe Mungu wetu atutie nguvu, wenye BF/GF anzaneni kuanua vilago vyenu maana hamna hati miliki yeyote aweza kumiliki.

Tuombe Mungu kwamba watu JF hawana hiyo tabia ni Great thinkers ila walio face book ni some of them ni vibaka. SAMAHANI kwa kusema hayo but there is reality.

Nawasilisha.
 
Du ndugu yangu usilaumu sisi watu wa facebook, huyo mwanamke akija hapa Jf bado atajilengesha tu wamchakachue tena huku ni watu wa hatari zaidi.
Mahusiano ni popote tu iwe Vyuoni, JKT, Mpirani Maofisini Sokoni yaani popote penye jinsia mbili tofauti mapenzi yanamea wawe wameoa/wameolewa wanaweza yaanzisha inachotakiwa kaliba (uvumilivu wa kuzuia misuli yetu isiamke ovyo)
 
Back
Top Bottom