Kuweni makini na bidhaa za WESTPOINT

Kagosaki

JF-Expert Member
Feb 11, 2010
208
56
Jamani napenda kuwatahadharisha kwamba muwe makini sana na bidha zinazotengenezwa na kampuni ya WESTPOINT.

Nilinunua fridge mpya hivi karibuni Quality Plaza. Baada ya wiki moja ikaharibika pamoja na kuwa na fridge guard. Nikaipeleka service, baada ya wiki moja ikaharibika tena.

Kwenye service bay ya kwao, nilikutana na watu wengi akiwemo mama mmoja alienunua jiko la umeme. Alipofika nyumbani kwake na kulichomeka, lilimrusha vibaya na kuzima umeme nyumba nzima.

Wengine walinunua vifaa vingine na kupata matatizo ndani ya wiki mbili. Nendeni mkajionee wenyewe pale service bay yao iliyoko jengo la blue kwenye makutano ya barabara ya kurasini na nyerere road, opposite Pegasus house.

Sijui kama TBS wanafanya kazi yao vizuri....
 
thax kwa info mkuu
kuna kitu nilitaka kufata pale this wkend
kumbeeee????????/
 
Hao halafu wana warant fake na ni wasumbufu sana uananunua kitu siku mbili kimeharibika halafu wanakwambia ubebe jiko lako toka huko madongo poromoka off Dar town kwa ghalama zako uwaletee kalakana yao kariakoo hovyoooooo kabisaaaaa!
 
mimi Mbona nimenunua fridge na Brenda huu mwez wa 9 Mbona havisumbui?Kwan haukupewa warrant?au umenunu Kwa mtu
 
Kweli walinisumbua sana hata mimi na wana secretary pale anaitwa Mariam ambae nimsumbufu sana! Unanunua bidhaa halafu unaingia gharama za kuwaletea tena kwenye karakana yao pale Kariakoo! Wapumbafu!
 
Karatta, kwani Quality Plaza si kuna supermarket pale? Nilinunua kwenye supermarket na nikapewa warranty lakini wateja wengine niliokutana nao kwenye karakana yao kila mmoja alikuwa analalamika juu ya bidhaa za WESTPOINT. Ni kama fake products...Halafu unaingia tena gharama kuleta fridge kutoka uliko hadi kwenye karakana yao!
 
Mmmh, isije kuwa ni probaganda za kibiashara ambazo hazijafanyiwa utafiti...kwanza pole kwa yaliyokukuta!
Lakini ushuhuda wangu ni tofauti, mi friji langu lipo bomba mwanzo mwisho, toka nimeliwasha mwaka juzi, huwa linapumzishwa
na mgao wa TANESCO tu.

Ni vizuri kuwa mwangalifu kwenye kila kitu unapotumia hela, si kwenye bidhaa za WESTPOINT tu.
 
Karatta, kwani Quality Plaza si kuna supermarket pale? Nilinunua kwenye supermarket na nikapewa warranty lakini wateja wengine niliokutana nao kwenye karakana yao kila mmoja alikuwa analalamika juu ya bidhaa za WESTPOINT. Ni kama fake products...Halafu unaingia tena gharama kuleta fridge kutoka uliko hadi kwenye karakana yao!

Mmmh, isije kuwa ni probaganda za kibiashara ambazo hazijafanyiwa utafiti...kwanza pole kwa yaliyokukuta!
Lakini ushuhuda wangu ni tofauti, mi friji langu lipo bomba mwanzo mwisho, toka nimeliwasha mwaka juzi, huwa linapumzishwa
na mgao wa TANESCO tu.

Ni vizuri kuwa mwangalifu kwenye kila kitu unapotumia hela, si kwenye bidhaa za WESTPOINT tu.



Nafikiri kuna wajanja wameingilia products za hawa watu. Nyumbani kwangu tuna friji ya Westpoint tuliyopewa kama zawadi kwenye harusi yetu mwezi Julai mwaka 2004 (8 years ago) mpaka leo haijawahi kupata tatizo lolote. Na ukiiona utafikiri tumeinunua mwezi uliopita.
 
Nimekubali kuliwa ila hawanipati tena!

Pole sana kagosaki. mimi nina friji ya west point niliinunua tangu mwaka 1998, sijawahi kuifanyia matengenezo na haijawahi kunikwamisha hata mara moja.
 
Siku hizi kuna bidhaa feki. Mimi fridge ya ZEC niliyonunua mtumba kariakoo mwaka 2006 ni nzima and has never been serviced todate. Ila hii ya WESTPOINT wameniingiza mjini.
 
Jamani napenda kuwatahadharisha kwamba muwe makini sana na bidha zinazotengenezwa na kampuni ya WESTPOINT. Nilinunua fridge mpya hivi karibuni Quality Plaza. Baada ya wiki moja ikaharibika pamoja na kuwa na fridge guard. Nikaipeleka service, baada ya wiki moja ikaharibika tena. Kwenye service bay ya kwao, nilikutana na watu wengi akiwemo mama mmoja alienunua jiko la umeme. Alipofika nyumbani kwake na kulichomeka, lilimrusha vibaya na kuzima umeme nyumba nzima. Wengine walinunua vifaa vingine na kupata matatizo ndani ya wiki mbili. Nendeni mkajionee wenyewe pale service bay yao iliyoko jengo la blue kwenye makutano ya barabara ya kurasini na nyerere road, opposite Pegasus house. Sijui kama TBS wanafanya kazi yao vizuri....


Labda ni hizo za Quality Plaza Kagosaki
mimi nina fridge ya westpoint tangu 2007 sipata taabu nayo....vinginevyo useme tu TBS wamelala bidha nyingi feki zinaingia nchini na sio westpoint peke yake!
Pia tuwe na tabia ya kuwashughilia kisheria wanatuuzia vimeo na kutusababishia matatizo
 
Kweli MAMA D, nimepata hasara sana maana hilo fridge hadi leo halifanyi kazi...TBS wamelela mno.
 
Hivi hawa TBS hawana kitengo cha kupokea malalamiko kutoka kwa walaji? Maana hawa wauzaji wa bidhaa bandia wanapata nguvu kwa kuwa kila anayeumizwa analilia upande wake na machozi yanakwenda na maji tu.

Pole mkuu, Westpoint si mbaya sana hata maofisini tunazitumia kwa muda mlefu tu, na unajuwa matumizi ya wengi yalivyo, kifaa kikidumu ujuwe cha ukweli.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom